Allah ametuumba na kutuweka katika dunia hii ili atujaribu na kutupa mitihani, kama alivyosema kuwa: «Yeye ndiye aliyeumba kifo na uhai ili akujaribuni; Ni nani miongoni mwenu mwenye matendo mazuri sana?». (Sura Almulk, aya 2). Mwenye kuamini na akawa mwenye kumuogopa Allah ataingia peponi, na atakaye chagua upotevu na upotokaji ataingia motoni. Uhai wa binadamu katika maisha haya vyovyote utakavyokuwa mrefu utafikia kikomo na utaondoka. Uhai wa milele na wa kudumu ni wa Akhera, kama Allah alivyosema kuwa: «Na kwa yakini, nyumba ya Akhera ndio maisha hasa laiti wangekuwa wanajua». (Sura Al-ankabuut, aya 64). Kiumbe bora zaidi kwa Allah ni Mtume, swallahlahu alayhi wasalam. Allah amemuambia kuwa: Utakufa kama wanavyo kufa watu wengine, na watu wote watakusanywa mbele ya Allah Siku ya Kiama ili awahukumu. «Kwa yakini, wewe utakufa na wao watakufa. Kisha nyinyi Siku ya Kiama mtashitakiana mbele ya Mola wenu». (Sura Azzumar, aya 31). Mtume, swallahlahu alayhi wasalam, ametuelez...