UHAKIKA WA KUFA NA UHAI

Allah ametuumba na kutuweka katika dunia hii ili atujaribu na kutupa mitihani, kama alivyosema kuwa: «Yeye ndiye aliyeumba kifo na uhai ili akujaribuni; Ni nani miongoni mwenu mwenye matendo mazuri sana?». (Sura Almulk, aya 2). Mwenye kuamini na akawa mwenye kumuogopa Allah ataingia peponi, na atakaye chagua upotevu na upotokaji ataingia motoni.
Uhai wa binadamu katika maisha haya vyovyote utakavyokuwa mrefu utafikia kikomo na utaondoka. Uhai wa milele na wa kudumu ni wa Akhera, kama Allah alivyosema kuwa: «Na kwa yakini, nyumba ya Akhera ndio maisha hasa laiti wangekuwa wanajua». (Sura Al-ankabuut, aya 64).
Kiumbe bora zaidi kwa Allah ni Mtume, swallahlahu alayhi wasalam. Allah amemuambia kuwa: Utakufa kama wanavyo kufa watu wengine, na watu wote watakusanywa mbele ya Allah Siku ya Kiama ili awahukumu. «Kwa yakini, wewe utakufa na wao watakufa. Kisha nyinyi Siku ya Kiama mtashitakiana mbele ya Mola wenu». (Sura Azzumar, aya 31).
Mtume, swallahlahu alayhi wasalam,  ametuelezea hali ya dunia na ufupi kwa kuilinganisha na Akhera kwamba ni kama msafiri aliyepumzika na kulala kidogo chini ya kivuli cha mti kisha akaondoka na kuuacha mti huo. (Tirmidhiy, Hadithi Na. 2377. Ibnumaja, Hadithi Na. 4109)
Allah pia ametusimulia kisa cha Mtume Yakubu, Allah amfikishie amani, alipokuwa akiwausia watoto wake na kusema: «Hakika, Allah amekuchagulieni dini. Basi msife isipokuwa tu mtakapokuwa Waislamu». (Sura Albaqara, aya 132).
Ikiwa mtu hajui ni lini uhai wake ambao Allah amempangia utamalizika na wapi na hakuna yeyote anayeweza kubadilisha, basi ni wajibu kwa mwenye akili kuhakikisha kuwa siku na saa za maisha yake anazijaza mambo ya kheri na wema, kwa sababu hali ilivyo ni kama Allah alivyosema kuwa: «Ukifika muda wao, basi hawatakawizwa hata kidogo na wala hawatawahishwa». (Sura Al-aaraaf, aya 34).
Kila aliyekufa kwa roho yake kutoka katika kiwiliwili chake, basi Kiyama chake kimefika na safari yake ya Akhera ameianza, safari ambayo ni miongoni mwa elimu ya visivyo onekana kwa macho na ambavyo akili ya mwanadamu haiwezi kujua ufafanuzi wa marefu na mapana yake. (Tazama uk. 77)
Kama ambavyo sheria imezingatia hukumu na maadili kwa mwanadamu kuanzia kuzaliwa kwake, kukua kwake na utoto wake, imetuwekea pia maadili na sheria ambazo zinalinda haki za maiti na zinazingatia hali za familia yake na ndugu zake. Shukurani kwa Allah ambaye ameifanya dini kuwa kamilifu, ametimiza neema na ametuongoza katika kuifuata dini hii tukufu. 
Dunia ni msafara mfupi wa kulekea Akhera.

Wakati wa kuwa mahututi

Inatakiwa kwa anayemtembelea mgonjwa amuombee kupona na kupata uzima, na kwamba kuuguwa kwake iwe sababu ya kufutiwa dhambi, kama Mtume,swallalahu alayhi wasalam, alivyokuwa akimwambia mgonjwa kwamba: «Si ubaya. Ni kisafishaji, Allah akitaka». (Bukhari, Hadithi Na. 3616).
Ni wajibu kwake: kuchagua maneno na matamshi ambayo yatamsaidia mgonjwa katika kupambana na ugonjwa na kupata matumaini ya kupona, kutumia fursa muafaka kwa ajili kulingania kwa Allah na kumkumbusha mgonjwa juu ya Allah na Siku ya Kiama kwa kutumia hekima na mawaidha mazuri. Mtume,swallalahu alayhi wasalam, ameweka mfano mkubwa sana wa jambo hilo, kama Swahaba mmoja anavyo tusimulia kwamba: «Kijana mmoja wa Kiyahudi ambaye alikuwa mtumishi wa Mtume aliugua. Mtume alikwenda kumjulia hali na kukaa mbele ya kichwa chake. Alimwambia: Ingia katika Uislamu. Kijana akamuangalia baba yake ambaye naye alikuwepo mbele yake. Baba yake akamuambia: Mtii Baba Kasimu. Kijana akaingia katika Uislamu. Mtume aliondoka huku akisema kwamba: «Shukurani anazistahiki  Allah ambaye amemuokoa huyu kijana asiingie motoni». (Bukhari, Hadithi Na. 1260). 
Zikianza kuonekana kwa mgonjwa dalili za kukaribia kufa, ni jambo linalo pendekezwa kumtamkisha na kumhimiza kulitamka Tamko la Tauhidi na ufunguo wa peponi (Laa Ilaaha Illallah = Hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah tu) kwa hekima na busara nzuri. Mtume,swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Watamkisheni maiti wenu Laa Ilaaha Illallah». Muslim, Hadithi Na. 916)
Hilo ni neno kubwa sana miongoni mwa maneno ambayo mtu anayatamka wakati wa uhai wake na wakati wa kufa kwake. Mtu ambaye atawezeshwa neno hilo likawa matamshi yake ya mwisho, atakuwa amepata heshima kubwa sana, kama Mtume,swallalahu alayhi wasalam, alivyosema kuwa: «Mtu ambaye maneno yake ya mwisho duniani ni Laa Ilaaha Illallah, ataingia peponi». (Abuudaud, Hadithi Na. 3118).

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU