Posts

Showing posts with the label islam

Kwa nini Uislamu ni dini ya kweli?

Image
“Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio pewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi ulio kuwa baina yao. Na anaye zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.”   Qur’an, Familia ya Imran (Aal-i Imran); 19 (3: 19) Dini inamaanisha  “malipo kwa mtindo wa malipo au adhabu”  na inaeleza uhusiano kati ya mfuasi na kiongozi mwenye madaraka. Kama neno lenyewe lilivyo, umetolewa ufafanuzi kadhaa wa neno dini. Zipo tofauti za kimsingi kati ya fafanuzi zinazotolewa na wanasayansi wa Kimagharibi (Ulaya) na wanazuoni Waislamu. Bado, kuna tofauti za kimsingi kati ya rai za pande zote mbili kuhusu chanzo cha dini na njia yake ya kimsingi ya kutokea.  Kwa mujibu wa rai ya Kiislamu, dini inamaanisha ukamilifu wa kanuni unaomwongoza mwanadamu ili aweze kuishi kulingana na lengo aliloumbiwa na ili atambue lengo hilo katika nidhamu mahusussi. Dini ni msingi unaorekebisha uhusian...

MWENYEZI MUNGU NI MMOJA WA KWELI KATIKA QUR-AN TUKUFU.

Image
Amesema Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anaye fanana naye hata mmoja). (Surat Ikhlas 1-4). (Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipo kuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu). (Surat Ambiyaa 25). (Kwa hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa Utatu. Hali hakuna mungu ila Mungu Mmoja. Na ikiwa hawaachi hayo wanayo yasema, kwa yakini itawakamata adhabu chungu wale wanao kufuru). (Surat Maida 73). (Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja). (Surat Sswafaat 4). (Au nani anaye uanzisha uumbaji, kisha akaurejesha? Na nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema: Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema kweli). (Surat Nnamli 64). Kwa hakika ujumbe huu (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) ndiyo mada ya msingi ndani ya Qur-an Tukufu HITIMISHO Kwa hakika dalili hizi na nyinginezo nying...

MWENYEZI MUNGU NI MMOJA WA KWELI KATIKA

Image
(Agano la kale): " Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. (Kumbukumbu la torati 6:4). "Je! Mwenyezi Mungu mmoja hajatuumbia roho ya maisha na kuturuzuku"?. (Malaki 2:15). " Ninyi ni mashahidi wangu, asema Bwana, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine. Mimi, naam, mimi, ni Bwana, zaidi yangu mimi hapana mwokozi ". (Isaya 43:10-11). " Bwana, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, Bwana wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu. "?. (Isaya 44:6). " Hubirini, toeni habari; naam, na wafanye mashauri pamoja; ni nani aliyeonyesha haya tangu zamani za kale? Ni nani aliyeyahubiri hapo zamani? Si mimi, Bwana? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi; Mungu mwenye haki, mwokozi; hapana mwingine zaidi ya mimi. (Isaya 45:21). Je! Unakumbuka dalili nyingine kama hizo....