Posts

Showing posts from December, 2019

Mwanaume Adaiwa Kuuwawa kwa Kupigwa Nyundo

Image
Na Amiri kilagalila Njombe TAZAMA VIDEO HII KISHA SUBSCRIBE YOUTUBE Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Sosteni Myamba (44) mkazi wa kijiji cha Itipingi halmashauri ya wilaya ya Njombe mkoani Njombe inasemekana ameuawa kwa kupigwa nyundo kwa madai ni kutokana na imani za kishirikina. Mwenyekiti wa kijiji cha Itipingi Ayubu Mgeni amethibitisha hilo na kufafanua kuwa marehemu huyo alikuwa na tabia ya kuwatuhumu baadhi ya ndugu akiwemo baba yake mzazi kuwa ni mshirikina hali ambayo imepelekea kuibuka kwa mgogoro ndani ya familia hiyo. Kiongozi wa familia hiyo Aidani Myamba amesema marehemu  alikuwa ana matatizo ya akili hali ambayo ilimfanya awe mtu wa kutuhumu wengine kuwa wanajihusisha na imani za kishirikina. Hata hivyo Jacob Myamba ambaye ni mdogo wa marehemu huyo anashikiliwa na jeshi la polisi wilaya ya kipolisi makambako kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.

Rais Macron Auita Ukoloni Kuwa ni Kosa kubwa

Image
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameungana na mataifa mengine manane ya Afrika Magharibi kutangaza mabadiliko makubwa ya sarafu moja ya kikanda ikiwa ni pamoja na kuondoa mahusiano ya sarafu hiyo na Ufaransa. TAZ\AMA VIDEO HII KISHA SUBSCRIBE YOUTUBE Macron, akiwa mjini Abidjan amesema ukoloni barani Afrika ulikuwa ni kosa kubwa lililofanywa na Ufaransa, huku akitoa mwito wa kuanzishwa mahusiano mapya na Ufaransa. Haikuwa mara ya kwanza kwa Macron kuelezea majuto hayo kwa niaba ya Ufaransa kuhusiana na enzi za ukoloni. Wakati wa kampeni za urais, alipamba vichwa vya habari pale alipoufananisha ukoloni wa Ufaransa nchini Algeria kuwa ni uhalifu dhidi ya ubinaadamu. Ziara ya Macron nchini Ivory Coast inakuja wakati viongozi wa kikanda walipokutana kutangaza kubadilisha jina la sarafu hiyo ya Faranga ya CFA.

Naibu Waziri wa Ardhi Aagiza Wadaiwa NHC Kuchululiwa Hatua

Image
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amekutana na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa saa nne na kulitaka shirika hilo kuhakikisha kufikia Januari 2020 inawachukulia hatua wapangaji wote wa Shirika hilo wanaodaiwa kodi inayofikia bilioni 8.23. TAZAMA VIDEO HII KISHA SUBSCRIBE YOUTUBE Dkt Mabula alikutana na Menejiment ya Shirika hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam ikiwa ni mkakati wake wa kulifanya Shirika la Nyumba la Taifa kuimarika kimapato pamoja na kufanya kazi zake kwa ufanisi. Alisema, katika kuifanya NHC inaimarika kimapato ni lazima madeni kutoka kwa wapangaji wake yanakusanywa kwa kuanzisha opreresheni maalum inatakayowezesha kutambuliwa wadaiwa wote wa kodi ili waweze kulipa kwa wakati. ‘’Ukiacha zile taasisi za serikali, wote wanaodaiwa ikifika januari 2020 wafikishwe kwenye vyombo vya sheria na zile taasisi za serikali mkamuone Katibu Mkuu HAZINA ili taasisi hizo zikatwe fedha moja kwa mo...

Zanzibar: Afariki kwa Mchezo wa ‘Spot Honda’ Baharini

Image
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Nasibu Omar Hafidhi mwenye umri wa miaka 35 mkaazi wa Michamvi amefariki dunia baada ya kuzama baharini wakati akiogelea kwa kutumia sport honda ya baharini. TAZAMA VIDEO HII KISHA SUBSCRIBE YOUTUBE Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Hassan Suleiman amesema tukio hilo la kuzama kwa marehemu huyo limetokea tarehe 17 ya mwezi huu majira ya saa 12 jioni huko bahari ya Michamvi. Aidha kamanda Suleiman ametoa wito kwa jamii na wale wanaocheza michezo hiyo ya baharini kuwa makini na michezo yao na kuchukua uangalizi kwa wale ambao bado hawajaifahamu vizuri michezo hiyo. Bunge laridhia Trump kushtakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka, urais wake ‘rehani’ Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi katika hospitali kuu ya Cottege Makunduchi na daktari bigwa na kukabidhiwa jamaa zake kwaajili ya mazishi.

Wanaume Zanzibar WATOA Talaka Kwa Njia ya SMS, Elimu ya Ndoa Yahitajika zaidi

Image
Wanaume visiwani Zanzibar wanadaiwa kutoa talaka kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi (SMS), kitendo kinachotafsiriwa kuwa ni dharau na kinyume cha Mila na Desturi za Zanzibar TAZAMA VIDEO HII KISHA SUBSCRIBE YOUTUBE Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan Juma amewataka wanandoa watarajiwa kuepuka talaka za kiholela ambazo athari zake ni kubwa katika jamii ikiwamo kutelekezwa kwa familia na watoto kutaabika Alisema utoaji wa talaka kiholela kwa kiasi kikubwa unadhihirisha kwamba watu wanaingia katika ndoa bila ya kupata elimu juu ya ndoa na familia 

Muuguzi Adaiwa Kubaka Mjamzito Chumba Cha Kujifungulia

Image
MKAZI wa Kijiji cha Majimoto wilayani Mlele mkoani Katavi, jina lake limehifadhiwa mwenye umri wa miaka 22, anadaiwa kubakwa na muuguzi wa   wa kituo cha afya Mamba, Abednego Alfred (32), wakiwa ndani ya chumba cha  kujifungulia. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi,Benjamin Kuzaga  alisema tukio hilo la kinyama na la kikatili  lilitokea Desemba  18, mwaka huu saa 2 usiku katika chumba cha kujifungulia wajawazito.  Alisema siku ya tukio, mwanamke huyo  alipatwa na uchungu wa kujifungua baada ya siku zake kutimia, alitoka nyumbani kwake Majimoto  kwenda kupata huduma kituoni hapo, huku akisindikizwa na mama yake mzazi . Baada ya kufika kituoni alipokelewa na    Alfred ambaye aliyekuwa muuguzi wa zamu siku hiyo. Alisema muuguzi alianza kumpatia huduma ya uzazi, lakini mwathirika wa tukio hilo alihisi  hali isiyo ya kawaida  sehemu zake za siri...

NAMNA YA KUSWALI

Image
Nia: Nia ni sharti la swala kuwa sahihi, kwa maana ya mtu kukusudia kwa moyo wake kumuabudu Allah kwa kuswali, huku akijua kwamba swala anayoswali ni Magharibi kwa mfano au Isha. Haitakiwi na sheria kuitamka hii nia, bali makusudio ya moyoni na akilini ndio yanayotakiwa. Kuitamka Nia ni jambo ambalo hilo halikuthibiti kunukuliwa kwa Mtume,swallalahu alayhi wasalam, wala maswahaba wake watukufu. Atasimama wima kwa ajili ya swala na kusema: (Allahu Akbar). Atanyanyua mikono yake mpaka usawa wa mabega yake au juu yake huku matumbo ya viganja vya mikono akiyaelekeza upande wa Kibla. Takbira haiwi sahihi isipokuwa tu kwa tamko hili la (Allahu Akbar). Maana yake ni kumtukuza na kumuadhimisha Allah. Allah ni mkubwa zaidi kuliko kila kisichokuwa yeye. Ni mkubwa zaidi kuliko dunia pamoja na starehe zote na matamanio yote yaliyomo humo. Tunaziweka kando starehe zote hizo na tunaelekea kwa Allah mkubwa, mtukufu katika swala kwa nyoyo zetu na akili zetu huku tukiwa wanyenyekevu. ...

Ni ipi dini ya mwisho ya Mwenyezi Mungu?

Image
Wanazuoni wa Kiislamu wanagawanya dini katika makundi makuu mawili: 1.  Dini za kweli. 2.  Dini potovu. Dini zenye msingi wa kumwamini Mungu mmoja na kuwaamuru watu kumwabudu na kumtii Yeye tu zinaitwa  "dini za kweli" . Dini za kweli zilizotoka kwa Allah. Kwa hivyo, pia zinaitwa dini zinazotoka mbinguni.  Dini ya kweli  pia huitwa  "dini ya upwekeshaji"  kwasababu zina msingi wa kumpwekesha Allah na kumwabudu Yeye tu.  Dini ambazo hazikuteremshwa na Allah, zilizoundwa na watu na hazina msingi wa kumwamini Mungu mmoja zinaitwa  "dini potovu" . Baadhi ya dini za kweli zilipotoshwa na watu baadaye; na ushirikina na imani potovu ambazo hapo mwanzoni hazikuwepo ziliongezwa baadaye. Dini zilizokuwa za kweli hapo mwanzoni lakini baadaye zikabadilishwa zinaitwa  "dini zilizogeuzwa" ; mathalani, Uyahudi na Ukristo. Dini ya kwanza kwa wanaadamu ni ya upwekeshaji iliyokuwa na msingi wa kumwamini Mungu mmoja, iliyoteremshwa kwa Adam,...

Ni zipi tofauti kuu kati ya Uisilamu na Ukristo wa leo?

Image
1.  Katika Ukristo, ipo imani ya utatu lakini katika Uisilamu, kuna imani ya kumpwekesha Allah. 2.  Uisilamu unahusisha dini zote za mbingu na mitume; Ukristo unaikubali Biblia tu kuwa ndio kitabu cha kweli; hauikubali Quran kuwa ndio kitabu kilichotegemea ufunuo. 3.  Ukristo unadai kuwa binadamu ni mwen ye dhambi ya kuzaliwa nayo na kwa ajili hiyo, lazima abatizwe ili atakaswe; Uisilamu unaeleza kuwa watu wote wanazaliwa wakiwa hawana makosa na kwamba hakuna mtu anayebeba dhambi ya mtu mwengine. 4.  Katika Ukristo, mapadri na viongozi wa dini wana mamlaka ya kusamehe makosa ya watu wanapokiri; katika Uisilamu, madhambi husamehewa na Allah pekee. 5.  Katika Ukristo, maneno ya Yesu yanazingatiwa kuwa ni maneno ya Mungu; katika Uisilamu, amri za kiungu zinafikishwa kupitia ufunuo na Jibril. 6.  Kwa mujibu wa Wakristo, Yesu alisulubiwa. Kwa mujibu wa Uisilamu, alipaishwa mbinguni, kwa Allah. 7.  Ingawa Wakristo wa leo wanadai kuwa dini yao...

Kwa nini Uislamu ni dini ya kweli?

Image
“Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio pewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi ulio kuwa baina yao. Na anaye zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.”   Qu r’an, Familia ya Imran (Aal-i Imran); 19 (3: 19) Dini inamaanisha  “malipo kwa mtindo wa malipo au adhabu”  na inaeleza uhusiano kati ya mfuasi na kiongozi mwenye madaraka. Kama neno lenyewe lilivyo, umetolewa ufafanuzi kadhaa wa neno dini. Zipo tofauti za kimsingi kati ya fafanuzi zinazotolewa na wanasayansi wa Kimagharibi (Ulaya) na wanazuoni Waislamu. Bado, kuna tofauti za kimsingi kati ya rai za pande zote mbili kuhusu chanzo cha dini na njia yake ya kimsingi ya kutokea.  Kwa mujibu wa rai ya Kiislamu, dini inamaanisha ukamilifu wa kanuni unaomwongoza mwanadamu ili aweze kuishi kulingana na lengo aliloumbiwa na ili atambue lengo hilo katika nidhamu mahusussi. Dini ni msingi unaorekebisha uhusia...

Haki Za Kinidhamu Za Mume

Image
Ingawaje mume na mke ambao hutengeneza maisha ya pamoja ya familia, hugawana na kushirikiana katika kuendesha mambo ya nyumba yao, wanaweza kuwa na maoni tofauti kuhusu mambo fulani. Mwanaume anaweza kuhisi kwamba ni yeye ndiye anayetakiwa kuwa na uamuzi wa mwisho kuhusu mambo ya familia, bila kupata upinzani kutoka kwa mke wake. Wakati huo huo mke wake anaweza akakataa kazi yake kama upande uliomtiifu. Ubishi na ugomvi unaweza ukaanza kwa sababu kila upande unajaribu kuanzisha mamlaka juu ya upande mwingine. Suluhu nzuri zaidi ya tatizo kama hili ni kwamba pande zote zinatakiwa kuacha kujionesha kama unao mamlaka makubwa zaidi kuzidi upande mwingine, na kujaribu kupata ufumbuzi wa matatizo yao kwa njia ya mazungumzo na uelewano wa kina. Hii inawezekana tu kufanikiwa kama pande zote zinaacha ukaidi. Baadhi ya wanamume huwaamuru wake zao kufanya mambo mengi na kama wakikabiliwa na upinzani, wanadhani ni sahihi kuwashika, kuwaadhibu au hata kuwapiga wake zao. Msimamo huu si sahi...