Zanzibar: Afariki kwa Mchezo wa ‘Spot Honda’ Baharini

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Nasibu Omar Hafidhi mwenye umri wa miaka 35 mkaazi wa Michamvi amefariki dunia baada ya kuzama baharini wakati akiogelea kwa kutumia sport honda ya baharini.

  • TAZAMA VIDEO HII KISHA SUBSCRIBE YOUTUBE

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Hassan Suleiman amesema tukio hilo la kuzama kwa marehemu huyo limetokea tarehe 17 ya mwezi huu majira ya saa 12 jioni huko bahari ya Michamvi.

Aidha kamanda Suleiman ametoa wito kwa jamii na wale wanaocheza michezo hiyo ya baharini kuwa makini na michezo yao na kuchukua uangalizi kwa wale ambao bado hawajaifahamu vizuri michezo hiyo.

Bunge laridhia Trump kushtakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka, urais wake ‘rehani’
Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi katika hospitali kuu ya Cottege Makunduchi na daktari bigwa na kukabidhiwa jamaa zake kwaajili ya mazishi.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

Kisa Cha Nabii Ibraahiym عليه السلام - Sehemu Ya 1