HAKIKA YA DUA
Dua ni hakika ya kuabudu na kuonesha dalili mahususi za kuabudu ambazo ni kukimbilia na kujisalimisha kwa Allah Mtukufu. Allah amesema kuwa: «Na Mola wenu amesema kuwa: Niombeni nitakujibuni. Kwa yakini, wale wanaofanya kiburi cha kuacha kuniabudu (kuniomba) wataingia motoni wakiwa dhalili». (Sura Ghaafir, aya 60) Allah Mtukufu ni Mkarimu zaidi ya Wakarimu. Kwa hiyo, mja anapojipeleka kwake hujibu maombi yake na kumpa kwa sababu ya kujinyongesha kwake. Mtume amesema kuwa: «Kwa yakini, Mola wenu ni mwenye haya, mkarimu. Anaona haya mja wake anaponyanyua mikono yake kwake kuirudisha ikiwa sifuri (mitupu)». (Abudaudi 1488 ) Je, Allah anawajibu wote waombao? Allah amemuahidi anaye omba kwa njia sahihi bila ya dhuluma au kuwaonea wengine kwamba atamjibu. Amesema kuwa: «Na wanapo kuuliza waja wangu kuhusu mimi, kwa yakini kabisa mimi niko karibu, ninajibu dua ya mwenye kuomba aniombapo». (Sura Albaqara, aya 186) Lakini kujibu huku kuna aina kadhaa ambazo Mt...