BAADA YA KUFA

Mauti yakithibitika na mwili ukatengana roho, inapendekezwa yafanyike mambo kadhaa. Miongoni mwa hayo ni haya yafuatayo:
  1. Kuyafumba macho ya maiti kwa upole kwa kuonesha heshima kwake.
  2. Kuwa na subira, kujidhibiti na kutojachia kwa kupaza sauti za vilio na kuomboleza na kuwahimiza familia na ndugu wa marehemu wawe na subira. Mtume, swallahlahu alayhi wasalam, alimuamrisha mmoja wa binti zake pale mtoto wake alipokufa kwamba awe na subira na kutegemea malipo kwa Allah. (Bukhari, Hadithi Na.1284. Muslim, Hadithi Na. 923)
  3. Kumuombea marehemu rehema na kusamehewa dhambi, na kuwaombea ndugu zake subira na faraja
    Mtume, swallahlahu alayhi wasalam, alifanya hivyo pale alipohudhuria kifo cha Abuusalama, Allah amuwiye radhi, mmoja wa Maswahaba watukufu. Aliingia nyumbani kwake huku Abuusalama akiwa ameshakufa na macho yake yakiwa wazi. Aliyafumba kisha akasema: «Hakika, inapotolewa roho macho yanaifuatilia». Sauti za familia yake zikalipuka kwa kilio na kulalama. Mtume akasema: «Msijiombee isipokuwa kheri tu, kwa sababu Malaika wanaitikia Aamiin kwa mnayoyasema». Kisha akasema: Ewe Mola wangu, msamehe Abuusalama na inyanyue hadhi yake awe pamoja na walio ongoka, na muwekee mbadala katika familia yake iliyo baki, na tusamehe sisi na yeye Ewe Mola wa walimwengu, na mpanulie kaburi lake lisimbane, na muwekee mwangaza humo». (Muslim, Hadithi Na. 920).
  4. Kufanya haraka kumuandaa maiti; kumuosha, kumsalia na kumzika. Mtume, swallahlahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mfanyieni haraka maiti. Kama ni wa kheri, basi ni kheri mnakompeleka, na kama hayuko hivyo basi ni shari mnayojiepusha nayo». (Bukhari, Hadithi Na. 1315. Muslim, Hadithi Na. 944).
  5. Kuwasaidia wafiwa kwa kuwafanyia baadhi ya majukumu yao. Mtume, swallahlahu alayhi wasalam, aliamrisha kiandaliwe chakula familia ya Jafar Bin Abitaalib mtoto wa ami yake pale Jafar alipouawa. Mtume alisema: «Iandalieni chakula familia ya Jafar, kwani wamefikwa na jambo lenye kuwashughulisha». (Abudaud, Hadithi Na. 3132. Tirmidhiy, Hadithi Na. 998.   Ibnumaja, Hadithi Na. 1610).  
Ni suna kufunika macho ya maiti wakati wa kufa kwake.  

Kumuosha maiti

Ni wajibu maiti kuoshwa kabla ya kuvishwa sanda na kuzikwa. Anatakiwa amuoshe maiti mmojawapo wa watu wa familia yake au ndugu zake wa karibu au Muislamu yeyote. Mtume, swallahlahu alayhi wasalam, pamoja na kuwa yeye ni twahara aliyetwaharishwa lakini alipokufa alioshwa.

Namna ya kuosha

Inatosha katika kumuosha maiti kumwagia maji mwili wote, na kusafisha Najisi kama ipo, pamoja na kusitiri sehemu zake za siri wakati wa kumuosha.
Ni vizuri mambo yafuatayo yazingatiwe:
Mwili wa maiti unatakiwa kuenezwa maji pamoja na kujali kusitiri sehemu zake za siri.
  1. Ni vizuri mambo yafuatayo yazingatiwe
  2.  Muoshaji avae kitu mkononi mwake wakati wa kuosha sehemu za siri za marehemu.
  3. Ataanza kwa kusafisha uchafu na najisi kwa marehemu.
  4. Kisha ataosha viungo vya Udhu kwa utaratibu unaoeleweka.
  5. Kisha ataosha kichwa na sehemu nyingine za mwili. Ni vizuri kumuosha maiti kwa mkunazi (majani ya mti wa mkunazi) au kwa sabuni, kisha atammwagia maji baada ya hapo.
  6. Inapendekezwa kuanza kumuosha upande wa kulia kisha wa kushoto.
  7. Ni vizuri kurudia kuosha mara tatu au zaidi kama ikihitajika kufanya hivyo. Mtume, swallahlahu alayhi wasalam, aliwaambia wale wanawake waliokuwa wakimuosha Zainab, binti yake kwamba: «Muosheni mara tatu au mara tano au zaidi ya hapo ikiwa mnaona kuwa inahitajika kufanya hivyo». (Bukhari, Hadithi Na. 1195).
  8. Inawezekana kuweka kitambaa au pamba na mfano wake katika sehemu za siri, masikioni, puani na mdomoni ili kuzuia isitoke damu au Najisi.
  9. Inapendekezwa kumuweka maiti manukato wakati wa kumuosha na baada ya kumuosha. Mtume, swallahlahu alayhi wasalam, aliwaamrisha wanawake waliokuwa wakimuosha binti yake Zainab kwamba katika hatua ya mwisho ya kuosha waweke Kafuri (aina ya manukato). 
Inapendekezwa kumuosha maiti kwa kutumia majani makavu ya mti wa Mkunazi yaliyochanganywa na maji au kwa sabuni yoyote au kwa kitu chochote cha usafi kisichokuwa na madhara. 

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

Kisa Cha Nabii Ibraahiym عليه السلام - Sehemu Ya 1