Posts

Tamko la Marekani juu ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hapa nchini

Image

Mama aliyevunjwa mkono kuchangiwa fedha mbele ya Rais Magufuli

Image
Rais John Magufuli alipowaamuru viongozi watendaji wa Kahama kumchangia mama aliyekuwa akitwanga kokoto kisha kuvunjwa mkono na mtuhumiwa aliyefahamika kwa jina la Daudi ambaye alimpiga na kumvunja mkono huku vyombo vya ulinzi na usalama vikishindwa kumchukulia hatua na kumsaidia. Rais Magufuli amesema amefanya hivyo ili viongozi hao wajifunze kushughulikia malalamiko ya wananchi badala ya kumsubiri yeye barabarani. Kila kiongozi mtendaji aliamuriwa kumchangia shilingi 50,000 na kufanikiwa kupata shilingi 500,000 papo hapo.

Bibi wa miaka 75 abakwa, auawa

Image
Jeshi la Polisi nchini Kenya linachunguza tukio la kubakwa na kuuawa kwa ajuza mwenye umri wa miaka 75 mkaazi wa Kijiji cha Kiandegwa, Kaunti ya Kirinyanga. Kwa mujibu wa taarifa za awali za jeshi hilo, ajuza huyo alitupwa kilometa kadhaa kutoka nyumbani kwake. Imeelezwa kuwa alikuwa peke yake nyumbani wakati ambapo wabakaji hao walipovamia na kutekeleza unyama dhidi yake. “Tunasadiki kuwa mwanamke huyo alibakwa kabla ya kuuawa na mwili wake kutupwa mbali na nyumba yake,” alisema Chifu Geoffrey Mithamo, kiongozi wa eneo la Wamumu. Kijana wa kiume wa bibi huyo amewaambia waandishi wa habari kuwa walipewa taarifa na majirani na kwamba walishtushwa na taarifa hizo kwakuwa walikuwa wamezungumza na mama yao siku moja kabla. “Tulishtushwa sana na taarifa hizo kwa sababu tulikuwa na mazungumzo marefu na yeye Jumapili majira ya saa nne usiku,” alisema kijana huyo. Wapelelezi kutoka kituo cha polisi cha Sagana walifika katika eneo la tukio Jumatatu, majira ya saa sita na nusu mchana na w...

Sehemu Ya Kwanza: Wajibu Wa Wanawake

Image
Madhumuni ya ndoa Ndoa ni haja ya kawaida kwa kila mwanadamu. Inayo manufaa mengi na mazuri, baadhi ya hayo manufaa mengi na mazuri yaliyo muhimu ni haya: Ujengaji wa familia ambayo kwayo mtu anaweza kupata usalama na utulivu wa akili. Mtu ambaye hakuoa au kuolewa hufanana na ndege asiye na kiota. Ndoa hutoa huduma ya hifadhi kwa kila mtu anayehisi amepotea kwenye maisha yasiyo na mpango; mtu anaweza kupata mwenzi wa maisha ambaye anaweza kushirikiana naye katika furaha na huzuni. Matamanio ya kawaida ya kijinsia yana nguvu na yenye maana. Kila mtu anatakiwa kuwa na mwenzi kwa lengo la kujitosheleza kijinsia kwenye mazingira yaliyo salama na tulivu. Kila mtu anapaswa kufaidi raha mustarehe ya kijinsia katika namna iliyo sahihi na inayostahiki. Wale wanao jiepusha na ndoa mara kwa mara husumbuliwa na maradhi ya kimwili na kisaikolojia. Maradhi hayo na matatizo fulani ya jamii ni matokeo ya moja kwa moja ya vijana kujiepusha na ndoa. Uzazi: Kupitia kwenye ndoa, binadamu wanaen...