Posts

Kumridhisha Mume Wako Na Si Mama Yako

Image
Msichana anapokuwa nyumbani kwa wazazi wake anawajibika kuwaridhisha. hata hivyo, mara aolewapo, wajibu wake hubadilika. Anapokuwa nyumbani kwa mume wake, mwanamke lazima ayapatie kipaumbele mahitaji ya mume wake. Hata hapo ambapo matakwa ya mume wake na wazazi wake yanatofautiana lazima amtii mume wake, hata kama wazazi wake hawakuridhika. Kutomtii mume ni kitendo ambacho kinaweza kuharibu uhusiano wa ndoa ya mtu, na kinyume chake. Aidha, kinamama wengi hawafaidi ilmu sahihi na busara. Mama wengine, hawajatambua kwamba wanatakiwa kuwaacha mabinti zao wafikie maelewano na wanaume zao wenyewe. Wanandoa lazima waachwe wapange mambo yao wenyewe na kama wakipata tatizo lolote walitatue wao kwa kutumia uwezo wao. Kwa kuwa mama wa wake hawajui jambo hili, basi wao katika akili zao hujaribu kumfanya mkwe wao afuate wanavyotaka wao. Hujaribu kufanya hivyo moja kwa moja au kwa kuzunguka, kuingilia mambo yao ya familia. Wanawatumia mabinti zao ambao hawajapata uzoefu na hawafahamu viz...

Basi la Abood Lapata Ajali Dar

Image
BASI la abiria mali ya Kampuni ya Abood Bus Services Ltd, limepata ajali mbaya maeneo ya Kimara Temboji jijini Dar es Salaam, asubuhi ya leo, Jumatano, Oktoba 30, 2019. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanadai kuwa, basi hilo lilikuwa likitoka Stendi ya Mabasi, Ubungo Dar, kupitia Barabara ya Morogoro, baada ya dereva wa basi hilo kugonga gema, lilipolekea taili la basi hilo kupinda na kwamba hakuna abiria yeyote alijeruhiwa. Akizungumza leo Oktoba 30, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mussa Taibu, amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 2:00 asubuhi, huku chanzo akikitaja kuwa ni wembamba wa barabara hiyo ambayo kwa sasa ipo katika upanuzi. “Ni kweli kuna taarifa hizo kwamba, limeacha barabara katika barabara zetu hizi zinazofanyiwa matengenezo ya kupanuliwa, Basi limeinama na sio kama limepinduka na hakuna aliyeumia, njia ni nyembamba na hii njia kuna vigema vingi, kwahiyo Dereva katika kuingia, aliingia vibaya na tairi likalala na kupelekea Basi likainama” ames...

TMA yawataka wakulima kutumia vyema mvua za masikap

Image
Wakulima wa kanda ya kati inayohusisha Mikoa ya Dodoma, Singida na maeneo jirani wameshauriwa kuutumia vyema msimu wa mvua za masika zinazotarajiwa kuanza wiki ya kwanza hadi ya pili ya mwezi Novemba 2019. Ushauri huo umetolewa na Meneja wa Mamlaka ya hali ya hewa (TMA) kanda ya kati Izidor Kirenga jana, wakati akizungumzia juu ya ujio wa mvua hizo na kudai kuwa zitaendelea hadi wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Aprili 2020. Amesema tayari taarifa juu ya ujio wa mvua hizo imeshasambazwa kwa maafisa ugani wa maeneo mbalimbali ambao watakuwa na jukumu la kuwashauri wakulima kujiandaa na upandaji wa mazao mbalimbali ambayo yanastahimili hali ya hewa ya ukanda wa kati. “Mvua hizi za masika kwa ukanda wa kati yaani mikoa ya Singida na Dodoma zinatarajia kuanza wiki ya kwanza au ya pili ya mwezi Novemba 2019 kuendelea hadi wiki ya kwanza au ya pili ya mwezi April, 2020 hivyo kwa wakulima wazitumie vyema kupanda mazao,” amefafanua Kirenga. Amesema kwa kawaida maeneo ya kanda ya kati m...

Makonda awakabidhi Suma JKT ujenzi hospitali Ubungo

Image
Kitengo cha uzalishaji mali cha Jeshi la kujenga Taifa (suma JKT), kimepewa kazi ya kujenga hospitali ya wilaya ya Ubungo. Kazi hiyo wamepewa na jana Oktoba 29, 2019 na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ambaye amesema kuwa ujenzi huo unatakiwa kamilika kwa miezi mitatu. Amebainisha hayo jana alipotembelea eneo itakapojengwa hospitali hiyo Kimara Baruti, ambapo aliambatana na viongozi wengine na kuangalia jinsi maandalizi mbalimbali yalivyoanza kufanyika. Makonda ametoa shukurani zake kwa mara nyingine tena kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa kukubali ombi lake la sh 1.5 bilioni za ujenzi wa hospitali hiyo. ” Wilaya hii ni mpya inahitaji viongozi shupavu wa kuwaletea maendeleo, ni kazi ya viongozi wanaochaguliwa na wananchi. “Kwa bahati mbaya Ubungo ilipata viongozi wanaojali matumbo yao tu. Hata leo hapa hawapo ila kesho watakuja na maneno matamu ili muwape kura” Alisema Mkuu huyo wa mkoa. Mkurugenzi mtendaji wa Suma JKT, Kanali Rajabu Mabele amesema kuwa watahakikisha uje...

Mamlaka ya Hali ya Hewa yatoa tahadhari

Image
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA imetoa tahadhari ya kuwepo kwa mvua kubwa katika Mikoa ya Mwanza, Geita, Kagera na sehemu ya Mkoa wa Simiyu. Ikitoa utabiri huo wa siku tano kuanzia leo TMA imesema mvua hizo zitakazokuwa za wastani zinaweza kusababisha uharibifu wa barabara, madaraja na miundombinu mingine hivyo mamlaka zinazohusika zinatakiwa kuchukua tahadhari. Hivi karibuni TMA iliripoti juu ya kutokea kwa mvua Ukanda wa Pwani Mikoa ya Tanga, Visiwa vya Unguja na Pemba ambayo ilileta madhara ikiwemo vifo na uharibifu wa mali.

Kocha Yanga Mziki wa Pyramids Hatuwawezi

Image
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo amefunguka kuwa wapinzani wao Pyramids wako juu kuliko wao ambapo hawezi kulalamika kwa matokeo ambayo waliyapata walipokutana nao katika Kombe la Shirikisho Afrika. Zahera Jumapili iliyopita alishuhudia kikosi chake kikikubali kipigo cha mabao 2-1, mbele ya Waarabu Pyramids katika mchezo wa kusaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya Kombe hilo la Shirikisho Afrika. Kwa sasa Yanga wanajiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Pyramids ambayo itapigwa nchini Misri Novemba 3, huku wakihitaji ushindi wa mabao 2-0 kwa ajili ya kusonga mbele. Zahera ameliambia Championi Jumatano, kuwa hawezi kulalamika kwa ajili ya matokeo ambayo wameyapata kutoka kwa wapinzani wao kutokana na ukweli kuwa wapinzani wao wako juu kuliko wao. “Hii ni kama bahati mbaya ya kupoteza mchezo huu kama ambavyo ilitutokea kule Zambia tulipocheza na Zesco. Ukiangalia mabao ambayo wameyapata ni kama yale ya mchezo uliyopita na Zesco lakini hatuwezi kulalamika san...

DAWA DAWA ONGEZA UUME NDANI YA WIKI MOJA TU OKOA NDOA YAKO LEO

Image
DOKTA ;0673160865 TUNATIBU NA KUPONESHA KABISA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME UUME MDOGO? BUSHA BILA KUPASUA KISUKALI NA VIDONDA VYA TUMBO? asilimia kubwa ya wanaume wanaupungufu wa nguvu za kiume NA maumbile madogo NI NINI KINACHOSABABISHA UUME KUZIDI KUWA MDOGO NA WEMBAMBA 1 kuugua chango LA uzazi 2 unene kupita kiasi 3 kuvaa nguo au chupi za kubana 4 kupiga punyeto kwa mda mrfu ,NI NINI TIBA YAKE MAKAKANUA MIX nidawa ya mitishamba iliyochanganywa NA mizizi kumi NA mbili urfusha NA kunenepesha UUME saizi upendayo ich 5,6,7, NA 8 kwa urfu NA sentimita 3,4, na 5 ipo dawa ya kunywa na kupaka NI NINI KINASABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME 1 kupungukiwa kwa homoni ya testerone 2 kuhudhurika kwa Neva au uti wa mgongo 3 utumiaji holela wa madawa ya kizungu 4 usongo wa mawazo na asira 5 utumiaji wa vyakula vya mafuta mengi NI NINI TIBA YAKE MAPRO POWER NO 2 NDIO tiba tosha kwa sasa kwani utibu matatizo matatu kwa pamoja 1 itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 40 adi 60, MPAKA masaa2 ,2...