MWENYEZI MUNGU NI MMOJA WA KWELI KATIKA QUR-AN TUKUFU.
Amesema Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu:
(Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anaye fanana naye hata mmoja). (Surat Ikhlas 1-4).
(Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipo kuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu). (Surat Ambiyaa 25).
(Kwa hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa Utatu. Hali hakuna mungu ila Mungu Mmoja. Na ikiwa hawaachi hayo wanayo yasema, kwa yakini itawakamata adhabu chungu wale wanao kufuru). (Surat Maida 73).
(Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja).
(Surat Sswafaat 4).
(Au nani anaye uanzisha uumbaji, kisha akaurejesha? Na nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema: Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema kweli). (Surat Nnamli 64).
Kwa hakika ujumbe huu (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) ndiyo mada ya msingi ndani ya Qur-an Tukufu
HITIMISHO
Kwa hakika dalili hizi na nyinginezo nyingi katika kitabu kitakatifu na Qur-an Tukufu zinaonyesha yasiyokuwa na shaka ndani yake ya kwamba Mwenyezi Mungu ni mmoja hakuna mwingine zaidi yake, kitabu kitakatifu kinasema: " Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi. Yule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye ". (Marko 12:28-33).
Na Qur-an Tukufu inataja jambo hili katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
(Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee). (Surat Ikhlas: 1).
Na kitabu kitakatifu hakitilii mkazo ya kwamba Mwenyezi Mungu ni mmoja tu bali kinatilia mkazo pia ya kwamba Mwenyezi Mungu ndiye muumbaji na muokoaji pekee, "Ninyi ni mashahidi wangu, asema Bwana, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu
mimi hatakuwapo mwingine. Mimi, naam, mimi, ni Bwana, zaidi yangu mimi hapana mwokozi ". (Isaya 43:10-11).
Kwa sababu hiyo inabainika ya kwamba Uungu wa Issa (Yesu) au Roho mtakatifu au wengine tofauti na hao wawili hauna mashiko, wala dalili juu yake hawakuwa isipokuwa ni viumbe miongoni mwa viumbe wa Mwenyezi Mungu, hawana chochote katika maamrisho, wao si waungu wala hawafananishwi na Mungu. Hakuna kinacho fanan nae kwa mujibu wa kitabu kitakatifu na Qur-an Tukufu.
Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewakasirikia Mayahudi kwa sababu ya upotevu wao na kuabudu miungu tofauti pamoja na Yeye, "Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israili" (Hesabu 25:3), na akaharibu Mussa (s.a.w) ndama yao ya dhahabu.
Kwa upande mwingine wamepata adhabu na mateso baadhi ya wakristo waliokuwa wakimpwekesha Mwenyezi Mungu, yote hayo ni kwasababu wameamini tauhidi ya Mwenyezi Mungu na wakakataa kubadilisha mafundisho sahihi ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu ya Nabii Issa (s.a.w) na wakakanusha uzushi wa utatu mtakatifu ulioanzishwa na Paulo na wafuasi wake.
Muhtasari wa maneno Mwenyezi Mungu amemtuma Adam na Nuuh na Ibrahim na Mussa na Issa na Muhammad (s.a.w) kuwalingania watu katika imani ya kumuamini Mwenyezi Mungu na kumtakasia ibada yeye peke yake hana mshirika wala mwenza utakasifu ni wake. Huu ndio ujumbe wao wote.

Comments
Post a Comment