Watoto 11 Hawajulikani Walipo Kwa Zaidi ya Siku 10

Watoto 11 wa kiume wakiwemo Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari wametoweka kwa zaidi ya siku 10 katika Kijiji cha Mtimbwilimbwi Halmashauri ya Nanyamba, na bado haijulikani walipo

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda amesema, Serikali ina taarifa hiyo ya Watoto kutoweka na wameshawahoji Wazazi huku juhudi za kuwatafuta zikiendelea

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amesema, sasa ni msimu wa korosho na inawezekana wapo kwenye mashamba ya Wakulima wakubwa wakiokota korosho

Ametoa wito kwa Wazazi kuwa karibu na Watoto, hasa kipindi hiki cha msimu wa korosho kwani baadhi ya Wakulima wakubwa huwachukua wototo kama vibarua jambo ambalo ni kinyume cha sheria  

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

Kisa Cha Nabii Ibraahiym عليه السلام - Sehemu Ya 1