TARATIBU ZA KULA NA KUNYWA

TARATIBU ZA KULA NA KUNYWA

Uislamu unatufundisha kuwa na kiwango cha juu cha adabu, kuheshimu neema wakati wa kula na kujali usafi.
Allah ameweka taratibu kadhaa katika kula na kunywa zinazohakikisha kuwepo kwa makusudio, hekima na busara za Allah, kama kukumbusha neema za Allah kwa mwanadamu, kujikinga na maradhi, kutofanya ubadhirifu na kiburi. 
Miongoni mwa taratibu hizo ni hizi:
  1. Imekatazwa kula na kunywa katika chombo kilicho tengenewa kutokana na Dhahabu au Fedha, au kilicho nakshiwa kwa dhahabu au fedha, kwa sababu huo ni ubadhirifu na kuchupa mipaka na pia ni kuwanyongesha watu masikini. Mtume,swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Msinywe katika vyombo vya Dhahabu na Fedha, na msile katika mabakuli yake, kwa sababu vyombo hivyo ni vyao (makafiri) hapa duniani na ni vyetu (Waislamu) huko Akhera».(Bukhariy, Hadithi Na. 5110. Muslim, Hadithi Na. 2067)
  2. Kuosha mikono kabla na baada ya kula. Linasisitizwa zaidi jambo hili kama mikono ina uchafu au mabaki ya chakula.
  3. Kutaja jina la Allah kwa kusema (Bismillah) kabla ya kuanza kula au kunywa. Maana yake ni kwamba: Ninaomba baraka na ninaomba msaada kwa jina la Allah. Kama atasahau na kukumbuka katikati ya kula, atasema: (Bismillah awwalihi wa aakhirihi) (Kwa jina la Allah mwanzo na mwisho wake)
Mtume,swallalahu alayhi wasalam alimuona mtoto mdogo ambaye alikuwa hajui taratibu za kula. Alimuambia, akiwa na lengo la kumfundisha, kwamba: «Ewe kijana, litaje jina la Allah (sema Bismillah) na kula kwa mkono wako wa kulia na kula sehemu ya chakula iliyopo mbele yako». (Bukhariy, Hadithi Na. 5061. Muslim, Hadithi Na. 2022)
  1. Kula na kunywa kwa mkono wa kulia. Amesema Mtume,swallalahu alayhi wasalam, kuwa: «Msile kwa mkono wa kushoto, kwa sababu shetani anakula kwa mkono wa kushoto».(Muslim, Hadithi Na. 2019)
  2. Inapendekezwa kwamba mtu asile au kunywa akiwa amesimama.
  3. Kula chakula kilichopo karibu yake, naasile katika sehemu ya wengine, kwa sababu kula katika sehemu ya wengine ni taratibu mbaya. Mtume,swallalahu alayhi wasalam amesema kumwambia kijana mdogo kuwa: «…na kula sehemu ya chakula iliyopo mbele yako».
  4. Inapendekezwa kuokota tonge lililo dondoka, kulipangusa kama kuna kitu na kuila kama itawezekana kufanya hivyo. Kufanya hivyo ni kuijali neema na chakula.
  5. Kutokitia dosari chakula, kutokidharau na kutokibeza. Mtu anatakiwa akisifie chakula au akiache na kunyamaza. Mtume,swallalahu alayhi wasalam, hakuwahi asilani kukikashifu chakula. Akikipenda alikuwa anakila, na asipokipenda alikuwa akikiacha. (Bukhariy, Hadithi Na. 5093.  Muslim, Hadithi Na.2064)
  6. Kutokula sana na kutoshiba kupita kiasi, kwa sababu hiyo ni sababu ya maradhi na uvivu. Kula kwa wastani ndio jambo bora zaidi. Mtume,swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwanadamu hajajaza chombo kibaya sana kuliko tumbo. Vinamtosha mwanadamu vijitonge vichache vitakavyo upa nguvu mgongo wake. Ikiwa ni lazima (kula zaidi ya vitonge hivyo vichache), basi theluthi (ya tumbo) iwe kwa chakula chake, na theluthi kwa kinywaji chake, na theluthi kwa kupumua kwake».(Tirmidhiy, Hadithi Na. 2380. Ibnumaajah, Hadithi Na. 3349)
  7. Muislamu akimaliza kula atasema: (Alhamdullilah).  Atamshukuru Allah kwa neema hii ya chakula ambayo amemneemesha kwayo na kawanyima watu wengi. Inawezekana kuongeza kusema: (Alhamdu Lillaahil-ladhii Atw-amanii Haadhatw-twaama Waraqaniihi Min-ghairi Hawlin Minnii Walaa Quwwa = Ninamshukuru Allah ambaye amenipa chakula hiki na amenipa riziki si kwa ujanja wangu wala nguvu zangu). 

Comments

Popular posts from this blog

Watatu kizimbani kwa wizi wa tausi watatu wa Ikulu

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

VYAKULA KATIKA UISLAM