VYAKULA KATIKA UISLAM

Msingi katika vyakula

Msingi katika vyakula na vinywaji vyote ni uhalali, isipokuwa tu vile vyakula na vinywaji vya haramu vilivyotengwa ambavyo vina madhara kwa binadamu katika afya yake, dini na tabia yake. Allah ameeleza neema zake kwa binadamu kwamba amewaumbia vitu vyote vilvyomo ardhini ili wanufaike navyo isipokuwa tu vile alivyo viharamisha kwao. Allah amesema kuwa: «Yeye ndiye aliyekuumbieni vyote vilivyomo ardhini». (Albaqara, aya 29)

Mazao na matunda

Mazao ya mimea yote ambayo wanadamu wanalima au mazao wanayoyapata kutoka katika miti ya misituni, nyikani na porini kwa aina zake zote ni halali na yanafaa kuliwa, isipokuwa tu yale ambayo yanadhuru mwili na afya au kuiathiri akili, kama pombe na mihadarati ambayo imeharamishwa kwa sababu ya kudhuru na kuathiri akili..

Vyakula vya baharini

Makusudio ya vyakula vya baharini ni vile ambavyo haviwezi kuishi isipokuwa kwenye maji tu, na kuishi kwake nchi kavu ni nadra.
Makusudio ya bahari hapa ni maji mengi. Inaingia humo mito na maziwa na aina nyingine za maji mengi.
Vyakula vyote vya majini, sawa viwe vya jamii ya wanyama au mimea, vilivyovuliwa vikiwa hai au kupatikana vikiwa vimekufa, ni halali na vinafaa kuliwa madamu havina madhara kwa afya.
Allah amesema kuwa: «Mmehalalishiwa viumbe vilivyovuliwa baharini na vyakula vyake».(Almaaida, aya 96)
Vilivyovuliwa ni vile viumbe vilivyovuliwa vikiwa hai, na vyakula vyake ni vile viumbe vya majini ambavyo vimekutwa vikiwa vimekufa.
«Mmehalalishiwa mawindo ya baharini (uvuvi)  na chakula chake». Sura Almaida, aya 96.

Wanyama wa nchi kavu

Ili wanyama wa nchi kavu wawe halali kuliwa, ni lazima masharti mawili yatimie:
  1. Wawe halali kuliwa.
  2. Wawe wamewindwa au wamechinjwa kwa taratibu za kisheria.

Ni wanyama gani walioharamishwa kuliwa? 

Jambo la msingi kwa wanyama wote ni kwamba ni halali kuliwa, isipokuwa tu wale wanyama ambao umethibiti ushahidi katika Qur’ani na Sunna wa kuwaharamisha.
Wanyama haramu ni kama ifuatavyo:
  1. Nguruwe: 
Huyu ni mnyama aliyeharamishwa na ni najisi katika Uislamu kwa sehemu zake zote na viungo vyake vyote, na kila kinacho tokana na yeye. Amesema Allah Mtukufu kuwa: «Mmeharamishiwa mizoga na damu na nyama ya nguruwe». (Almaaida, aya 3). Allah pia amesema kuwa: «…au nyama ya nguruwe, kwa sababu ni uchafu».(Al-an-aam, aya 145). Uchafu una maana ya  najisi.
  1. Kila mnyama wa jamii ya wanyama wakali wenye meno yaliyochongeka: 
Makusudio ya wanyama hawa ni kila mnyama anayekula nyama, sawa awe mkubwa kama simba na chui, au mdogo kama paka na mfano wake. Mbwa ni miongoni mwa wanyama hao.
  1. Kila ndege mwenye kucha ngumu: 
Hawa ni ndege wote wanao kula nyama kama vile Kipanga, Tai, Bundi na mfano wake.
  1. Wadudu: 
Wadudu wote wa nchi kavu haifai kuwala, kwa sababu haiwezekani kuwachinja, isipokuwa nzige. Nzige wanafaa kuliwa, kama alivyosema Mtume,swallalahu alayhi wasalam, kuwa: «Tumehalalishiwa (kula) aina mbili za wanyama waliokufa: Samaki na nzige». (Ibnumaaja, Hadithi Na. 3218)
  1. Nyoka na Panya: 
Ni haramu kuliwa, na tumeamrishwa kuwaua. Mtume,swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Aina tano za wanyama ni wabaya. Wanatakiwa kuuliwa popote; ndani ya ibada ya Hija na Mji Mtukufu na nje ya ibada ya Hija na Mji Mtukufu: Nyoka, kunguru, panya, mbwa anayeuma watu na mwewe». (Bukhari 3136 Muslim 1198)
  1. Punda wafugwao majumbani: 
Hawa ni wale punda wanao tumika vijijini kwa uasafiri na usafirishaji wa mizigo.
Ni wajibu wa Muislamu kuhakikisha kuwa chakula ni halali wakati wa kukinunua.

Aina za wanyama halali:

Wanyama aliowahalalisha Allah wako aina mbili: 

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU