SWALA YA IJUMAA

SWALA YA IJUMAA

Katika siku ya Ijumaa na katika wakati wa swala ya Adhuhuri, Allah amefaradhisha swala ambayo ni katika alama kubwa sana za Uislamu, na ni katika faradhi zake muhimu sana. Katika swala hiyo Waislamu hukusanyika mara moja kwa wiki, na husikiliza mawaidha na maelekezo ambayo imamu wa swala ya Ijumaa anayatoa kwao, kisha wanaswali swala ya Ijumaa.
Thawabu katika swala ya Jamaa zinakuwa kwa kadiri ya kwenda mapema kwenye swala hiyo.

Utukufu wa siku ya Ijumaa

Siku ya Ijumaa ni siku tukufu na bora zaidi katika siku za wiki. Allah ameichagua kuwa siku bora zaidi ya  nyingine, na akaitukuza kuliko nyakati nyingine kwa sifa nyingi za kipekee. Miongoni mwa sifa hizo za kipekee ni hizi: 
  • Kwamba Allah ameiteua siku hiyo iwe maalumu kwa umati wa Muhammad na wala sio kwa nyumati nyingine, kama Mtume,swallalahu alayhi wasalam, alivyosema kuwa: «Allah amewakosesha Ijumaa wale waliokuwa kabla yetu. Wayahudi wakawa na siku ya Jumamosi na Wakristo wakawa na siku ya Jumapili. Allah akatuongoza sisi kwa kutupatia  siku ya Ijumaa». (Muslim, Hadithi Na. 856)
  • Kwamba katika siku hiyo aliumbwa Adamu, na pia katika siku hiyo kitatokea Kiyama, kama Mtume,swallalahu alayhi wasalam, alivyosema kuwa: «Siku bora zaidi ambayo jua limechomoza ni siku ya Ijumaa. Katika siku hiyo aliumbwa Adamu, na katika siku hiyo aliingizwa peponi, na katika siku hiyo  alitolewa peponi, na Kiyama hakitatokea isipokuwa tu katika siku ya Ijumaa». (Muslim, Hadithi Na. 854).

Nani analazimika kuswali swala ya Ijumaa?

Swala ya Ijumaa ni wajibu kwa mwenye sifa zifuatazo:
  1. Swala ya
 Ijumaa ni wajibu kwa mwenye sifa zifuatazo
  1. Mukallaf (Mwenye kubeba majukumu kisheria):
 Sio wajibu kwa mwendawazimu, wala kwa mtoto ambaye hajabaleghe.
  1. Mkazi:
 Sio wajibu kwa msafiri, na kwa anayekaa mashambani; nje ya miji na vijiji.

Namna na sheria za swala ya Ijumaa

  1. Inapendekezwa kwa Muislamu kuoga kabla ya swala ya Ijumaa, kwenda mapema msikitini kabla ya kuanza kwa hotuba na kuva nguo nzuri sana.
  2. Waislamu wakusanyike katika msikiti mkubwa na waongozwe na imamu. Apande juu ya Minbari, awakabili  waliokuja kuswali, awahutubie hotuba mbili akitenganisha kati ya hotuba hizo kwa kukaa kidogo.  Awakumbushe kumcha Allah na kuwapa maelekezo pamoja mawaidha na aya mbalimbali
  3. Ni wajibu kwa waliokuja kuswali kusikiliza hotuba. Ni haramu kwao kuzungumza au kushughulika na jambo jingine na kuacha kufaidika na hotuba, hata kama kushughulika huko ni kwa kuchezea zulia kijiwe au mchanga. 
    Kisha imamu atateremka kwenye Minbari. Swala itaqimiwa na atawasalisha watu rakaa mbili, akisoma kwa sauti ya juu katika rakaa hizo.
  4. Sheria inataka Swala ya Ijumaa itekelezwa kwa mkusanyiko wa idadi fulani ya watu. Kwa hiyo, mwenye kupitwa na swala ya Ijumaa au akaichelewa kwa dharura basi atasali swala ya Adhuhuri badala ya Ijumaa, na wala haitasihi kwake swala ya Ijumaa.
  5. Mwenye kuchelewa swala ya Ijumaa, na ikawa hakuwahi pamoja na imamu isipokuwa sehemu chache tu ya rakaa, atakamilisha kuswali swala ya Adhuhuri.
  6. Kila ambaye sio wajibu kwake kuswali swala ya Ijumaa kama vile mwanamke na msafiri akisali msikitini pamoja na Waislamu, swala yake ya Ijumaa itakuwa sahihi, na hatalazimika kuswali swala ya Adhuhuri.

Wanaosameheka kutoswali Ijumaa

Sheria imehimiza ulazima wa kuswali swala ya Ijumaa kwa  ambao ni wajibu kwao, na ikahadharisha kuiacha na  kushughulika na mambo ya kidunia. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Enyi mlioamini,  itakapo adhiniwa kwa ajili ya swala katika siku ya Ijumaa, basi fanyeni haraka kwenda kwenye utajo wa Allah na acheni biashara. Kufanya hivyo ni bora zaidi kwenu ikiwa mnajua». (Sura Aljum-a, aya 9) 
Na sheria imemuonya anayeacha kuisali bila ya sababu za kisheria kwamba mtu huyo atapigwa chapa  katika moyo wake. Mtume,swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kuacha Ijumaa  tatu kwa kuzembea bila ya udhuru wowote, Allah atapiga chapa juu ya moyo wake». (Aabudaud, Hadithi Na.1052, Ahmad, Hadithi Na. 15498).
Maana ya kwamba Allah ataupiga chapa moyo wake ni kwamba Allah atauwekea lakiri moyo wake, ataufinika na kuweka humo ujinga na ugumu wa kutenda mema, kama zilivyo nyoyo za wanafiki na wanaofanya maasi.
Udhuru unaoruhusu kuacha kuswali Ijumaa ni kila jambo linalo kusababishia uzito mkubwa usiokuwa wa kawaida, au jambo ambalo linahofiwa kukuletea madhara makubwa katika maisha yako na afya yako.
«Enyi mlioamini, inapoadhiniwa kwa ajili ya swala katika siku ya Ijumaa, fanyeni haraka kwenda kumtaja Allah na acheni biashara». Sura Aljum’a, aya 9.

Je, ratiba ya kazi ni udhuru katika kuacha kuswali swala ya Ijumaa?

Msingi ni kwamba kazi na majukumu kudumu sio udhuru kwa Muislamu katika kuacha swala ya Ijumaa. Allah anatuamrisha kuacha kazi zetu na kwenda kuswali. Anasema «Enyi mlioamini,  itakapo adhiniwa kwa ajili ya swala katika siku ya Ijumaa, basi fanyeni haraka kwenda kwenye utajo Allah na acheni biashara. Kufanya hivyo ni bora zaidi kwenu ikiwa mnajua». (Sura Aljum-a, aya 9).
Inatakiwa kwa Muislamu kuchagua kazi na majukumu  ambayo katika kazi na majukumu hayo atapata nafasi ya kutekeleza maamrisho ya Allah hata kama masilahi yake ni madogo sana kuliko kazi na majukumu mengine. Allah Mtukufu anasema kuwa: «Na mwenye kumcha Allah atamfanyia njia, na atamruzuku kwa namna asiyodhania, na mwenye kumtegemea Allah, basi anamtosha». (Sura Attalaak, aya 2-3).

Ni wakati gani kazi inakuwa udhuru wa kuacha swala ya Ijumaa?

Kazi ya kudumu na ya kuendelea haizingatiwi kuwa udhuru wa kuacha kuswali swala ya Ijumaa kwa mtu ambaye swala ya Ijumaaa ni wajibu kwake isipokuwa tu katika hali mbili: 
  1.  Yawepo katika kazi manufaa makubwa ambayo hayapatikani isipokuwa tu kwa kubakia kwake kazini na kuacha Ijumaa, na kwamba kwa kuiacha kazi yake yatatokea madhara makubwa, na pia asiwepo mtu wa kushika nafasi yake katika kazi hiyo. 
Mifano: 
• Daktari aliyeko katika uokoaji, ambaye anatoa huduma katika kesi na matukio ya dharura.
• Mlinzi na polisi ambaye analinda mali za watu na nyumba zao zisiibwe na kudhibiti matukio ya uhalifu.
• Mtu anayesimamia utendaji wa kazi za viwanda vikubwa na mfano wake, kazi ambazo zinahitaji uangalizi wa karibu.
  1. Kazi itakapokuwa ndio chanzo pekee cha kupatia riziki yake, na hana njia nyingine ya kukidhi mahitaji yake ya msingi ikiwa ni pamoja na chakula, maji na mahitaji mengine ya msingi kwake yeye na kwa familia yake isipokuwa kazi hiyo tu, ataruhusiwa kubakia kazini na kuacha kuswali swala ya Ijumaa kwa dharura hiyo mpaka apate kazi nyingine au apate chanzo kingine kitachompatia mahitaji yake ya chakula, maji na mahitaji ya msingi yatakayomtosha yeye na anaowahudumia. Pamoja na hayo, ni wajibu kwake kuendelea kutafuta kazi na chanzo kingine cha riziki.

Comments

Popular posts from this blog

Watatu kizimbani kwa wizi wa tausi watatu wa Ikulu

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

VYAKULA KATIKA UISLAM