Ni ipi dini ya mwisho ya Mwenyezi Mungu?

Dear Brother / Sister,
Wanazuoni wa Kiislamu wanagawanya dini katika makundi makuu mawili:
1. Dini za kweli.
2. Dini potovu.
Dini zenye msingi wa kumwamini Mungu mmoja na kuwaamuru watu kumwabudu na kumtii Yeye tu zinaitwa "dini za kweli". Dini za kweli zilizotoka kwa Allah. Kwa hivyo, pia zinaitwa dini zinazotoka mbinguni. Dini ya kweli pia huitwa "dini ya upwekeshaji" kwasababu zina msingi wa kumpwekesha Allah na kumwabudu Yeye tu. 
Dini ambazo hazikuteremshwa na Allah, zilizoundwa na watu na hazina msingi wa kumwamini Mungu mmoja zinaitwa "dini potovu".
Baadhi ya dini za kweli zilipotoshwa na watu baadaye; na ushirikina na imani potovu ambazo hapo mwanzoni hazikuwepo ziliongezwa baadaye. Dini zilizokuwa za kweli hapo mwanzoni lakini baadaye zikabadilishwa zinaitwa "dini zilizogeuzwa"; mathalani, Uyahudi na Ukristo.
Dini ya kwanza kwa wanaadamu ni ya upwekeshaji iliyokuwa na msingi wa kumwamini Mungu mmoja, iliyoteremshwa kwa Adam, mtu wa kwanza na Mtume wa kwanza. Tafiti za kielimujamii zinakubali kuwa dini ya mwanzo ya wanaadamu ilikuwa ya upwekeshaji. Kwa hakika, Schmidt, mtafiti wa historia za dini mbalimbali na mwanaelimujamii, alionesha kwamba Mbilikimo, ambao ni jamii ya kale zaidi duniani, walikuwa na imani ya Mungu mmoja. Uchunguzi wa Schmidt umekanusha madai ya Durkheim kwamba Utambikaji ulikuwa dini ya mwanzo ya wanadamu na akaondosha nadharia hiyo iliyoenea huko Magharibi.
Baada ya Nabii Adam (a.s), baadhi ya watu waliacha kuamini upweke (wa Allah), wakatoka kwenye dini za kweli na kuingiza baadhi ya imani potovu kadiri wakati ulivyosonga mbele kwa kutii nafsi zao na ushawishi wa Shetani. Hivyo, dini potovu zikaibuka. Kadiri watu walivyojitenga na dini ya kweli, Mwenyezi Mungu aliwapelekea mitume wengine na dini ili wawaite kwenye imani ya upwekeshaji. Hata hivyo, baadhi ya watu walikubali wito huo na wengine waling’ang’ania imani zao potovu. Wachilia mbali kuendelea kung’ang’ania imani zao wenyewe, walijaribu kuwazuia wale waliotaka kurejea kwenye dini ya kweli na wakawakandamiza na kuwatesa. Hivyo, mara zote kumekuwa na mapambano baina ya walioamini dini ya kweli na ambao hawakuamini, katika kila karne na enzi. Mapambano haya bado yanaendelea na hayataisha mpaka Siku ya Kiama.
Dini ya Mwisho ni Uislamu.
Leo hakuna hata kimoja katika vitabu vitukufu vilivyoshushwa kabla ya Quran chenye hali yake asili. Kadiri wakati ulivyosonga mbele, uasili wake ulipotea na vikaandikwa upya na watu. Kwa hivyo, ushirikina na imani potovu vikachanganywa ndani mwake. Mathalani, ni ukweli wa kihistoria kuwa Taurati isingeweza kudumishwa na Wayahudi baada ya Nabii Musa, kwani waliishi uhamishoni kama watumwa kwa karne nyingi na walipoteza imani yao na wakaabudu sanamu; pia ni uweli wa kihistoria kuwa Taurati iliyopo sasa iliandikwa na baadhi ya wanazuoni na ikapokelewa kana kwamba ilikuwa ile  Taurati ya asili. Ni dhahiri kuwa kitabu kilichoandaliwa baada ya kupita muda huo mrefu uliovurugika hakiwezi kuwa Taurati ileile aliyoshushiwa Nabii Musa. Kwa hivyo, ina baadhi ya madai na kashfa zisizowastahiki mitume na amri zilizo kinyume na dini yenyewe. 
Zaburi aliyopelekewa Dawud ilipatwa na hali hiyo hiyo.
Ama kuhusu Injili (Biblia), Nabii Isa (Yesu) hakupokea wahyi wa kimaandishi kwasababu alipata utume alipokuwa na umri wa miaka thelathini na kazi ya utume iliisha alipofikisha umri wa miaka thelathini na tatu.  Alikwenda kijiji hadi kijiji kingine na mji mmoja hadi mwingine ili kuwaongoza watu katika kipindi kifupi sana cha miaka mitatu. Katika siku zake za mwisho, kila mara alifuatwa na watawala wa Kirumi kutokana na uchochezi wa Wayahudi. Hakuweza kupata muda au fursa ya kuandikwa Injli. Kwa hakika, Injili zilizopo leo zimeitwa kwa majina ya watu walioziandika na zinaonekana kama wasifu wenye mahubiri, mafunzo na wongozo wa Yesu kwa mitume wake. Kando ya hayo, hazikuandikwa na mitume wake, ambao walikuwa waumini wa mwanzo, bali waliosikiliza maneno ya kiungu aliyopewa Yesu kuwafikishia.
Zipo tofauti baina ya Biblia zilizopo, kwa upande wa maudhui na masimulizi. Kwa hakika, Biblia hizo zilikubaliwa na baraza la mapadri elfu moja mnamo mwaka 325 BK huko Nicaea. Baraza lilichunguza mamia ya Biblia na kukubali Biblia 4 zilizodai kuwa Yesu alikuwa katika uungu kwa muwafaka wa wajumbe 318 na wakaziharibu Biblia zingine kwa kuzichoma moto.
Kama ilvyoonekana, kanuni ya kwamba Yesu alikuwa mwana wa Mungu – Allah atukinge dhidi ya hilo – ilipokelewa na baraza lililokutana miaka mingi baada ya Yesu. Kwa hivyo, ni muhali kusema kuwa Biblia zilizopo leo ni kama Biblia za asili

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU