NAFASI YA TABIA NJEMA KATIKA UISLAMU JE UNASIFA HIZI????

Tabia njema katika Uislamu sio jambo la anasa wala la ziada. Tabia njema ni sehemu muhimu inayofungamana na dini katika pande zake zote. Tabia na maadili mema katika Uislamu yana nafasi na daraja la juu sana. Linadhihirika wazi hilo katika hukumu na sheria zote za Kiislamu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, ameletwa ili aje kutimiza maadili na tabia njema. Nafasi ya maadili na tabia njema katika Uislamu: Manufaa ya tabia njema katika Uislamu: Mifano katika maisha ya Mtume:

NAFASI YA TABIA NJEMA KATIKA UISLAMU

  1. Tabia njema ni miongoni mwa makusudio muhimu sana ya kuletwa Mtume Muhammad kwa watu
Amesema Allah Mtukufu kuwa: «Yeye ndiye aliyempeleka Mtume kwa  watu wasiojua kusoma, akiwa anatokana na wao, (ili) awasomee aya zake na awatakase». (Aljumua, aya 2). Allah Mtukufu anaelezea neema zake kwa waumini kwamba amemtuma Mtume wake ili awafundishe Qur`ani na awawafundishe kuzitakasa nafsi zao. Kutakasa kuna maana ya kuusafisha moyo usiwe na shirki  na tabia mbaya, kama vile chuki, husda, na pia kusafisha kauli na vitendo zisitamke na kutenda desturi na tabia mbaya. Amesema Mtume, swallalahu alayhi wasalam, kuwa: «Hakika, hakuna vingine isipokuwa kwamba mimi nimepewa Ujumbe ili nitimize tabia njema». (Albaihakiy, Hadithi Na. 21301). Mojawapo ya sababu muhimu sana za kuletwa kwa Mtume ni kuboresha na kuendeleza tabia na maadili bora ya mtu mmoja mmoja na jamii. 
  1. Tabia njema ni sehemu muhimu katika imani na itikad
Mtume, swallalahu alayhi wasalam, alipoulizwa kwamba: «Ni muumini gani aliye bora zaidi katika imani?», alijibu kuwa: «Ni yule mwenye tabia nzuri sana miongoni mwao». (Attirmidhiy, Hadithi Na. 1162. Abudaud, Hadithi Na. 4682) .
Allah ameitaja imani kwamba ni wema na kusema kuwa: «Sio wema kwamba mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na wa magharibi tu. Bali wema ni wa (yule) ambaye anamuamini Allah na Siku ya Mwisho na Malaika na Vitabu na Manabii». (Albaqara, aya  177). Wema ni neno linalo jumuisha aina mbali mbali za kheri, ikiwa ni pamoja na tabia, kauli na vitendo. Na kwa sababu hii, ndio Mtume alisema kuwa: «Tabia nzuri ndio wema». (Muslim, Hadithi Na. 2553)
Jambo hili linadhihiri kwa uwazi kabisa katika kauli ya Mtume isemayo kuwa: «Imani ni mambo sitini na kitu. Bora zaidi ya mambo hayo ni kusema: Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah tu. Na jambo la chini kabisa ni kuondosha kero njiani. Na kuona haya ni katika sehemu ya imani». (Muslim, Hadithi Na. 35).
  1. Tabia njema zimefungamanishwa na aina zote za ibada
Huwezi kukuta Allah anaamrisha ibada fulani isipokuwa kwamba utakuta kuwa anagusia makusudio ya ibada hiyo kitabia na kimaadili au anagusia athari ya ibada hiyo kwa mtu na kwa jamii. Mifano ya hili ni mingi. Miongoni mwa mifano hiyo ni hii ifuatayo: 
Swala: «Na simamisha swala. Kwa yakini, swala inakataza  mambo machafu na maovu». (Al-ankabuut, aya 45)
Zaka: «Chukua kutoka katika mali zao Zaka, uwasafishe na uwatakase kwa Zaka hiyo». (Attauba, aya 103). Pamoja na kwamba uhalisia wa Zaka ni kuwafanyia hisani watu na kuwasaidia, lakini pia inamrekebisha mtu na kumtakasa asiwe na tabia mbaya.
Swaumu: «Enyi mlio amini, mmeandikiwa kufunga saumu, kama ilivyoandikwa kwa wale walio kuwepo kabla yenu, ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Albaqara, aya 183).  Makusudio ni kumcha Allah kwa kutekeleza maamrisho yake na kuepuka makatazo yake. Kwa sababu hiyo anasema Mtume, swallalahu alayhi wasalam, kuwa: «Mtu ambaye hakuacha uongo na kuufanyia kazi uongo, Allah hana haja kwa mtu huyo kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhariy, Hadithi Na. 1804).
Mtu ambaye funga yake haikumuathiri yeye mwenyewe na tabia zake katika kuishi na watu wengine, hakulifikia lengo la funga.
  1. Thawabu na malipo makubwa ambayo Allah ameyaandaa kwa ajili ya mtu mwenye tabia nj
Ushahidi wa hayo kutoka katika Qur`ani na Suna ni mwingi. Miongoni mwa ushahidi huo ni huu ufuatao: 
  • Tabia njema ni amali njema itakayokuwa nzito zaidi katika Mizani Siku ya Kiama:
Anasema Mtume, swallalahu alayhi wasalam kuwa: «Hakuna kitu chochote kitakacho wekwa katika Mizani Siku ya Kiama kikawa kizito sana kuliko tabia njema. Na kwa yakini, mwenye tabia njema atafikia daraja la mwenye kufunga na  mwenye kusali». (Attirmidhiy, Hadithi Na. 2003)
  • Tabia njema ni sababu kubwa ya kuingia peponi:
Anasema Mtume, swallalahu alayhi wasalam, kuwa: «Mambo yatakayo waingiza sana watu peponi ni uchamungu na tabia njema». (Attirmidhiy, Hadithi Na. 2004. Ibnumaaja, Hadithi Na. 4246)
  • Mwenye tabia njema atakuwa mtu wa daraja la karibu sana na Mtume Siku ya Kiama:
Amesema Mtume, swallalahu alayhi wasalam, kuwa: «Kwa yakini, miongoni mwa wanaopendwa na mimi sana miongoni mwenu na watakaokuwa karibu sana na mimi miongoni mwenu kwa makazi Siku ya Kiama ni wale wenye tabia nzuri sana miongoni mwenu». (Attirmidhiy, Hadithi Na. 2018)
  • Kwamba daraja la mtu mwenye tabia njema ni pepo ya juu kwa mujibu wa dhamana ya Mtume  na uthibitisho wake:
Amesema Mtume, swallalahu alayhi wasalam, kuwa: «Mimi ni mdhamini wa nyumba itakayo kuwepo katika viunga vya peponi kwa mtu ambaye ameacha kubishana hata kama alikuwa sahihi. Na (mimi ni mdhamini wa) nyumba itakayo kuwepo katikati ya pepo kwa mtu ambaye ameacha kusema uongo hata kwa utani. Na (mimi ni mdhamini wa) nyumba itakayo kuwepo pepo ya juu kwa mtu ambaye amekuwa na tabia nzuri». (Abuudaud, Hadithi Na. 4800)
«Hakuna vingine isipokuwa kwamba, nimetumwa kuja kukamilisha tabia nzuri».

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU