NAFASI YA KIPEKEE YA TABIA NJEMA KATIKA UISLAMU

NAFASI YA KIPEKEE YA TABIA NJEMA KATIKA UISLAMU

Tabia njema katika Uislamu zinasifika kwa sifa kadhaa za kipekee ambazo, kwa sifa hizo, dini hii tukufu inakuwa ya kipekee. Miongoni mwa sifa hizo ni hizi: 
  1. Tabia Njema hazikuwekwa kwa ajili ya aina fulani tu ya watu.
Allah ameumba wanadamu wakiwa katika maumbo, rangi na lugha tofauti. Amewafanya sawa; hakuna yeyote bora zaidi kuliko mwengine isipokuwa tu kwa kiwango cha imani yake, uchamungu wake na wema wake. Amesema Allah Mtukufu kuwa: «Enyi watu! Hakika, sisi tumekuumbeni kutokana na mwanaume na mwanamke, na tumekufanyeni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika, aliye mtukufu zaidi kwa Allah miongoni mwenu ni mchamungu zaidi katika nyinyi». (Alhujuraat, aya 13).
Tabia nzuri zinayafanya mahusiano ya Muislamu na  watu wote yawe ya aina ya pekee; hakuna tafauti kati ya tajiri na masikini, au kiongozi na mtu wa kawaida, au mweusi au mweupe, au Muarabu au sio Muarabu.

Tabia njema katika kuishi na wasiokuwa waislamu

Allah Mtukufu anatuamrisha tuwe na tabia nzuri na watu wote. Uadilifu, hisani na huruma ni tabia za Muislamu ambazo anatakiwa kuzionesha katika maneno yake na vitendo vyake anapokuwa na Muislamu mwezake au kafiri. Anatakiwa kuhakikisha kuwa tabia nzuri ndio nyenzo yake ya kuwalingania na kuwahubiria wasiokuwa Waislamu ili waweze kuifuata dini hii tukufu.
Amesema Allah Mtukufu kuwa: «Allah hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita kwa sababu ya dini, na  hawakukufukuzeni kwenye miji yenu. Hakika,  Allah anawapenda wafanyao uadilifu». (Almumtahinah, aya 8)
Ilivyo ni kwamba Allah ameharamisha kwetu kuwapenda makafiri na kupenda shirki na ukafiri walio nao. Amesema Allah Mtukufu kuwa: «Hakuna vingine isipokuwa kwamba Allah anakukatazeni kuwapenda wale ambao wamekupigeni vita kwa sababu ya dini, na wakakufukuzeni kwenye miji yenu, na wakasaidia katika ufukuzaji huo. Na yeyote anayewapenda, hao ndio madhalimu». (Almumtahinah, aya 9)
  1. Tabia za njema hazihusu binadamu tu

Tabia njema kwa wanyama

Mtume, swallalahu alayhi wasalam, anatueleza tukio la mwanamke aliyehukumiwa kuingia motoni kwa sababu ya kumfunga paka wake na akafa kwa sababu ya njaa. Kwa upande wa pili, Mtume, swallalahu alayhi wasalam, anatueleza tukio la mtu ambaye Allah amemsamehe dhambi zake kwa sababu ya kumpa maji mbwa ambaye alikuwa na kiu kali. Mtume anasema: «Mwanamke ameingia motoni kwa sababu ya paka aliyemfungia akawa hampi chakula na wala hakumwacha akala wadudu wa ardhini». (Bukhariy, Hadithi Na. 3140. Muslim, Hadithi Na. 2619)
Pia Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Wakati mtu mmoja alipokuwa anatembea njiani, alishikwa na kiu kali. Aliona kisima, akaingia kisimani  na kunywa maji. Halafu alipokuwa anatoka, alimuona mbwa anatweta na kutoa ulimi nje huku akila tope kutokana na kiu. Yule mtu akasema: Hakika, huyu mbwa ana kiu kali kama nilivyokuwa mimi. Akaingia tena kisimani, akakijaza maji kiatu chake, halafu akakishikilia kwa kutumia mdomo wake mpaka akapanda juu na kumpa maji mbwa. Allah alimshukuru mtu yule na akamsamehe madhambi yake. Maswahaba wakauliza: Ewe mjumbe wa Allah,  hivi sisi tunapata malipo kwa sababu ya hawa wanyama? Mtume akajibu:  Katika (kulifanyia hisani) kila ini bichi (kiumbe hai) kuna malipo». (Bukhari, Hadihti Na. 5663. Muslim, Hadithi Na. 2244).
«Katika (kuhudumia) kila ini bichi (kiumbe chenye uhai) kuna thawabu».

Tabia njema katika kutunza mazingira

Uislamu unatuamrisha kuistawisha ardhi, kwa maana ya kufanya kazi humo, kufanya maendeleo, kuzalisha na kujenga hali bora ya maisha, pamoja na kuitunza neema hii na kuacha kuiharibu na kuzifanyia ubadhirifu rasilimali zake, sawa uharibifu huo uwe unamgusa mwanadamu au mnyama au mmea. Uharibifu ni kitendo ambacho Uislamu haukikubali na unakichukia. Allah hapendi ufisadi (uharibifu) katika nyanja zote za maisha. Amesema: «Na Allah hapendi ufisadi (uharibifu)». (Albaqara, aya 205).
Hali hii ya kujali mazingira inafika mpaka kwenye kiwango kwamba Mtume, swallalahu alayhi wasalam, anawausia Waislamu wafanye mambo ya kheri hata katika mazingira magumu sana na hali tete sana. Anasema: «Endapo kitatokea Kiama na mmoja wenu ameshika mche mkononi, basi kama ataweza kuupanda mche huo kabla Kiama hakijasimama, afanye hivyo». (Ahmad, Hadithi Na. 12981)
  1. Tabia njema katika nyanja zote za maisha

Familia

Uislamu unatilia mkazo umuhimu wa tabia njema katika ngazi  ya familia; kati ya wanafamilia wote. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, anasema kuwa: «Mbora wenu zaidi ni yule mbora wenu kwa familia yake. Na mimi ni mbora wenu zaidi kwa familia yangu». (Attirmidhiy, Hadithi Na. 3895)
Mtume, swallalahu alayhi wasalam, pamoja na kuwa ni mwanadamu bora sana, alikuwa  akifanya kazi akiisaidia familia yake katika mambo makubwa na madogo. Aisha, Allah amuwiye radhi, mke wa Mtume, anasimulia hali hii na kusema kuwa: «(Mtume) Alikuwa anakuwepo katika (kufanya) kazi za familia yake». Hii ina maana kwamba alikuwa akiisaidia familia yake na kufanya kazi za nyumbani walizokuwa wakizifanya. (Bukhariy, Hadithi Na. 5048).
Mtume, swallalahu alayhi wasalam, alikuwa akifanya utani na kucheza na familia yake. Mkewe, mama wa waumini Aisha, Allah amuwiye radhi, anahadithia kuwa: «Nilitoka pamoja na Mtume katika baadhi ya safari zake nikiwa bado mdogo na sijanenepa. Mtume aliwaaambia watu: Tangulieni mbele, wakatangulia. Aliniambia: Njoo tushindane kukimbia. Tukashindana kukimbia na nikamshinda. Alinyamaza na hakusema kitu. Nilipokuwa nimenenepa na nikawa nimesahau (kuwa tulishindana kukimbia na nikamshinda), nilitoka naye tena katika baadhi ya safari zake. Aliwaambia tena watu: Tangulieni mbele, wakatangulia. Akaniambia: Njoo tushindane kukimbia. Tukashindana kukimbia na akanishinda. Alicheka huku akisema: «(Ushindi) Huu ni lipizo la (ushindi wako) ule». (Ahmad, Hadithi Na. 26277).

Biashara

Kupenda mali wakati mwingine kunaweza kumtawala mwanadamu, akavuka  mipaka na akaingia katika haramu. Kwa sababu hiyo, Uislamu unakuja ili kuhimiza juu ya umuhimu wa kudhibiti jambo hilo kwa kupitia tabia njema. Miongoni mwa mahimizo hayo ni haya: 
  • Uislamu unakataza kuchezea na kudhulumu katika vipimo. Unamuahidi anayefanya hivyo kuwa atapata adhabu kali sana. Allah Mtukufu anasema kuwa: «Ole wao wenye kupunja!  Ambao wanapo pimiwa na watu, wanataka wapimiwe vipimo kamili. Na (lakini wao)  wanapo wapimia watu kwa kipimo cha ujazo au kwa kipimo cha uzito, wanapunja». (Almutaffifiin, aya 1-3)
  • Uislamu unahimiza kusamehe na upole katika kuuza na kununua, kama alivyosema Mtume kuwa: «Allah anampa rehema mtu msamehevu anapo uza, na anapo nunua, na anapo kopesha». (Bukhariy, Hadithi Na. 1970)

Ufundi

Uislamu unawahimiza mafundi wawe na maadili na tabia  kadhaa. Miongoni mwa maadili hayo ni haya yafuatayo:
  • Kufanya kazi kwa ufanisi, uzuri na umahiri, kama alivyosema Mtume, swallalahu alayhi wasalam, kuwa: «Kwa hakika, Allah anapenda mmoja wenu anapofanya kazi aifanye kwa ufanisi». (Abuu Yaalaa, Hadithi Na. 4386. Albaihaqiy, Hadithi Na. 5313) 
  • Kutekeleza ahadi walizokubaliana na watu. Amesema Mtume, swallalahu alayhi wasalam, kuwa: «Alama za mnafiki ni tatu» na akataja kuwa miongoni mwa alama hizo ni «..na akitoa ahadi hatekelezi». (Bukhariy, Hadithi Na. 33)
  1. Tabia njema katika nyanja zote za maisha
Katika Uislamu hakuna maeneo maalumu ya kufanya tabia njema. Muislamu anatakiwa kutekeleza sheria ya Allah na kushikamana na tabia njema hata katika vita na katika mazingira magumu. Uzuri wa lengo hauhalalishi nyenzo mbaya ya kufikia lengo hilo, na pia hakufuniki makosa na upotokaji wa nyenzo hiyo.
Kwa sababu hii, Uislamu umeweka misingi ambayo inamdhibiti Muislamu na inadhibiti shughuli zake hata katika uadui na vita, ili hali isije ikawa ni utii wa matakwa ya hasira, kukosa uvumilivu na kushibisha njaa za husuda, ukatili na ubinafsi.

Miongoni mwa tabia njema vitani

  1. Imeamrishwa kuwatendea haki na uadilifu maadui, kutowadhulumu na kutowashambulia kwa ghafla:
Amesema Allah Mtukufu kuwa: «Na kuwachukia watu fulani kusikuchukueni mkaacha kufanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hilo liko karibu sana na uchamungu». (Almaaida, aya 8).  Maana ni kwamba kuwachukia kwenu maadui wenu kusikuchukueni mkavuka mipaka na mkafanya dhuluma. Bali hakiksheni mnakuwa waadilifu katika kauli zenu na vitendo vyenu. 
  1. Imekatazwa kuwavamia ghafla na kuwafanyia uhaini maadui.
Uvamizi na hiana ni haramu, hata kuwafanyia maadui. Amesema Allah Mtukufu kuwa: «Kwa yakini,  Allah hawapendi wenye kufanya hiana».   (Al-anfaal, aya 58)
  1. Imekatazwa kutesa na kudhalilisha maiti:
Ni haramu kudhalilisha maiti, kama alivyosema Mtume, swallalahu alayhi wasalam, kuwa: «Na msidhalilishe (maiti)».  (Muslim, Hadithi Na. 1731)
  1. Imekatazwa kuua raia ambao hawashiriki katika vita, na pia imekatazwa kuharibu ardhi na mazingira:
Huyu hapa Abuubakar Assiddiiq, Allah amuwiye radhi, kiongozi wa Waislamu na Swahaba bora zaidi anamuusia Usama Bin Zaid wakati alipomteua kuwa kamanda wa jeshi lililokwenda Sham, kwamba: «Msiue mtoto mdogo, wala mzee kikongwe, wala mwanamke, wala msikate mtende na kuuchoma, wala msikate mti wenye kutoa matunda, wala msichinje mbuzi, wala ng`ombe, wala ngamia isipokuwa tu kwa ajili ya kula. Pia mtawakuta watu wamejifungia katika nyumba za ibada. Waacheni wafanye humo yale waliyojifungia kwa ajili yake». Ibnu Asaakir 2/50).
المسلم ملتزم بأخلاقه حتى في أحلك الظروف

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU