Kingwangala "Tuwaache Watu WETU Wamsherehekee Rais, Huyu ni Mtu Wao Tusimtenge na Watu Wake"
Dr Kingwangala Ameandika Kupitia Ukurasa wake wa Instagram:
Watu wetu wa kila aina jana wamesherehekea birthday yake kwa upendo na Mshikamano wa kipekee. Nchi nzima imemuombea dua Rais wetu. Hali iliyoonesha kuwa kweli jana ni siku aliyozaliwa Rais Chuma/Jiwe tunayempenda. Birthday yake ilikuwa ya heshima, ya kiTaifa. Na miongoni mwetu wapo waliotania kuwa wanaenda ikulu kummwagia maji Rais, wengine walimwagia maji picha yake! Ilimradi tu kila mtu alisherehekea birthday ya Mheshimiwa kwa namna yake. Kuna watu wamekuwa wakiiga sauti ya Rais, wakiiga mavazi nk. Sidhani kama ni dhambi, zaidi kwa mwanamkakati kama mimi, nikifanya tathmini yangu, mara moja naona kuwa Rais anapendwa na watu wake.
Watu wanaona Rais ni mali yao. Wanajihusisha naye. Na hii ni dalili kuwa mwakani Rais atapita kwa upepo wa kisulisuli, pengine zaidi ya asilimia 90! My take: tuwaache watu wetu wamsherehekee Rais wao, huyu ni mtu wao, ni mali yao! Tusimtenge na watu wake. Imagine Rais angekuwa haleti utani hata kidogo, uso wa mbuzi mwanzo hadi mwisho, na sisi tukauona upande wake wa pili kwamba ni ‘binadamu’ mwenye utu, upendo na huruma, unadhani tungekuwa tunanyoosha mikono kumshauri kwa dhati kabisa kwenye vikao?! Kwanza tungezikimbia teuzi! ๐๐๐. Nani angebaki kumsaidia kazi hii ngumu aliyonayo? Utani wa Rais unalainisha vyuma kidogo. Tuwaache watanzania wamfurahie Rais wao jamani!" Kingwangala
Comments
Post a Comment