Aya 101 – 105: Aya Mahali Pa Aya Nyingine

Lugha

Tofauti kati ya neno Aa’jamiyy na A’jamiyy ni kuwa la kwanza lina maana ya mtu asiyekuwa fasaha katika Kiarabu, hata kama ni mwarabu. Na lapili lina maana ya lugha nyingine isiyokuwa Kiarabu.

Maana

Na tunapobadilisha Aya mahali pa Aya nyingine, na Mwenyezi Mungu anajua anayoteremsha. Wao husema: “Hakika wewe ni mzushi.” Bali wengi wao hawajui.
Wanaosema hapa ni washirikina waliomkadhibisha Muhammad (s.a.w.). Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewaumba viumbe na Yeye ni mwenye hekima, Mjuzi wa kujua masilahi yao na uharibifu wao. Mara nyingine hekima inaona kuwa ni masilahi kuweka kwa waja wake sharia ya hukumu kwa muda fulani, wakafanya.
Kisha ukiisha ule muda, sharia ile inaondolewa naYule ambaye imetukuka hekima yake huweka hukumu nyingine mahali pa ile hukumu ya kwanza kulingana na masilahi vilevile.
Haya ndiyo makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu: Tunapobadilisha Aya mahali pa Aya nyingine’
Washirikina walipokuwa wakiona hivi humwambia Muhammad (s.a.w.) kuwa wewe unajifanyia mwenyewe tu haya kisha unayanasibisha kwa Mwenyezi Mungu kwa uwongo na uzushi. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anajua kuwa Yeye ndiye aliyeteremsha mabadiliko haya kwa Mtume wake mkweli, mwaminifu na anajua kuwa wao ndio wazushi kwa kusema kwao kuwa Mtume ni mzushi.
Tafsiri wazi zaidi niliyosoma kuhusu Aya hii ni ile iliyopokewa kutoka kwa Ibn Abbas, kwamba inapoteremshwa Aya ya ugumu kisha ikateremshwa Aya ya laini, maquraishi husema kuwa Muhammad anawachezea maswahaba zake; leo anawaamrisha hivi na kesho anawakataza na kwamba yeye hayasemi haya ila yeye mwenyewe tu, ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii. tumezungumzia kuhusu kufuta hukumu katika Juz. 1 (2:106).
SemameiteremshRohtakatifkutokkwMolwakoili awathibitishe wale walioamini na kuwa ni uwongofu na bishara kwa Waislamu.
Roho takatifu ni Jibril. Ameitwa hivyo kwa sababu ameteremsha Qur’an ambayo ni takatifu kutoka kwa Mwenyezi Mungu hadi kwa Muhammad (s.a.w.). Umetangulia mfano wa Aya hii katika Aya ya 89 ya sura hii.
Hapa imetajwa kwa kuwarudi washirikina walionasibisha kubadilisha kwa Mtume. Kule imetajwa kwa mnasaba wa kuwa Mwenyezi Mungu amesema atamleta shahidi kwa kila umma na Muhammad atakuwa shahidi wa umma wake kwamba yeye amiefikisha Qur’an ambayo ni ubainifu wa kila kitu.
Na hakika tunajua kwamba wao wanasema yuko mtu anayemfundisha.
Washirikina walimtuhumu Muhammad (s.a.w.) kwamba yeye anafundishwa Qur’an na mtu mwingine. Hakuna mwenye shaka kwamba hii ni aina ya vita vya propaganda za uwongo wanazozitangaza wafisadi duniani kwa masilahi yao. Leo watu wameendelea na mfumo wa aina yake katika propaganda dhidi ya wenye ikhlasi na viongozi wema. Wamekuwa na ufundi ambao unawahadaa watu wema wengi walio wasafi.
Lugha ya huyo wanayemuelekezea sio fasaha na hii ni lugha ya kiarabu bayana.
Yaani lugha ya huyo mtu wanayemsema ni kiarabu cha mtaani.
Hii ni kuwarudi washirikina na kauli yao kuhusu Muhammad (s.a.w.) kwamba anafundiswa na mtu mwingine. Hapa inaonyesha kwamba huyo mtu waliyemsema kuwa anamfundisha, lugha yake ni ya mtaani na lugha ya Qur’an ni kiarabu fasihi. Sasa itawezekana vipi asiyejua fasihi amfundishe mwengine fasihi.
Walirudiarudia uzushi huu maadui wa Uislamu baadae na mpaka leo wahubiri wengi wa Kikiristo wanathubutu kusema, kwa kutojua au kujitia kutojua, kwamba kwenye Qur’an kuna fani na hekima ambazo wakati huo hazikuwa na athari yoyote.
Kama tukichukulia kuwa zilikuweko, basi isingewezekana yeyote kuzikusanya na kuzijua na kama angelizijua basi umashuhuri wake ungelizidi ule wa Aristatle ambaye Waarabu wanamwita mwalimu wa kwanza. Licha ya wao kujua kwamba hakuwa na yeyote aliyekuwa wakati wa Mtume aliyedaiwa kujua hizo elimu zilizomo ndani ya Qur’an.
Hakika wale ambao hawaziamini Aya za Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu hawaongoi, nao watapata adhabu chungu.
Makusudio ya Aya za Mwenyezi Mungu ni dalili zinazosema kuhusu kuweko kwake, miujiza inayoshuhudia utume wa Mitume na hukumu zilizoteremshwa kwao. Ama makusudo ya uongofu hapa ni thawabu; yaani Mwenyezi Mungu hatampa thawabu, bali atamwadhibu kwa aina za adhabu

Mwongo Kafiri

Hakika wanaozua uwongo ni wale tu wasioziamini Aya za Mwenyezi Mungu wala ufufuo, hisabu na malipo; kama washirikina waliomwambia Muhammad (s.a.w.) yale waliyomwambia.
Na hao ndio waongo.
Wanajasiri kusema uwongo na kufanya ufisadi na dhambi kwa vile wao hawaogopi adhabu ya uwongo na wala hawatarajii thawabu.
Unaweza kuuliza: Kauli yake Mwenyezi Mungu: Hakika wanaozua uwongo ni wale tu wasioziamini Aya za Mwenyezi Mungu’ si inatosha, sasa kuna haja gani tena ya kusema: Na hao ndio waongo’? Je, kuna makusudio gani ya kukaririka huku? Wafasiri wamejibu kuwa lengo ni kutanabahisha kuwa sifa ya uwongo kwao imethibiti; sawa na kumwambia mtu: ‘Wewe ni mwongo tena mwongo sana’ yaani hali yako na mazoweya yako ni uwongo tu.
Swali la pili ni: Mwenyezi Mungu anasema “Hakika wanaozua uwongo ni wale tu wasioziamini Aya za Mwenyezi Mungu” Hii si ni kuwafanya makafiri kuwa ndio waongo tu; na inajulikana kuwa kuna makafiri walio wakweli sana na wakutegemewa zaidi, katika mazungumzo yao, kuliko wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho?
Jibu: Hakika Mwislamu muongo anamwamini Mwenyezi Mungu kinad- hariya na ni kafiri kimatendo. Kwa hiyo yeye kwa wasifu wake ni muumini kinadhariya na kifikra, atachukuliwa duniani kuwa ni Mwislamu. Na kafiri kwa wasifu wake atachukuliwa kuwa ni kafiri kulingana na Aya hii na yaliyopokewa kutoka kwa Mtume, alipoulizwa: Je, Mumin anasema uwongo? Akajibu: La; kisha akasoma Aya hii.
مَنْ كَفَرَ بِاللَّهِ مِنْ بَعْدِ إِيمَانِهِ إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ وَلَٰكِنْ مَنْ شَرَحَ بِالْكُفْرِ صَدْرًا فَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ مِنَ اللَّهِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ {106}
AnayemkufurMwenyezi Mungbaadyimani yakeIsipokuwaliyelazimishwa na hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya imani. Lakini aliyekifungulia kifua chake ukafiri, basi haghadhabya Mwenyezi Mungu iko juu yanwatapatadhabu kubwa.
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اسْتَحَبُّوا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الْآخِرَةِ وَأَنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ {107}
Hiyo ni kwa sababu wao wamestahabmaishya dunia kuliko ya akhera. Na kwamba Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri.
أُولَٰئِكَ الَّذِينَ طَبَعَ اللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَسَمْعِهِمْ وَأَبْصَارِهِمْ ۖ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ {108}
Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amepiga chapa juu ynyoyzanjuya masikio yao; na hao ndio wenye kughafilika.
لَا جَرَمَ أَنَّهُمْ فِي الْآخِرَةِ هُمُ الْخَاسِرُونَ {109}
Hapanshakkwamba wao ndio wenye kuhasirika Akhera.
ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ هَاجَرُوا مِنْ بَعْدِ مَا فُتِنُوا ثُمَّ جَاهَدُوا وَصَبَرُوا إِنَّ رَبَّكَ مِنْ بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَحِيمٌ {110}
Kisha hakika Mola wako kwa wale waliohajiri baada ykusumbuliwkisha wakafanya jihadi na wakasubiribilshakMola wakbaadyhayni Mwingwmaghufira, mwenye kurehemu.
يَوْمَ تَأْتِي كُلُّ نَفْسٍ تُجَادِلُ عَنْ نَفْسِهَا وَتُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَا عَمِلَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ {111}
Sikambayo kila nafsi itakuja jitetea. Na kila nafsi italipwa sawa na yale iliyoyafanyanahawatadhulumiwa.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

Kisa Cha Nabii Ibraahiym عليه السلام - Sehemu Ya 1