Ahl al-Kitab (Watu wa Kitabu) inamaanisha nini?

Wafuasi wa dini za mbinguni kama vile Uyahudi na Ukristo wanaitwa “Ahl al-Kitabu” (Watu wa Kitabu). Watu wa Kitabu wametajwa kwa wingi ndani ya Quran. Watu wa Kitabu wanazingatiwa kuwa ni “makafiri” kwa sababu hawamkubali Mtume (s.a.w.) lakini sio makafiri kwa upande wa “kumkanusha Allah.”

Quran inatoa kipaumbele kwa watu wa Kitabu kuhusiana na masuala fulani ikilinganishwa na makafiri wengine. Mathalani, inaruhusiwa kuwaoa wasichana na wanawake wa watu wa Kitabu na inaruhusiwa kula nyama ya wanyama waliowachinja. (al-Maida, 5) Kipaumbele hiki wanapewa wao kwa sababu wako karibu na imani ikilinganishwa na makafiri wengine. Quran inawahutubia ifuatavyo:

Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanye sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu.” (Aal-i Imran, 64) Yaani, tusitambuane kuwa ni Miungu. Hebu tuzitathmini amali zetu kwa kutegemea amri ya Allah na radhi zake. Hebu na tuwe waja wa Allah. Hebu na tujijue kuwa ni waja Wake. Hebu tuheshimiane kwa kutegemea kanuni hii. (1)

Quran inaeleza kuwa Watu wa Kitabu wanawafanya wanazuoni wao na Mapadri wao kuwa ni Miungu. (at-Tawba, 31) Wakati Adiy b. Haram, aliyesilimu kutoka katika Ukristu, alisema, “Ewe Mjumbe wa Allah! Hatuwafanyi kuwa ni Miungu wetu”, Mjumbe wa Allah (s.a.w.) akasema,

“Wanaharamisha alichokihalalisha Allah na kuhalalaisha Allah alichokiharamisha. Hili linamaanisha kuwafanya Miungu wao.” (2)

Kwa kweli, sio lazima kumwita mtu “Mungu” ili kumfanya awe Mungu. (3)

Aya ifuatayo inaeleza njia ya kuifuata wakati wa kutendeana na watu wa Kitabu:
Wala msijadiliane na Watu wa Kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipo kuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Na semeni: Tumeyaamini yaliyo teremshwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake.”  (al-Ankabut, 46)
Katika aya hiyo, Watu wa Kitabu wanashughulikiwa katika makundi mawili:
1. Kundi la Wajeuri.
2. Kundi la Waadilifu.
Tunaamrisha kutendeana nao kwa njia bora kabisa. Mtazamo huu utawavutia kuja katika Uisilamu na hawatopata tabu kuukubali Uisilamu kwa sababu wakiukubali hawana haja ya kumkataa Musa (Moses) na Isa (Jesus).  Hivyo, wataifuata dini ya Mtume wa mwisho na wataokolewa na kuwa ni wafuasi wa dini iliyogeuzwa.
Quran inaeleza kuwa Wakristu wako karibu na Uisilamu kuliko Wayahudi:
Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na Washirikina. Na utawakuta walio karibu mno kwa mapenzi ni wale wanao sema: Sisi ni Manasara. Hayo ni kwa sababu wapo miongoni mwao makasisi na wamonaki, na kwa sababu wao hawafanyi kiburi.” (al-Maida, 82)
Historia inaithibitisha aya ya hapo juu. Idadi ya Wayahudi walioukubali Uisilamu ni ndogo mno. Hata hivyo, Wakristu wengi wameukubali Uisilamu kutokana na utafiti wao. Idadi ya Wakristu walioukubali Uisilamu barani Ulaya ni zaidi ya mamia kwa maelfu. Makanisa mengi yamegeuzwa kuwa misikiti barani Ulaya na yanahudumia kuwa ni vituo vya Kiisilamu kwa sasa.

Matunda mema ya shughuli za Kiisilamu katika nchi za Kikristu ni ukweli; hata hivyo, ni ukweli pia kuwa wakuu wa nchi hizo wana msimamo dhidi ya Uisilamu.

Allah Mtukufu, anaetuamuru tutendeane na kundi adili la Watu wa kitabu kwa njia bora kabisa, anaeleza yafuatayo kuhusu kundi katili:
Piganeni na wasio muamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho, wala hawaharimishi alivyo harimisha Mwenyezi Mungu na Mtume, wala hawashiki Dini ya Haki, miongoni mwa walio pewa Kitabu, mpaka watoe kodi kwa khiari yao, hali wamet’ii.” (at-Tawba, 29)
Suala la kuwa ima sifa zilizotajwa katika aya hiyo “zinahusisha Watu wa Kitabu wote au hapana?” ni kitu cha kujadiliwa. (4) Haipaswi kupuuzwa kuwa aya hiyo haisemi kuwa, “piganeni na Watu wa Kitabu wote mpaka walipe Jizyah (Kodi)” lakini inasema, “piganeni na wale miongoni mwa Watu wa Kitabu wenye sifa hizi na zile.” (5) Matendo ya Mjumbe wa Allah (s.a.w.) yalikuwa kama hivyo. Wakati wa zama za Makkah za Uisilamu, Mtume (s.a.w.) aliwatuma baadhi ya Waisilamu kwenda Ethiopia, ambayo ilikuwa ni nchi ya Kikristu, na kusema kuwa watakuwa salama wakiwa huko. Wakati wa zama za Madinah, Mtume aliingia katika mazungumzo na Wayahudi na Wakristu, akiwataarifu kuhusu dini ya Uisilamu na kujaribu kuwashawishi. Baadhi ya Watu wa Kitabu waliukubali Uisilamu kutokana na matendo haya.
Kama inavyoelezwa katika Quran, “Wote hao (watu wa Kitabu) si sawa sawa,” (Aal-i Imran, 113). Ni kinyume na Quran na ukweli wa kihistoria kuwazingatia wote kuwa ni sawasawa katika kundi moja.
 
Aya ifuatayo haizuii kutoingia katika mazungumzo na wao na kuwa na mahusiano ya kibinadamu pamoja nao. “Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.”  (al-Maida, 51) Kwa kweli, kuwaoa wasichana na wanawake wa Watu wa Kitabu kumeruhusiwa na Quran. (al-Maida, 5)

Hamdi Yazir anaeleza yafuatayo kuhusiana na aya iliyotajwa-hapo-juu: Waumini hawakatazwi kuwafanyia hisani Wayahudi na Wakristu, kuwafanya marafiki na kuwapa usimamizi; wanakatazwa kuwafanya ni marafiki zao wa ndani na wasaidizi wa uovu kwa sababu hawawezi kuwa ni marafiki wa kweli wa waumini. (6)
Inawezekana kufupisha suala hili kama ifuatavyo: Ni jambo la kuwa na mahusiano ya kiutu pamoja nao na ni jambo jengine kuishangaa dini yao, desturi zao na mila; yaliyopita hayakatazwi na Quran lakini ya baadaye ndio yanayokatazwa.
Marejeo:
1. Yazır, II, 1132
2. Razi, XVI, 37
3. Yazır, IV, 2512
4. Riza, X, 333; Qutub, III, 1631-1634
5. Ateş, III, 1133-1134
6. Baydawi, II, 211

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU