Msikiti Mtukufu unapatikana katika mji wa Makka, magharibi ya rasi ya Arabuni. Katika Uislamu, msikiti huu una sifa nyingi takatifu za kipekee, na miongoni mwa sifa hizo ni hizi: Ndani ya msikitini wa Makka kunapatikana Kaaba Takatifu: Kaaba ni jengo la pande nne na takriban lenye umbo la ujazo. Ipo katikati ya Msikiti Mtukufu katika mji wa Makka. Kaaba ndio Kibla ambacho Waislamu wanaelekea hapo wakati wa kuswali, na wakati wa kufanya ibada nyingine ambazo Allah ameziamrisha. Nabii Ibrahimu kipenzi cha Allah na mwanawe Ismail, Allah awafikishie rehema na amani, ndio walioijenga kwa amri ya Allah Mtukufu, kisha jengo lake limefanyiwa maboresho mara nyingi. Allah amesema kuwa: «Na (kumbukeni) wakati Ibrahimu alipoinua kuta za nyumba (Kaaba yeye na) na Ismaili wakasema: Ewe Mola wetu, tukubalie. Hakika, wewe tu ndiye mwenye kusiki, mwenye kujua». (Sura Abaqara, aya 127) Mtume Muhammad,swallalahu alayhi wasalam, alishiriki yeye na makabila ya Makka katika...
Comments
Post a Comment