NDOA KATIKA UISLAMU

Ndoa katika Uislamu (kwa Kiarabu nikah) ni mapatano ya kisheria kati ya mwanamume na mwanamke. Inafungwa kwa njia ya mkataba wa ndoa ambao mara nyingi ni wa kimaandishi mbele ya mashahidi wawili na mlezi (wali) wa bibi harusiTalaka inawezekana kwa masharti fulani. Washia wana pia ndoa ya muda (kwa Kiarabu mutʻa) ambapo muda fulani hukubaliwa kati ya wanandoa.
Katika mapokeo ya Uislamu ndoa hutiliwa moyo kwa kukumbuka tamko la mtume Mohammad: “Enyi vijana, aliye na uwezo wa kuoa aoe, kufanya hivyo kutamsaidia kuinamisha macho yake chini na kuwa mtii. Na utii ni sehemu ya imani”. (Bukhari)
Katika aya mbalimbali Qur'an inasema kuwa Mungu ameumba waume na wake ili waishi pamoja kwa mapenzi, wazae watoto na kuishi kwa amani na utulivu; kwa njia hiyo wataweza kutii amri zake na kufuata mafundisho ya Mtume wake.

Umuhimu wa ndoa katika Uislamu na jamii kwa ujumla[hariri | hariri chanzo]

Katika Uislam ndoa ina faida kubwa na nyingi mno kwa jamii. Faida za ndoa ni kama zifuatazo:
1. Kujenga undugu katika jamii.
2. Njia halali ya kuzaliana
3. Ni kitendo cha uchaji Mungu
4. Njia mojawapo ya ibada. "Mnapokuwa katika ndoa mnakuwa mpo katika kumuabudu Mwenyezi Mungu na kufuata mwenendo wa mtume wake".
Kwa ujumla suala la ndoa ni muhimu na ni lazima kwa jamii. Maneno haya yanathibitishwa na wanazuoni kama Imamu Abu HanifaAhmad bin Hanbal na Malik wanaosema, "Ingawa asili yake inaonekana ni jambo lisilokuwa la lazima, lakini kwa baadhi ya watu linakuwa ni lazima (wajibu)".
Wanazuoni wamefikia makubaliano kuwa ndoa ni lazima kwa Muislamu mwenye uwezo wa kumhudumia mke. Allah ameahidi kuwasaidia wale wenye kuoa kwa ajili ya kujikinga pale aliposema: “Waozesheni miongoni mwenu wale walio wajane na wema miongoni mwa wajakazi wenu waume au wake iwapo masikini, Allah atawatajirisha kutokana na hazina zake”. (24:32)

Wanawake wasioruhusiwa kuolewa

Kwa mujibu wa Uislamu, wanawake wafuatao hawaruhusiwi kuolewa na yule mtu anayehitaji kuoa.
1. Mke wa baba. Mke wa baba yako (mama) huruhusiwi kumuoa. Mke huyo awe ameachika au amefiwa na mume wake, yaani, baba yako.
2. Mama, wakiwemo mabibi wa pande zote. Mama yako mzazi na yeye pia haramu kwako. Mama yako pamoja na bibi zako wote upande wa mama na baba.
3. Binti, wakiwemo wajukuu wa kike kutokana na watoto wako wa kike au wa kiume. Ikiwa una mtoto wa kike pamoja na watoto wa mtoto wako wa kike au wa kiume (wajukuu) nao huruhusiwi kuwaoa.
4. Dada, akiwemo wa baba au mama mmoja. Dada yako ikiwa mmechanga baba au mama mmoja na yeye pia huruhusiwi kumuoa.
5. Shangazi kwa baba, au mama mmoja na baba.
6. Binti wa kaka. Yaani mwanao (mtoto wa kaka yako).
7. Binti wa dada. Mwanao, mtoto wa dada yako.
8. Mama aliyekunyonyesha. Ikiwa kuna mama ambaye alishiriki katika kukunyonyesha wakati wa utoto wako, huyo naye ni haramu kwako.
9. Mabinti wa mama aliyekunyonyesha. Watoto wa mama aliyekunyonyesha pia haramu kuwaoa.
10. Mkwe wako wa kike (mama wa mke). Mama yako mkwe, mama wa mkeo pia huruhusiwi kumuoa.
11. Ndugu wawili wa kike kuwaoa wakati mmoja. Yaani, huwezi kuwaoa mtu na dada yake.
12. Mwanamke mshirikina (anayeabudu sanamu). Ikiwa utabaini kuwa ni mshirikina, yaani, anayeabudu vitu vingine mbali na Muumba wake, huyo ni haramu kumuoa.
13. Kahaba. Mwanamke yeyote ambaye shughuli zake kubwa ni umalaya, naye ni haramu kumuoa.

Wanawake wasioruhusiwa kuchumbiwa

1. Mwanamke aliye katika eda.
2. Mwanamke aliyechumbiwa na mume mwingine.

Mambo yatakikanayo kutimia ili ndoa ikamilike kufungwa[hariri | hariri chanzo]

1. Muoaji na muolewaji.
2. Mashahidi wawili.
3. Mahari (Kama zawadi kwa mwanamke).
4. Mlezi: Baba au mwakilishi wake wa kutoa idhini.
5. Kauli ya kuozesha na kukubali.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU