Muumini ni nani? Ni zipi sifa za muumini?

Muumini ni mtu anayemwamini Allah, ahera  na misingi ya Imani. Kama mtu atasema yeye ni muislamu atazingatiwa kuwa ni muislamu.
Tunaweza kuorodhesha sifa kuu za muislamu ambazo Allah amezitaja katika Qur’an kama ifuatavyo:
Waumini humuamini Allah pekee. Hakuna dhati nyengine isipokuwa yeye wanayoiabudu akilini mwao. (al-Fatiha, 1/1-7; an-Nisa, 4/36)
Wanamuogopa Allah. Huepuka kufanya mambo ambayo yamekatazwa na Allah au yaliyo kinyume na radhi zake. (Aal-i Imran, 3/102; Yasin, 36/11; at-Taghabun, 64/15-16; az-Zumar, 39/23)
Wanamuamini Allah pekee. (al-Baqara, 2/249; at-Tawba, 9/25-26)
Hawamuogopi yeyote ila Allah. (al-Ahzab, 33/39)
Wanamshukuru Allah. Kwa hivyo, kuwa na matatizo ya kiuchumi au kuwa katika hali nzuri haiwafanyi wasikitike au kujivuna. (al-Baqara, 2/172; al-Isra, 17/3; Ibrahim, 14/7)
Wameamini kutokana na elimu ya hakika. Hawana mawazo ya kurudi bila ya kupata radhi za Allah. Wanaendelea kuhudumia dini yao kwa ari kila siku. (al-Hujurat, 49/15; al-Baqara, 2/4)
Wanashikamana na Qur’an. Hupangilia matendo yao yote kwa mujibu wa Qur’an. Ni wenye kuacha mara moja kufanya jambo pale wanapogundua ni lenye kukinzana na Qur;an. (al-Araf, 7/170; al-Maida, 5/49; al-Baqara, 2/121)
Wanamtaja Allah daima. Wanajua kuwa Allah huona na kusikia kila kitu; Ni wenye kuweka akilini mwao daima kuwa nguvu za Allah hazina ukomo. (Aal-i Imran, 3/191; ar-Rad, 13/28; an-Nur, 24/37; al-Araf, 7/205; al-Ankabut, 29/45)
Ni wenye kufahamu udhaifu wao mbele ya Allah. Ni wapole. Hata hivyo haina maana ya kuonekana dhaifu mbele ya watu wengine na kuwa wanyonge. (al-Baqara, 2/286; al-Araf, 7/188)
Ni wenye kufahamu kuwa kila kitu hutoka kwa Allah. Kwa hivyo, hawapatwi na fazaa wanapokutwa na jambo; huwa na subira na kuegemea kwa Allah. (at-Tawba, 9/51; at-Taghabun, 64/11; Yunus, 10/49; al-Hadid, 57/22)

Ni wenye kutazamia maisha ya ahera; wameamua kuwa ahera ndiyo lengo lao kuu. Hata hivyo, hufaidika na neema za duniani; Ni wenye kujaribu kutengeneza mazingira ambayo ni kama pepo hapa duniani. (an-Nisa, 4/74; Sad, 38/46; al-Araf, 7/31-32)
Ni wenye kuwafanya waumini peke yao kuwa ndiyo marafiki zao na wanaowaamini. (al-Maida, 5/55-56; al-Mujadala, 58/22)
Ni wenye akili. Daima wapo makini, kwa sababu wana ufahamu wa ibada zao. Daima huwahudumia waumini na dini kwa kutumia akili. (al-Mumin, 40/54; az-Zumar, 39/18)
Ni wenye kupambana kiakili kwa nguvu dhidi ya wakanushaji kwa ajili ya Allah. Hususan wakanushaji wakubwa. Huendelea na mapambano yao bila ya hofu wala uvivu. (al-Anfal, 8/39; al-Hajj, 22/78; al-Hujurat, 49/15; at-Tawba, 9/12)
Hawana woga wa kusema ukweli. Hawana hofu ya kuuweka wazi ukweli kwa kuhofia watu. Hawaogopi wakisemacho wakanushaji dhidi yao; hawapuuzi mashambulizi na dhihaka zao; Hawaogopi kukosolewa na wale wenye kuwalaumu. (al-Maida, 5/54, 67; al-Araf, 7/2)
Kufikisha dini ya Allah kwa watu. Ni wenye kuwaita watu katika dini ya Allah kwa kutumia njia tofauti. (Nuh, 71/5-9)
Si madhalimu. Ni wenye huruma na huathirika na shida za wengine. (an-Nahl, 16/125; at-Tawba, 9/128; Hud, 11/75)
Ni wenye kujizuia na hasira; ni wenye uvumilivu na kusamehe. (Aal-i Imran, 3/134; al-Araf, 7/199; ash-Shura, 42/40-43)
Ni waaminifu. Huonyesha utu wenye nguvu na husifika kwa kujiamini. (ad-Duhan, 44/17-18; at-Takwir, 81/19-21; al-Maida, 5/12; an-Nahl, 16/120)
Wanaumizwa na ukandamizaji na ukatili. (ash-Shuara, 26/49, 167; al-Ankabut, 29/24; Yasin, 36/18; Ibrahim, 14/6; an-Naml, 27/49, 56; Hud, 11/91)
Ni wenye kuvumilia shida. (al-Ankabut, 29/2-3; al-Baqara, 2/156, 214; Aal-i Imran, 3/142, 146, 195; al-Ahzab, 33/48; Muhammad, 47/31; al-Anam, 6/34)
Hawana hofu na dhulma pamoja na umauti. (at-Tawba, 9/111; Aal-i Imran, 3/156-158, 169-171, 173; ash-Shuara, 26/49-50; as-Saffat, 37/97-99; an-Nisa, 4/74)
Ni wenye kupambana na mashambulizi na vitimbi ya wakanushaji. (al-Baqara, 2/14, 212)
Wapo chini ya himaya ya Allah. Vitimbi vyote dhidi yao hushindwa. Allah huwafanya washindi kwa kuwahami dhidi ya uzushi wote na vitimbi. (Aal-i Imran, 3/110-111, 120; Ibrahim, 14/46; al-Anfal, 8/30; an-Nahl, 16/26; Yusuf, 12/34; al-Hajj, 22/38; al-Maida, 5/42, 105; an-Nisa, 4/141)
Ni wenye umakini mkubwa dhidi ya wakanushaji. (an-Nisa, 4/71, 102; Yusuf, 12/67)
Ni wenye kuwafanya maadui shetani na wafuasi wake. (Fatir, 35/6; az-Zukhruf, 43/62; al-Mumtahina, 60/1; an-Nisa, 4/101; al-Maida, 5/82)
Ni wenye kupambana na wanafiki; hawautumii muda wao pamaja nao. (at-Tawba, 9/83, 95, 123)
Ni wenye kujikinga na udhalimu wa wakanushaji. (al-Ahzab, 33/60-62; al-Hashr, 59/6; at-Tawba, 9/14-15, 52)
Ni wenye kufanya mambo yao kwa kushauriana. (ash-Shura, 42/38)
Hawana wivu au kuiga maisha ya kifahari ya makafiri. (al-Kahf, 18/28; at-Tawba, 9/55; Taha, 20/131)
Hawaathiriki na utajiri na cheo. (al-Hajj, 22/41; al-Qasas, 28/79-80; an-Nahl, 16/123)
Ni wenye uangalifu na umakini kuhusu ibada; wanatekeleza sala, funga na ibada kwa uangalifu. (al-Baqara, 2/238; al-Anfal, 8/3; al-Muminun, 23/1-2)
Hawafuati wingi bali vipimo vilivyowekwa na Allah. (al-Anam, 6/116)
Ni wenye kupambana kwa nguvu ili kufika kwa Allah na kuwa waumini wa kupigiwa mfano. (al-Maida, 5/35; Fatir, 35/32; al-Waqia, 56/10-14; al-Furqan, 25/74)
Si wenye kutenda kwa kuegemea ushawishi wa shetani. (al-Araf, 7/201; al-Hijr, 15/39-42; an-Nahl, 16/98-99)
Hawawafuati wazee wao kwa upofu. Wanatenda kwa mujibu wa Qur’an. (Ibrahim, 14/10; Hud, 11/62, 109)
Hawapotei kwa israfu. (al-Anam, 6/141; al-Furqan, 25/67)
Wanajihifadhi kutokana na zinaa na huoa kwa njia ambayo Mwenyezi Mungu anataka. (al-Muminun, 23/5-6; an-Nur, 24/3, 26, 30; al-Baqara, 2/221; al-Maida, 5/5; al-Mumtahina, 60/10)
Hawana kupita kiasi katika dini. (al-Baqara, 2/143; an-Nisa, 4/171)
Sio wabinafsi (al-Insan, 76/8; Aal-i Imran, 3/92, 134; at-Tawba, 9/92)
Wanatilia umuhimu usafi. (al-Baqara, 2/125, 168; Muddaththir, 74/1-5)
Hawachunguzani. (al-Hujurat, 49/12)
Wanaepuka uchoyo. (an-Nisa, 4/128)
Wanaomba msamaha kwa Allah. (al-Baqara, 2/286; Aal-i Imran, 3/16-17, 147, 193; al-Hashr, 59/10; Nuh, 71/28)
Maswali juuyau islamu

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU