Kwa nini Uislamu ni dini ya kweli?

Dear Brother / Sister,

Kwa nini Uislamu ni dini ya kweli?

“Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio pewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi ulio kuwa baina yao. Na anaye zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.” Qur’an, Familia ya Imran (Aal-i Imran); 19 (3: 19)
Dini inamaanisha “malipo kwa mtindo wa malipo au adhabu” na inaeleza uhusiano kati ya mfuasi na kiongozi mwenye madaraka. Kama neno lenyewe lilivyo, umetolewa ufafanuzi kadhaa wa neno dini. Zipo tofauti za kimsingi kati ya fafanuzi zinazotolewa na wanasayansi wa Kimagharibi (Ulaya) na wanazuoni Waislamu. Bado, kuna tofauti za kimsingi kati ya rai za pande zote mbili kuhusu chanzo cha dini na njia yake ya kimsingi ya kutokea. 
Kwa mujibu wa rai ya Kiislamu, dini inamaanisha ukamilifu wa kanuni unaomwongoza mwanadamu ili aweze kuishi kulingana na lengo aliloumbiwa na ili atambue lengo hilo katika nidhamu mahusussi. Dini ni msingi unaorekebisha uhusiano unaozingatia amri tukufu na utawala wa upande mmoja na utii na ufuasi wa upande wa pili, isipokuwa inafahamika kutokana na aya ambayo kwa mujibu wa Qur’an, thamani ya dini na kujitolea kumewekwa ili kuzingatie utii wa hiari. Kwa maneno mengine, kwa mujibu wa ufahamu wa Kiislamu, dini ni msingi unaoelekeza watu wenye kufahamu waelekee kwenye mema (kwa vitendo) na furaha kwa matakwa yao, na sheria ya kiungu inayorekebisha vitendo vya watu kwa kuzingatia uchaguzi wao.
Aya hiyo ndio sehemu ya kwanza ambayo neno Uislamu limetajwa katika Qur’an Tukufu. Maana ya Uislamu katika kamusi ni “kuwa mwaminifu, kutii, kujisalimisha na kuwa katika mwelekeo na amani”. Kama neno, Uislamu linamaanisha “kukubali kuwepo kwa mambo yote aliyotangaza Mtume Muhammad (s.a.w) kwa niaba ya dini na kuwa katika utii unaoidhihirisha hayo”. Jina la dini ya kweli aliyotumwa Mtume ni Uislamu. Bado, katika lugha ya Kiarabu, Uislamu ni hali isiyo na kikomo inayoonesha kuitii dini hiyo. Mtu anayefuata dini ya Uislamu ametajwa kuwa ni Muslam katika lugha ya Kiarabu na kama musalman katika lugha ya Kiajemi. Katika lugha ya Kituruki, maneno Islamiyet na Muslumanlik hutumika kwa ajili ya dini hiyo na neno musluman hutumika kwa mtu anayefuata dini hiyo.
Kuna uhusiano mkubwa kati ya maana ya neno Uislamu kwenye kamusi. Kwa mujibu wa ufahamu wa Kiislamu, dini ni sheria inayoeneza muwafaka kwa kuzuia kutoafikiana na ukinzani kati ya viumbe wenye matakwa na akili. Dini inaeleza muwafaka si miongoni mwa watu tu isipokuwa pia kati ya watu na Allah. Kwa njia hii, ukubalifu kati ya matakwa ya Muumba na matakwa ya viumbe huenezwa.     
Kwa kuwa dini zote za kimbinguni zina msingi wa kumpwekesha Allah, dini ya Uislamu aliyoijulisha Mtume Muhammad na dini zingine zilizotangazwa na mitume wengine kimsingi zinalingana. Hata hivyo, kwa mujibu wa baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu, maneno kama vile dini ya Uislamu na jamii ya Kiislamu yanaweza tu kutumika kwa ajili ya dini aliyotummwa Mtume Muhammad na wafuasi wake. Ingawa Uislamu unaafikiana na dini za kweli zilizotangulia, dini hiyo ina baadhi ya sifa mahususi na baadhi ya maamrisho mahususi ya kipekee kwa jamii inayoifuata. Kwa mujibu wa kundi jingine la wanazuoni, pia inawezekana kwa dini zilizotangulia za mbinguni kuweza kuitwa Uislamu. Wanaeleza kuwa, katika Qur’an Tukufu kuna aya kadhaa zenye kuunga mkono rai hiyo: maneno ya majibu ya mitume wa Yesu kuwa “Shuhudia kuwa sisi ni Waislamu”, maelezo kuhusu Ibrahim kuwa “Alikuwa Muislamu hanif” na tena kutoa nafasi ya sifa ya ujumla kama vile “Amekupeni jina ‘Waislamu’ hapo kabla na hata sasa” ni mifano ya hilo. Kulingana na mtu kuwa na mitazamo kinzani, maelezo kama hayo yanawahusu Mitume.
Kwa mtazamo wetu, katika vitabu vitukufu isipokuwa Qur’an Tukufu, neno dini halikutajwa kwa ajili ya wafuasi wa vitabu hivyo na kama tutaona maneno kama vile Uyahudi na Ukristo yalitokea baadaye na yakatumiwa kwa ajili ya wafuasi wao baadaye, maana ya maneno “Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu” yanaweza kufahamika kirahisi. Ingawa dini ilitangazwa na Mtume Muhammad ina kanuni mahususi, huku Qur’an ikithibitisha kwa msisitizo tamko la mitume waliotangulia linaloonesha kuwa walchotangaza kimsingi lilikuwa katika Uislamu; hata hivyo, kwa mujibu wa hekima ya kiungu, njia kamilifu zaidi ya imani hiyo inaweza tu kufikiwa kwa kutumwa Mtume Muhammad.
Kwa hali hiyo,njia pekee ya kuweza kupata radhi za Mtukuka Allah ni kuamini yote Anayoyasema. Kutokana na hayo, kwa kuanzia katika uhalisia, ingawa majina ya dini hizo zingine yanaweza kuwa yalitajwa ili kueleza itikadi fulani, muwafaka wa watafutaji ndani ya mipaka ya Allah Mtukuka unathibitisha lengo la msingi na haliepukiki kwa wakati uliotakiwa kwa ajili ya matamko ya Kiungu ili kuingiza fikra hiyo katika akili na dhamiri ya wanadamu. Wanazuoni wa Kiislamu wameeleza ufahamu huo kama “jamii tiifu” na “jamii iliyolinganiwa”; neno la kwanza hapo linaeleza watu wanaoendea matakwa yao ya utii kwenye yale haswa yaliyotangazwa na kudhihirishwa na Mtume Muhammad; na la pili linaeleza kundi linalowezekana kuwa hivyo ambalo bado halijafikia kiwango hicho isipokuwa katika kipindi cha tafakuri kilichotajwa hapo. Kwa hivyo,kwa kulinganisha na majina kama vile “Uyahudi” na “Ukristo”, baadhi ya waandishi wa Kimagharibi wanaouita Uislamu kwa kulifinya ina kuwa ni “Umuhammadi” halifai kwa sababu liko mbali na ukweli na pia lina sifa ya kuzuia mawasiliano pamoja na yaliyotajwa hapo juu.
Kuifahamu aya kwa njia hiyo katika nukta ya lengo kuu haikinzani na fikra kuwa kilammoja aliyeishi katika wakati wowote au mahali popote na akaacha kumshirikisha Allah na kuweza kujielekeza katika imani hiyo anaweza kuitwa “Muislami” kwa mujibu wa ufahamu wa Qur’an’. Kwa hakika, katika aya kadhaa, inaweza kuonekana kuwa vigezo hivyo vimezingatia kukokoka watu katika ahera.
Kwa maana pana, Uislamu (kuwa Muislamu) unaeeza utii moyo, ulimi na tabia. Utii muhimu zaidi na wa thamani kubwa kati ya hayo ni wa moyo. Katika Qur’an, kunaonekana kuwa neno Uislamu pia linatumika kwa ajili ya utii ambao haujafikiakiwango cha imani.
Maneno “Waliopewa vitabu” limefahamika kwa ujumla kuhusiana na yaliyomokwenye maneno “Watu wa Kitabu”. Neno elimu limeelezwa kama “ufunuo na shuhuda waziwazi”. Katika aya, matamshi ya watu wa Vitabu wanaoangukia katika ridhaa baada tu ya elimu kuja ni kwa ajili ya kuonesha kuwa walijulishwa kiasi cha kutosha kuhusu matamshi ya Kiungu na ingawa hawana udhuru kwa hilo, wanaangukia katika vurugu na kugombana kwa sababu ya makosa yao na kwa kufikiria manufaa yao na tamaa za kibinadamu. Kwa kuanzia na “Kwa sababu ya dhuluma miongoni mwao”, baadhi ya maelezo yalitolewa na watu yaliyodokezwa hapa yalikuwa yanawahusisha Wayahudi au Wakristo au makundi yote mawili. Nuru ya elimu ya kihistoria, hapa, inaweza kusemwa kuwa badala ya kusonga mbele katika njia ya amani na ustaarabu kwa kutumia ufunuo mwongofu uliowekewa, jamii, zilizoambiwa kwa ufunuo wa kiungu, huku akili ya kawaida ikiwekwa mbali kwa sababu ya matakwa ya kibinafsi na hususani kutenganisha katika makundi ya kidini kwa kuzingatia kuwa matakwa yao kinzani yamekosolewa. Licha ya onyo hilo, kukariri kosa hilohilo kwa wanaoamini Qur’an kumesababisha kizuizi muhimu katika kutimiza Mpango wa kufikisha ujumbe wa Kiungu kwa wanadamu kwa njia bora zaidi na kuchukua nafasi wanayostahiki katika the mashindano ya ustaarabu.
Maswali juuyau islamu

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU