Nyalandu Apenya CHADEMA kwa Ushindi wa Asilimia 66

Lazaro Nyalandu aliyewahi kuwa Mbunge wa Singida Kaskazini kupitia CCM, leo Desemba 1, 2019, katika uchaguzi uliofanyika Jijini Dodoma, hatimae amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Kanda ya Kati kwa kupata Kura 60 kati ya 86 zilizopigwa na kufanya ushindi wake kuwa ni wa asilimia 66.


Matokeo hayo yametangazwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa chama hicho Patrick Sosopi, ambapo amesema kuwa Nyalandu amemzidi kete aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda hiyo Alphonce Mbasa, ambaye amepigiwa Kura 26, ambazo ni sawa na asilimia 33.2.

Kwa mujibu wa Sosopi, Kura zilizopigwa ni 86 na hakuna iliyoharibika.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

Kisa Cha Nabii Ibraahiym عليه السلام - Sehemu Ya 1