Na Mwandishi Wetu Serikali imeanza mpango wa kuwa na vituo vya malezi kwa watoto nchini nzima ili kuhakikisha wanajamii wanayapa kipaumbele malezi na makuzi kwa watoto ili kuhakikisha kunakuwa na taifa madhubuti. Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akihitimisha Semina ya Mafunzo ya Elimu ya Malezi, maendeleo na makuzi kwa wakufunzi kutoka vyuo vya Maendeleo ya Wananchi. Dkt. Jingu amesema kuwa vituo hivyo vitaratibiwa na Serikali ila vitaendeshwa na kusimamiwa na wananchi katika maeneo yao na mpaka sasa kuna zaidi ya vituo 1500 nchi nzima na vingine vinaendelea kuanzishwa. Ameongeza kuwa malezi ni msingi mkubwa katika kuhakikisha tunapata kizazi chenye maadili, uwajibikaji na uzalendo katika kizazi itakayosaidia kujenga taifa bora. "Mafunzo haya ni muhimu na mmeamua suala sahihi, watoto wanahitaji malezi ya karibu na sio malezi tu bali wapate malezi sahihi" alisema Dkt. Jingu Dkt. Jingu pia amewataka washiriki wanatumia stadi hiyo kuisaidia jamii na nchi kuweza kuwa na muelekeo mzuri kwa kuwa na vijana wazalendo wawajibikaji kwa maendeleo ya taifa. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Noel Mbonde amesema kuwa Wizara ya Elimu itahakikisha inashirikiana na wadau wa maendeleo kuhakikisha Elimu ya Malezi, maendeleo na makuzi kwa watoto inatekelezwa. Ameongeza kuwa Wizara ya Elimu imehakikisha kila Chuo cha Maendeleo ya wananchi kinakuwa na kituo cha kulea watoto ili kuhakikisha inawasaidia watoto. Naye Mwakilishi wa washiriki ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mbinga Bw. Lotty Mwang'onda amesema kuwa mafunzo waliyoyapata yatawasaidia kuleta mabadiliko hasa katika jamii inayowazunguka katika vyuo vyao ili kuhakikisha malezi, maendeleo na makuzi yanazingatiwa katika ukuaji wa mtoto. Ameongeza kuwa wao kama washiriki wameshukuru kwa uzoefu na kama wataalam wa wanaofanya kazi na jamii watashirikiana na jamii kuhakikisha elimu walioyoipata inawafikia jamii inayowazunguka. Aidha Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Karibu Tanzania KTO Bw. Aidan Mchawa ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa ushirikiano wao na asasi za kiraia katika kuhakikisha wanatoa huduma kwa wananchi na kuhakikisha program ya Malezi, maendeleo na makuzi ya awali ya mtoto inarudisha misingi ya malezi ya mtoto hasa wa kitanzania. Naye mshiriki Bi. Felister Nanguka ameishukuru Serikali kwa kuwezesha upatikanaji wa elimu ya mafunzo ya Malezi, maendeleo na makuzi katika jamii hasa vijijini na kuahidi kufanya kazi hiyo kwa nguvu zao kwa kukaza msuli ili kuhakikisha watoto wanapata malezi stahili. Shirika la Karibu Tanzania KOT limeandaa mafunzo kwa wakufunzi kutoka vyuo kumi vya Maendeleo ya Wananchi nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu malezi, maendeleo na makuzi ya awali ili wakaitoe elimu hiyo kwa jamii inayowazunguka.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amemuelekeza Inspekta Jenerali wa Polisi Nchini, Simon Sirro kuwaondoa Makamanda wa Polisi wa Mikoa Miwili ya Kusini Pemba   na Kaskazini Pemba kwa kushindwa kutekeleza Mradi wa Ujenzi wa Nyumba 16 za Makazi ya Polisi uliozinduliwa mwishoni mwa mwaka 2018 na Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan pamoja na kuacha mikutano ya siasa ya Chama cha ACT Wazalendo  kuendelea Kisiwani Pemba  hali ambayo  kukaidi agizo la Kiongozi Mkuu wa Nchi..

Masauni ametoa agizo hilo jana Alhamisi Desemba 12, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Unguja.

Amesema kwa muda mrefu kisiwa cha Pemba kimekuwa na matukio yasioridhisha jambo linaloashiria kuwa wameshindwa kazi.

Makamanda hao ni Hassan Nassir Ally wa Mkoa wa Kusini Pemba na  Sheikhan Mohamed Sheikhan wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Akitoa mfano wa matukio hayo, Masauni amesema Maalim Seif anafanya mikutano kila kona huku ikijulikana kuwa imezuiwa.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU