Rais Magufuli amshukuru Spika na Wabunge 'Mmenitia moyo na kunipa nguvu'

Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemshukuru Spika wa Bunge, Job Ndugai na Wabunge kwa azimio la kumpongeza.

Rais Magufuli amesema kuwa wamemtia moyo na kumpa nguvu zaidi ya kufanya kazi huku akiwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya Bungeni.

"Mhe. Spika. Nakushukuru wewe na Wabunge kwa azimio la kunipongeza. Mmenitia moyo na kunipa nguvu zaidi ya kufanya kazi. Nami nawapongeza kwa kazi nzuri mnazofanya Bungeni na Majimboni kwenu. Mbarikiwe sana.Kwa niaba ya Serikali naahidi kuendelea kushirikiana na Bunge letu Tukufu," ameandika leo Rais Magufuli kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

Kisa Cha Nabii Ibraahiym عليه السلام - Sehemu Ya 1