Picha: Hiki Ndicho Kilichomkuta Mchezaji Huyu Maarufu wa Simba SC

Mlinzi wa pembeni wa Simba Sports Club na Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ hii leo amesherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa sambamba na wachezaji wenzake.

Kwenye furaha hizo za kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, Zimbwe Jr amejikuta akiyakoga matope kutoka kwa baadhi ya nyota wenzake ambao alikuwa nao.

Katika kusherehesha tukio hilo klabu yake ya Simba iliandika kuwa sasa ni zamu yake maana kwa muda mrefu amekuwa akiwashughulikia wenzake tu.

”Baada ya kuwashughulikia wenzake kwa muda mrefu, leo imekuwa zamu ya Mohamed Hussein. Shughuli imefana sana ” Imeandika Simba SC.


Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

Kisa Cha Nabii Ibraahiym عليه السلام - Sehemu Ya 1