Mbabe Wa ahukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa makosa ya uhalifu DRC


Kiongozi wa zamani wa waasi wa Congo amehukimiwa kifungo cha miaka 30 jela la Mahakama ya Kimataifa ya jinai kwa makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu .

Waoiiganaji waliomtii Bosco Ntaganda walitekeleza mauaji ya ukatili dhidi ya raia, Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), walisema mwezi Julai.

Ntaganda, ambaye alipewa jina la bandia "Terminator", alipatikana na makosa 18 mkiwemo ubakaji, utumwa wa ngono , na kuwatumikisha watoto kama wanajeshi.

Hukumu dhidi yake ni ya muda mrefu kuwahi kutolewa katika historia ya mahakama ya ICC

Onyo: Taarifa hii inaweza kuwa na maelezo ambayo yanaweza kuwaogofya baadhi ya wasomaji

Ntaganda alikuwa ni mtu wa kwanza kupatikana na hatia ya utumwa wa ngono na mahakama ya ICC kwa kwa ujumla ni mtu wa nne ambaye mahakama hiyo imempata na hatia tangu ilipoundwa mwaka 2002.

Ntaganda amnbaye alizaliwa nchini Rwanda mwenye umri wa miaka 46-muasi wa zamani amekuwa akihusika na mizozo mbali mbali ya kivita nchini Rwanda na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Wachambuzi wanasema kujisalimisha kwake katika ubalozi wa Marekani nchini Rwanda kilikuwa ni kitendo cha kujilinda kutokana na hatari iliyokuwa inamkabilibaada ya kupoteza mamlaka ndani ya kikundi chake cha waasi wa M23.

Bosco Ntaganda ni nani?

Alizaliwa nchini Rwanda 1973 ambako alikulia
Alikimbilia DRC akiwa kijana mdogobaada ya watu wa kabila lake la Watutsi kushambuliwa
Akiwa na umri wa miaka 17, alianza maisha yake ya mapigano -wakati fulani akiwa kama muasi na wakati mwingine kama mwanajeshi wa Rwanda na DRC
Baina ya mwaka 2002-3: Alikuwa kiongozi wa wanamgambo katika jimbo la Kongo la Ituri
2006: Alishtakiwa na Mahakama ya ICC kwa madai ya kuwaingiza watoto jeshini katika jimbo la Ituri
Alikuwa mkuu wa vikosi vilivyofanya mauaji ya kikatili ya Kiwanja mwaka 2008 ambapo watu 150 waliuawa
2009:Alijiunga na jeshi la taifa la Kongo akapewa cheo cha Generali
2012: Alitoroka jeshi, na kuanzisha uasi uliowalazimisha watu 800,000 kuyakimbia makazi yao
2013: Alijisalimisha katika ubalozi wa Marekani mjini Kigali nchini Rwanda, baada ya migawanyiko ndani ya kundi la waasi
2019: Amepatikana hati ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya ICC na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela
Alifanya nini?
Mwezi Julai , majaji watatu walimpata Ntaganda na hatia ya makosa yote 18 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu uliofanyika katika jimbo lenye utajiri wa madini lililoko mashariki wa DRC la Ituri kati ya mwaka 2002 na 2003.

Ntaganda alikuwa "kiongozi muhimu " ambaye alitoa amri ya "kuwalenga na kuwauwa raia" jaji Robert Fremr alisema katika hukumu yake.

Waendeshamashtaka walikuwa wamesema Ntaganda alikuwa mtu muhimu katika kupanga, na kuendesha harakati za waasi wa Union of Congolese Patriots (UCP) na tawi lake la kijeshi la Patriotic Forces for the Liberation of Congo (FPLC).

Kikundi cha kijeshi kiliendesha mashambulio dhidi ya watu walioaminiwa kuwa hawatoki katika kabila la Wahema, ICC ilibaini.

Katika shambulio moja , wapiganaji 49 waliwakamata watu katika shamba la migomba nyuma ya kijiji kwa kutumia "fimbo, vifungo pamoja na visu na mapanga ".

"Wanaume , wanawake na watoto pamoja na watoto wachanga walipatikana katika shamba hilo .Baadhi ya miili ilipatikana ikiwa uchi, baadhi yake ikiwa imefungwa kwa kamba na baadhi ilikuwa imekatwa kichwa ," Alisema jaji Fremr.

Ghasia katika jimbo hilo ziliwauwa watu zaidi ya 60,000 tangu mwaka 1999 huku wanamgambo wakipigania udhibiti wa vyanzo vichache vya madini, yanasema makundi ya haki za binadamu.

Majaji waliamua kuwa Ntaganda binafsi alimuua Padri wa kikatoliki wakati wapiganaji aliowaongoza walipofanya uvamizi jimboni humo.

Image caption
Uhalifu ulifanyika wakati Ntaganda alipohudumu kama naibu mkuu wa majeshi wa kiongozi wa waasi wa UCP Thomas Lubanga
Uhalifu ulifanyika wakati Ntaganda alipohudumu kama naibu mkuu wa majeshi wa kiongozi wa waasi wa UCP Thomas Lubanga.

Mwaka 2012 Lubanga alikuwa mtu wa kwanza kupatikana na hatia na mahakama ya ICC na akahukimiwa kifungo cha miaka 14 jela.

Wote waliopatikana na hatia hadi sasa na mahakama ya ICC wanatoka barani Afrika. Mtu wa tano , Jean-Pierre Bemba, makamu wa zamani wa rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo , awali alipatikana na hatia ya uhalifu wa kivita kabla ya kufutwa na mahakama ya rufaa ya ICC mwaka jana.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU