Mama Adaiwa Kumzika Mtoto WAKE Akiwa Hai

Polisi katika Wilaya ya Apac, nchini Uganda wameanza uchunguzi dhidi ya Mwanamke (19) anayedaiwa kumzika mwanaye wa kiume (miezi 2) akiwa hai siku ya jana (Jumatatu)

Imesemekana kuwa, mwanamke huyo alifikia hatua hiyo baada ya wazazi wake kumnyima chakula wakidai kuwa amezaa Mtoto Haramu

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ameeleza kuwa mtuhumiwa alitoweka na mtoto wake nyumbani kwao kwa muda wa siku tatu na aliporudi Jumatatu hakuwa amerudi naye na kusema kuwa amemzika baada ya kutengwa na familia

Vyombo vya Usalama Wilayani humo vimethibitisha kujiri kwa tukio hilo na vinaendelea na uchunguzi huku mtuhumiwa akiwa Rumande

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

Kisa Cha Nabii Ibraahiym عليه السلام - Sehemu Ya 1