Baada ya Kupata Ugonjwa wa Akili, Afungiwa Chumbani na Minyororo Miezi Miwili

Shadrack Johanes (26), mkazi wa Old Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga, amefungiwa chumbani akiwa uchi kwa miezi miwili akiwa amefungwa minyororo mikononi na miguuni

Ndugu wa kijana huyo wamedai kuwa, walilazimika kuchukua hatua hiyo baada ya kuwa amepata tatizo la akili kwani alianza kupiga watu, kuvunja vioo vya magari na nyumba za watu

Shangazi wa kijana huyo, Devota Emmanuel amesema kutokana na kutumia fedha nyingi kuwalipa waliokuwa wanaharibiwa mali zao waliamua kumfungia ili asiendelee kuwatia hasara

Alidai walimpeleka Hospitali ya Rufaa ya Bugando lakini madaktari hawakubaini kinachomsumbua na kuwapa rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili, lakini kutoka na hali ngumu ya maisha walishindwa kwenda Muhimbili

Amesema, “Baba yake yuko Bukoba na ameshakata tamaa. Tumemfunga minyororo hii ili asitoroke na tukimvalisha nguo anazichana, ndiyo maana tukaamua kumwacha aishi hivyo akiwa uchi"

Kaka wa kijana huyo, Golden Johanes amesema imekuwa vigumu kwao kumsaidia mdogo wake kutokana na madaktari kushindwa kubaini kinachomsumbua na anaamini huenda mdogo wake "amechezewa kishirikina"

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

Kisa Cha Nabii Ibraahiym عليه السلام - Sehemu Ya 1