Video za ngono mitandaoni zilivyokatisha maisha ya binti

Sanduku lilillobeba mwili wa Tiziana Cantone
Image captionTiziana alijikatisha uhai baada ya video zake za ngono kusambaa mitandaoni
Pengine haikuchukua muda mrefu kwa Tiziana Cantone kuanza mfululizo wa matukio ambayo yalisababisha kujikatisha uhai
Mwezi Aprili mwaka 2015, mwanadada kutoka Mugnano, nje kidogo mwa Naples,alituma picha za video za ngono kupitia WhatsApp. waliopokea video hizo miongoni mwao ni rafiki yake wa kiume Sergio Di Palo, ambaye mahusiano yake naye hayakuwa mazuri.
Video hizo zilimuonesha Tiziana akifanya vitendo vya ngono na wanaume kadhaa ambao hawakufahamika.
''Alikuwa mrembo lakini mwenye kuvunika oyo upesi,''alikumbuka Teresa Petrosino ambaye walikua marafiki kwa miaka 15.''Alikuwa na watu wasiofaa kwa wakati usiofaa.''
Video hizo zilisambazwa kwenye tovuti mbalimbali zinazoonyesha masuala ya ngono.Vitendo vyenyewe kwenye video hizo havikua kitu isipokua sentensi moja tu kutoka mdomoni mwa Tiziana Conte
''Unarekodi video?'' alimuuliza mwanaume aliyekuwa ameshika Kamera. ''Safiiii''.
Maneno hayo yaliashiria kuwa mwanadada huyo anapenda kupigwa picha wakati akifanya ngono.Sentensi hiyo ilifanya watazamaji waendelee kuitazama bila wasiwasi:Kama alikua anafurahia kupigwa picha, bila shaka hatachukia watu wakiitazama.
Lakini waitaliano walifanya zaidi ya kutazama.Watazamaji walitumia maneno yake kwa msisitizo wakatengeneza t-shirt ambazo ziliwekwa picha yake na pia kwenye tovuti.
Hakuna aliyekuwa akifikiria kuwa Tiziana asingependa, kwa kuwa alionekana kufurahia kwenye video hizo.
Lakini mambo hayakua hivyo.
''Watu huchanganya kukubali jambo na jambo hilo kusambaa zaidi,'' anaeleza mtaalamu wa masuala ya mitandao Selvaggia Lucarelli.
''Unaweza kupiga picha ya video, ukawaonesha watu kadhaa,lakini kunakua na makubaliano kuwa watu hao wasisambaze zaidi.''

Mapambano ya kisheria

Tiziana Cantone, aligopeshwa sana na hali hii.
''Mimi na yeye hatukuwahi kuongea kuhusu kilichomo kwenye video.'' alisema rafiki yake Teresa.''Sikuwahi kuziona, na sikutaka kuziona.Unaweza kuona alikuwa akisumbuka mno.''Lakini alikuwa na nguvu.''
Bi Cantone akaamua kupambana.Lakini hakukua na njia ya haraka ya kufanya ili kuondosha video hizo.
Aliipeleka kesi mahakamani, akidai kuwa video hizo zilipelekwa kwenye mitandao bila ridhaa yake.Lakini mpaka wakati huo hakuweza kuishi maisha ya kawaida.
''Hakutaka kutoka nje akiogopa watamuona.'' Alieleza Teresa.
''Alielewa kwa kiasi fulani kuwa hali hii haiwezi kutatulika;kuwa mume wake,watoto wake wanaweza kuziona video hizo siku moja;na kuwa video hizo hazitaondoka mitandaoni.''
Maria Teresa Giglio
Image captionMama wa Tiziana anapambana kurudisha heshima ya mtoto wake
Ilimchukua wiki kadhaa Mama yake Teresa Giglio kupata nguvu kuwaambia wanahabari kuhusu maisha ya binti yake.
''Binti yangu alikua na tabia njema lakini pia alikua na mapungufu yake,'' aliiambia BBC. ''Hakua na mapenzi ya baba, tangu alipozaliwa.Hakuwahi kumuona baba yake.Hii iliathiri maisha yake.''
Mama na mwana waliishi pamoja.Katika kipindi cha furaha, Tiziana alipenda kusikiliza wanamuziki wa Italia, kusoma vitabu vya simulizi, kupiga kinanda.Lakini baada ya video kutapakaa mitandaoni hali hiyo haikuwepo tena.
''Maisha yake yaliharibika, mbele ya kila mtu,'' alisema mama yake.''Watu walimfanya kichekesho,akaitwa majina mabaya ya aibu.''
Mwezi Septemba, Mahakama ya Naples iliamuru video hizo zitolewe mitandaoni na kwenye tovuti.Lakini ilimtaka Tizianz alipe faini ya dola 21,600 za marekani, gharama za huduma za kisheria.Fedha ilikua nyingi sana.
Tarehe 13 mwezi Septemba mwaka 2016, Maria Teresa Giglio alikwenda kazini, akiwa amemuacha binti yake nyumbani.
Bi Giglio alipokea simu kutoka kwa wifi yake ,sauti ikiwa ya kupoa sana ikimtaka arejee nyumbani.
Aliporejea alikuta Polisi, gari ya kubeba wagonjwa, ''haraka nikaelewa''alisema , huku akilia.
''Siku alipokufa maisha yangu yalikomea hapo.''
Tiziana na Mama yake
Image captionMama wa Tiziana anataka kufahamuu ukweli kushusu sakata la kifo cha binti yake

Nani aliweka video Mtandaoni?

Kitendo cha Tiziana Cantone kujitoa uhai, kilifanya video hizo zifuatiliwe na watu wengi zaidi kuliko kusahaulika.
Mama yake alijilazimisha azitazame video hizo.
''Nilitaka kuona kila kitu ili niweze kuuelewa ukweli.'' huyu hakua Tiziana wangu'' alishawishika kuwa binti yake alikua anatumia dawa za kulevya.
Bi Giglio amemtaka mpenzi wa zamani wa binti yake, Di Pialo, kueleza hasa alishiriki vipi katika mpango wa kusambaza video zile.
''Hakunisaidia kuokoa maisha yake.Lakini labda anaweza kunisaidia kupata ukweli.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU