UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

Msikiti Mtukufu unapatikana katika mji wa Makka, magharibi ya rasi ya Arabuni. Katika Uislamu, msikiti huu una sifa nyingi takatifu za kipekee, na miongoni mwa  sifa hizo ni hizi:
  1. Ndani ya msikitini wa Makka kunapatikana Kaaba Takatifu:
Kaaba ni jengo la pande nne na takriban lenye umbo la ujazo. Ipo katikati ya Msikiti Mtukufu katika mji wa Makka.
Kaaba ndio Kibla ambacho Waislamu wanaelekea hapo wakati wa kuswali, na wakati wa kufanya ibada nyingine ambazo Allah ameziamrisha.
Nabii Ibrahimu kipenzi cha Allah na mwanawe Ismail, Allah awafikishie rehema na amani, ndio walioijenga kwa amri ya Allah Mtukufu, kisha jengo lake limefanyiwa maboresho mara nyingi. 
Allah amesema kuwa: «Na (kumbukeni) wakati Ibrahimu alipoinua kuta za nyumba (Kaaba yeye na) na Ismaili wakasema: Ewe Mola wetu, tukubalie. Hakika, wewe tu ndiye  mwenye kusiki, mwenye kujua». (Sura Abaqara, aya 127)
Mtume Muhammad,swallalahu alayhi wasalam, alishiriki yeye na makabila ya Makka katika kuweka Jiwe Jeusi kwenye sehemu yake pale walipoijenga Kaaba upya.
  1. Pia ndio msikiti wa kwanza katika uso wa ardhi:
Swahaba Abu-dharri, Allah amridhie, alipomuuliza Mtume swallalahu alayhi wasalam kwamba: «Ewe Mtume wa Allah, ni msikiti gani wa kwanza kuwekewa ardhini? Mtume akajibu: Al-masjid Alharam. Abu-dharri akasema: Nikauliza tena: Kisha ni msikiti upi? Mtume akajibu: Al-masjid Al-aqsaa. Nikauliza: Kulikuwa na muda gani kati yake? Mtume akajibu: Miaka arubaini. Halafu, popote itakapo kukuta swala baada ya hapo, Swali kwani ubora uko hapo». (Bukhari, Hadithi Na. 3186, Muslim, Hadithi Na. 520).
  1. Kuongezwa mara dufu kwa thawabu za kuswali humo:
kasema mtume: ( malipo ya swala katika msikiti wangu huu ni bora kuliko swala elfu moja (1000)  katika mingine isipokuwa msikiti wa Makka na msikiti wa makka ni bora mara laki moja kuliko misikiti mingine) Ibnu Maja 1406-Ahmad 14694.)
  1. Pia Makka ni sehemu takatifu kwa Allah na Mtume wake swallalahu alayhi wasalam
Allah amesema kuwa: «Kwa yakini, hakuna vingine isipokuwa kwamba nimeamrishwa kumuabudu Bwana wa mji huu (Makka) ambao Allah ameutukuza. Na chake yeye tu kila kitu. Na nimeamrishwa kuwa miongoni mwa Waislamu». (Sura Annamli, aya 91).
Mji wa Makka Allah ameutukuza kwa viumbe wake na kufanya kwamba ni haramu humo kumwaga damu au kumdhulumu yeyote au kuwinda wanyama wake au kukata miti yake au majani yake. 
Mtume,swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, Allah ameitukuza Makka na wala watu sio waloitukuza. Kwa hiyo, sio halali  kwa mtu yeyote anayemuamini Allah na Siku ya Mwisho kumwaga damu humo, na mti hautakiwi kukatwa humo». (Bukhari, Hadithi Na. 104, Muslim, Hadithi Na. 1354)
  1. Makka ndio mji unaopendwa sana na Allah na Mtume wake swallalahu alayhi wasalam
Swahaba mmoja alisema kuwa: «Nilimuona Mtume wa Allah, Allah amfikishie rehma na amani, akiwa amesimama Hazura (mtaa kati mitaa ya mji wa Makka) huku akiwa amepanda mnyama wake akisema: Nina’apa kwa Allah kwamba wewe (Makka) ndio ardhi bora zaidi na ni ardhi ya Allah inayopendwa zaidi na Allah. Na kama sio kwamba nimefukuzwa humu, nisinge ondoka». (Tirmidhi, Hadithi Na. 3925, Nasai, Hadithi Na. 4252) .
  1. Allah amefaradhisha kuhiji nyumba yake Tukufu kwa mwenye uwezo wa kufika huko
Nabii Ibrahimu aliwatangazia watu kwenda kuhiji, watu wakamiminika kutoka kila kona. Manabii, Allah awafikishie rehema na amani, pia wamehiji katika mji huo, kama Mtume,swallalahu alayhi wasalam, alivyolieleza hilo. Allah akielezea habari ya yeye kumuamrisha Ibrahimu amesema kuwa: «Na watangazie watu Hija, watakuja wakitembea kwa miguu na wengine juu ya wanyama waliokonda wakitokea kila kona ya dunia iliyo mbali». (Sura Alhajj, aya 270) 

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU