Ukristo ni nini? Utatoa maelezo kuhusu Ukristo uliotajwa ndani ya Quran?

Ukristo ni dini ambayo kiasili imetegemea ufunuo, yenye kitabu kitukufu na ambayo kiasili ni dini ya kumwamini Mungu mmoja; hata hivyo, iligeuzwa kuwa imani ya utatu hapo baadaye. Kuna dhana ya kidini kama mitume, malaika, ahera na qadar (majaaliwa) katika dini hii lakini hayafahamiki na kufafanuliwa kwa namna sawa kama ilivyo katika Uisilamu.

Kwa uhakika, Ukristo ni dini inayoegemea kwenye imani ya Mungu mmoja. Yapo maelezo yenye kutilia mkazo ukweli huu katika Biblia na vyanzo vyengine. Kumpwekesha Allah kumetajwa (Yohana.V / 44). Hata hivyo, baadhi ya ibara na maelezo ya kuunda katika maandishi hayo hayo yamesababisha kuibuka kwa imani ya utatu. Baadhi ya waandishi wa Biblia na muda kati ya Yesu na muda wa kuandikwa Biblia una mchango mkubwa katika ufahamu huu. Kwa upande mwengine, utatu hauelezewi waziwazi popote pale katika kitabu kitakatifu cha Ukristo. Hata hivyo, baadhi ya maelezo kama “mimi na Baba ni kitu kimoja”, roho ya baba yako”, “roho ya Mungu” kumepelekea kwa baadhi ya tafsiri zinazomzingatia Yesu na roho mtakatifu kuwa ni Mungu pamoja na Mungu.
Mtu wa mwanzo kuanzisha tafsiri hizi alikuwa ni Paul, ndiye aliyeunganisha wanafunzi baadaye. Paul, anaetambulika kuwa ni “mwanathiolojia mkubwa wakati wa zama za Yesu Isa”, anajulikanwa kuwa ndio mwasisi wa Ukristo leo. Kwa mujibu wa wanazuoni wa kisasa, Ukristo wa leo unajumuisha ufasiri wa Paul kuliko mfumo uliotambulishwa na Yesu. Hata pia inaweza kusemwa kuwa karne zilizofuata zimetegemea imani yao ya kidini kwa tafsiri ya Paul kuliko Biblia. Mapendekezo ya Paul yamelenga kwenye Yesu Masiya kuliko Mungu. Kwa mujibu wake, Yesu hakuwa ni mtu tu bali pia alifufuliwa kwa uwezo wa Mungu.
Kama inavyoonekana, Ukristo wa leo umeegemea kwenye tafsiri ya Paul. Mifumo yote miwili ya dini hii ya asili na Biblia, kitabu chao kitakatifu, kimegeuzwageuzwa. Ukristo ni dini iliyogeuzwageuzwa. Hata hivyo, Ukristo uliogeuzwageuzwa na Wakristo wanaoishi leo na ukristo uliotajwa ndani ya Quran ni tofauti kabisa.
Katika Quran, neno “Nasrani” linatumiwa kwa Mkristo na neno “Nasara” kwa Wakristo. . (Aal-i Imran, 3/67; al-Baqara, 2/62, 111, 113, 135, 140; al-Maida, 5/14, 18, 51, 69, 82; at-Tawba, 9/30; al-Hajj, 22/17). Wakristo pia wametajwa na aya zilizokuwemo ibara “Ahl al-Kitab” (Watu wa Kitabu) kama aya ifuatayo:
“Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote.” (Aal-i Imran, 3/64)
Kwa mujibu wa Quran, kama vile Wayahudi, Wakristo hawakutimiza ahadi yao; kwa hivyo, uadui na kinyongo vitawatawala hadi Siku ya Kiama. Bwana Muhammad (s.a.w.) ni mjumbe aliyetumwa kwao, pia. Aliwafafanulia mambo mengi yaliyofichwa na Watu wa Kitabu. Hata hivyo, Wayahudi na Wakristo walisema wao walikuwa ni “watoto wa Allah na vipenzi vyake”; hivyo, walimpinga Bwana Muhammad (s.a.w.). Wayahudi walimzingatia Uzayr na Wakristo walimzingatia Yesu kuwa ni mwana wa Mungu. Wamekuwa ni makafiri tokea walipomfanya binadamu kuwa ni mungu. (al-Maida, 5/12-18; at-Tawba, 9/20) Walitenda kinyume na asili ya dini ya upwekeshaji kwa kuwasifia watoto kuwa ni Mungu. Hata hivyo, yafuatayo yanaelezwa katika Quran:
Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anaye fanana naye hata mmoja.” (al-Ikhlas, 112/1-4).
Quran inaeleza kuwa Yesu ni mja wa Allah na mjumbe na kwamba anafikisha ujumbe wa kumpwekesha Allah. (al-Maida, 5/46-47, 62-69, 72-77). Kwa hali hiyo, Wakristo waliomfanya Yesu kuwa ni mungu wanasema, “Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa Utatu.” (al-Maida, 5/73); hivyo, wameikengeuka njia ya kweli na kwenda nje ya mstari wa upwekeshaji. Allah anawaita Wakristo walio nje ya kanuni ya upwekeshaji kuja kwenye uasili wa dini, kuja kumpwekesha Allah na kwenye njia ya Uisilamu. (al-Maida 5/46).

Kama inavyoelezwa hapo juu, Ukristo asili yake ni dini ya kweli. Mtume wake ni Yesu na kitabu chake ni Biblia. Yesu, aliyeunda nukta ya mazingatio ya Ukristo wa leo na misingi ya thiolojia ya Paul, ni mja wa Allah na mjumbe wake. Yesu yeye mwenyewe anaeleza hayo kama ifuatavyo:
(Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai, Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu. Na amani iko juu yangu siku niliyozaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai.” (Maryam, 19/30-33).
Isitoshe, Wakristo waliomfanya Yesu na mama yake kuwa ni mungu, wanaounda imani ya utatu watakumbana na Yesu Siku ya Kiama; hivyo, uongo uliosemwa na Wakristo utafunuliwa mara moja. Suala hili linaelezwa katika Quran kama ifuatavyo:
Na pale Mwenyezi Mungu atakapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu? (Na Isa) atasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hainifalii mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema basi bila ya shaka umekwisha yajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye Mjuzi mkubwa wa yaliyo fichikana. Sikuwaambia lolote ila uliyo niamrisha, nayo ni: Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Na mimi nilikuwa shahidi juu yao nilipokuwa nao. Na ulipo nifisha ukawa Wewe ni shahidi juu ya kila kitu.” (al-Maida, 5/116, 117).
Ukristo katika zama za Mtume (s.a.w.) ulikuwa ushageuzwageuzwa kama ulivyo Ukristo wa leo.

Kisha, Ukristo wa leo sio sawa na Ukristo uliofikishwa na Yesu. Wao wenyewe walitunga sentensi kama vile “Na Wakristo wanasema Masihi ni mwana wa Mungu.” (at-Tawba, 9/30) na “Wamewafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni marabi badala ya Mwenyezi Mungu, na pia Masihi bin Maryamu.” (at-Tawba, 9/31).
Vivyo hivyo, Ukristo wa leo hauna uhusiano na Biblia iliyoletwa na Yesu. (al-Maida, 5/68) Kwa kuwa, kama vile wanazuoni wa Kiyahudi, mapadri wa Kikristo walibadilisha maamrisho ya Kitabu walichoteremshiwa na Allah kwa sababu ya manufaa ya kupata kitu. (at-Tawba, 9/34)
Maswali juuyau islamu

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU