SWALA YA MSAFIRI NA MGONJWA
- Ni sunna kwa msafiri, katika hali ya kusafiri kwake au kukaa kwake kwa muda ambao haupungui siku nne, kupunguza swala zenye rakaa nne na kuziswali rakaa mbilimbili. Ataswali swala ya Adhuhuri, Alasiri na Ishaa rakaa mbili badala ya rakaa nne, isipokuwa tu kama atasali nyuma ya imamu mkazi. Atalazimika kumfuata katika swala yake na kuswali rakaa nne kama imamu..
- Sheria inamtaka kuacha swala za sunna zinazofungamana na faradhi isipokuwa tu sunna ya kabla ya swala ya Alfajiri.
- Inafaa kwake kukusanya kati ya swala ya Adhuhuri na Alasiri, na kati ya Magharibi na Ishaa, na kuzisali katika wakati wa swala mojawapo, hasa hasa iwapo litafanyika hilo wakati wa safari ili kumpunguzia uzito, kumhurumia na kumuondoshea uzito.

Allah ametuamrisha kuijali swala katika hali zetu zote.
Swala ya mgonjwa
Swala ni lazima kwa kila Muislamu katika hali zote madamu ana akili yake timamu na utambuzi wake. Lakini Uislamu umezingatia tofauti za hali za watu na mahitaji yao, na miongoni mwake ni mgonjwa.
Ili kubainisha hilo tunasema:
- Mgonjwa ambaye hawezi kusimama au ikiwa kusimama anapata uzito au kutamcheleweshea kupona, basi atasamehewa kusimama na atasali akiwa amekaa. Akishindwa kukaa ataswali akiwa amelala ubavu. Mtume,swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Swali ukiwa umesimama. Ukishindwa, swali ukiwa umekaa. Ukishindwa, swali ukiwa umelala ubavu». (Bukhari, Hadithi na. 1066)
- Mwenye kushindwa kurukuu au kusujudu, ataashiria kiasi awezacho.
- Mtu ambaye kukaa ardhini kutamuia uzito atakaa kwenye kiti na mfano wake.
- Mtu ambaye kujitwaharisha kwa kila swala kutamuia uzito kwa sababu ya maradhi yake, inafaa kwake kukusanya kati ya swala ya Adhuhuri na Alasiri, na kati ya swala ya Magharibi na Ishaa.
- Mtu ambaye inakuwa uzito kwake kutumia maji kwa sababu ya maradhi, inafaa kwake kutayamamu ili kuekeleza swala.

Comments
Post a Comment