SHURUTI ZA SWALA

  1. Kutwaharika na hadathi na najisi: Umeshatangulia kuelezwa ufafanuzi wa hadathi na najisi (Tazama uk. 93).
  1. Kusitiri uchi:
Inashartiwa kusitiri uchi kwa nguo isiyo onesha mchanganuo wa maungo kwa sababu ya ufupi wake au wepesi wake unao onesha vilivyo ndani.
Na uchi wa mwanamume ni kutoka kwenye kitovu mpaka kwenye goti. Na uchi wa mwanamke katika swala ni mwili wake wote isipokuwa uso wake na viganja vyake
Allah amesema kuwa: «Enyi wanadamu, jipambeni kwenye kila msikiti». (Sura Al-aaraaf, aya 31). Kusitiri uchi ndio kiwango cha chini cha kujipamba. Maana ya «kila msikiti» ni kila swala.
  1.  Kuelekea qibla:
Allah Mtukufu amesema kuwa: «Na kutokea popote ulipotoka, elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtukufu». (Sura Albaqara, aya 149).
  • Qibla cha Waislamu na Alkaaba Tukufu ambayo ameijenga baba wa Mitume Ibrahim, Allah amfikishie amani, na Mitume, Allah awafikishie amani, wamehiji hapo. Sisi tunajua kwamba Alkaaba hiyo ni mawe yasiyodhuru wala kunufaisha, lakini Allah ametuamrisha kuelekea kwenye Qibla hicho katika kuswali ili Waislamu wote wawe wamoja katika kuelekea sehemu moja. Sisi tunamuabudu Allah kwa huku kuelekea.
  • Lililo wajibu kwa Muislamu ni kuelekea Alkaaba ikiwa anaiona mbele yake. Ama mtu ambaye yuko mbali, inamtosha kuelekea upande wa Makka kwa kukisia. Ukoseaji kidogo katika kuelekea haudhuru, kama Mtume,swallalahu alayhi wasalam, alivyosema kuwa: «Sehemu iliyopo kati ya mashariki na magharibi ni Kibla». (Tirmidhiy, Hadithi Na. 342).
  • Akishindwa kuelekea Kibla kwa sababu ya ugonjwa au jambo jingine, wajibu unaondoka, kama yanavyo ondoka mambo yote ya wajibu kwa kushindwa kuyafanya. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mcheni Allah kadiri muezavyo». (Sura Attaghaabun, aya 16).
  1. Kuingia kwa wakati wa swala:
Hilo ni sharti la swala kuwa sahihi. Swala haisihi kabla ya kuingia wakati wake, na ni haramu kuiahirisha na kuiswali nje ya wakati wake. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Kwa yakini, swala kwa waumini ni jambo la lazima, lililowekewa wakati maalum». (Sura Annisaa, aya 103).
Katika kuingia kwa wakati, inatakiwa kusisitiza mambo yafuatayo:
  • Jambo bora zaidi kuswali mwanzo wa wakati.
  • Ni wajibu kuitekeleza swala katika wakati wake, na ni haramu kuiahirisha kwa sababu yoyote ile (Tazama uk. 106).
  • Mtu ambaye swala imempita kwa sababu ya kulala au kusahau ni wajibu kwake kufanya haraka kuitekeleza mara atakapoikumbuka.

Shuruti za swala:

Kutwaharika na hadathi na najisi
Kusitiri uchi
Kuelekea qibla
Kuingia kwa wakati wa swala

Swala ni wajibu kwa nani?

Swala ni wajibu kwa kila Muislamu, mwenye akili timamu, baleghe, asiyekuwa katika Hedhi na asiyekuwa katika Nifasi. Mwanamke hatakiwi kuswali wakati wa Hedhi yake au wakati wa Nifasi yake. Pia hatalipa swala baada ya kutwaharika kwake na damu kukatika (Tazama uk. 96).

Mtu anahukumiwa kuwa amebaleghe wakati wa kupatikana kwa mojawapo ya alama zifuatazo:

  1. Kufikia umri wa miaka kumi na tano
  2. Kuota kwa nywele ngumu katika sehemu za siri za mbele au za nyuma.
  3. Kushusha Manii usingizini au wakati wa kuwa macho
  4. Mwanamke kuingia katika Hedhi au kubeba mimba.

Swala tano za faradhi na nyakati zake

Allah amefaradhisha kwa Muislamu swala tano katika siku moja. Swala hizo ndio nguzo kuu ya dini yake, na ni faradhi zilizosisitizwa sana kwake. Pia Allah ameziwekea nyakati za wazi kama ifuatavyo:
Swala ya Alfajiri: Ni rakaa mbili. Wakati wake unaanza tangu kuchomoza kwa alfajiri ambayo ni mwanzo wa mwangaza ulioko angani kwa upande wa mashariki. Unakwisha kwa jua kuchomoza. 
Swala ya Adhuhuri: Ni rakaa nne. Wakati wake unaanza tangu jua kupinduka kwa jua kuelekea upande wa magharibi baada ya kuwa katikati angani -. Wakati wake unakwisha pale ambapo kivuli cha kila kitu kinakuwa sawasawa na urefu wake. 
Swala ya Alassiri: Ni rakaa nne. Wakati wake unaanza tangu kutoka kwa wakati wa Adhuhuri pale kivuli cha kila kitu kinapokuwa mfano wake. Unakwisha kwa kuzama kwa jua. Inatakikana kwa Muislamu kufanya haraka kuswali kabla miale ya jua haijakuwa dhaifu na rangi yake kuwa ya manjano. 
Swala ya Magharibi: Ni rakaa tatu. Wakati wake unaanza tangu jua linapozama na kupotea sahani yake (duara lake) angani. Unakwisha kwa kupotea kwa mawingu mekundu ambayo yanatokea baada ya jua kuzama. 
Swala ya Isha: Ni rakaa nne. Wakati wake unaanza kuanzia kupotea kwa mawingu mekundu, na unamalizika katikati ya usiku. Inawezekana kuisali wakati wa dharura mpaka kuchomoza kwa Alfajiri.  

Sehemu ya kuswalia

Uislamu umeamrisha kuiteleza swala katika kundi (jamaa), na umependekeza kuwa hilo lifanyike katika msikiti ili liwe baraza na mjumuiko wa Waislamu, na kwa sababu hiyo, izidi kuimarika misingi ya udugu na upendo baina yao. Uislamu umelifanya hilo kuwa jambo bora zaidi kuliko mtu kuswali peke yake kwa daraja nyingi, kama Mtume,swallalahu alayhi wasalam, alivyosema kuwa: «Swala ya mtu katika kundi inaizidi swala ya mtu peke yake kwa daraja ishirini na saba». (Bukhariy, Hadithi Na. 619. Muslim, Hadithi Na. 650. Ahmad, Hadithi Na. 5921).
Lakini swala inasihi mahali popote, na hii ni miongoni mwa rehema za Allah kwetu, kama Mtume,swallalahu alayhi wasalam, alivyosema kuwa: «Na ardhi imefanywa kwangu msikiti na yenye kutoharisha Kwa hiyo, mtu yeyote katika uma wangu ikimkuta swala, basi aswali». (Bukhariy, Hadithi Na. 328. Muslim, Hadithi Na. 521).
«Ardhi imefanywa kwangu msikiti na kitwaharisho. Kwa hiyo, mtu yeyote katika umma wangu ikimkuta swala (mahali popote) basi asali».

Masharti ya sehemu ya kuswalia:

Uislamu umepawekea masharti sehemu ya kuswalia iwe tohara(safi). Allah Mtukufu amesema kuwa: «Na tulimuamrisha Ibrahim na Ismail kwamba itwaharisheni nyumba yangu kwa ajili ya wanaotufu na wanaokaa itikafu na wanaorukuu, wanaosujudu». (Sura Albaqara, aya 125). Msingi ni Twahara, na Najisi ni kitu cha kutoka. Kwa sababu hiyo, madamu hujajua kuwepo kwa Najisi, basi wewe hukumu kwamba ni Twahara. Inafaa kuswali juu ya kila sakafu twahara, na haitakiwi kujilazimisha kuweka mswala au kitambaa ikawa hapasaliwi ila tu juu ya vitu hivyo.
Kuna idadi kadhaa ya masharti mengine ya jumla ambayo ni wajibu kwa mwenye kuswali kayazingatia. Miongoni mwa masharti hayo ni haya:
  1. Kutowakera watu katika mahali mtu anaposwali, kama vile mtu anayeswali katika njia ambazo watu wanapita na katika sehemu ambazo inakatazwa kusimama, jambo ambalo linasababisha usumbufu na msongamano wa watu. Mtume wa Allah,swallalahu alayhi wasalam, amekataza kuudhi na kudhuru. Amesema kuwa: «Hakuna kudhuru na hakuna kudhuriana» (Ibnimaaja, Hadithi Na. 2340. Ahmad, Hadithi Na. 2865).
  2. Kisiwepo kitu kinachomshughulisha mwenye kuswali, kama picha au sauti za juu na mziki.
  3. Isiwe sehemu hiyo imeandaliwa kimsingi kwa ajili ya kumuasi Allah, kama sehemu za kucheza mziki na ngoma na vilabu vya usiku. Ni makuruhu kuswali katika sehemu hizo.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU