POMBE NA VILEO

POMBE NA VILEO

Pombe na kilevi ni kila kitu kinacho ivuruga akili na kuisumbua au kuifunika na kuaiathiri, kama alivyosema Mtume,swallalahu alayhi wasalam, kwamba: «Kila kinacholevya ni pombe na kila pombe ni haramu».(Muslim, Hadithi Na. 2003) Ni sawa kilevi kiwe kimetengenezwa kutokana na matunda kama vile zabibu au tende au tini, au kimetengenezwa kutokana na nafaka kama vile ngano au mahindi au mpunga, au kimetengenezwa kutokana na vitu vitamu kama vile asali. Kila kinacho ivuruga akili ni pombe, ni haramu kwa jina lolote au kwa mtindo wowote, hata kama itakuwa imeeongezwa kwenye juisi ya kawaida au pudini au chocoleti.

Hukumu ya pombe

Pombe ni katika madhambi makubwa sana, na uharamu wake umethibiti na kusisitizwa kwa ukali katika Qur`ani na Sunna, kama ifuatavyo:
  • Amesema Allah kuwa: «Enyi waumini, hakuna vingine isipokuwa kwamba pombe na kamari na masanamu na kupiga ramli ni Najisi katika vitendo vya shetani. Jiupusheni navyo ili mpate kufaulu.».(Almaaida, aya 90).Allah ameipa wasifu pombe kwamba ni najisi, ni katika matendo ya shetani na akatuamuru kujiepusha nayo ikiwa   tunataka kufuzu na kufanikiwa.
  • Amesema Mtume,swallalahu alayhi wasalam, kwamba: «Kila kinacholevya ni pombe, na kila kinacholevya ni haramu. Na atakaye kunywa pombe duniani akafa hali akiwa anaendelea kulewa, hatokunywa pombe Akhera».(Muslim, Hadithi Na. 2003)
  • Mtume,swallalahu alayhi wasalam, katika kuilezea pombe namna inavyopingana na imani, amesema kwamba: «Na mtu hanywi pombe wakati anapokunywa na akabaki kuwa muumini».(Bukhariy, Hadithi Na. 5256. Muslim, Hadithi Na. 57)
  • Uislamu umewajibisha adhabu kwa mwenye kunywa pombe. Heshima yake inashuka na uadilifu wake  katika jamii unaondoka.
  • Uislamu umemuahidi mwenye kubobea katika kunywa pombe na mfano wa pombe mpaka akafa na hakutubu kwamba atapata adhabu kali. Mtume,swallalahu alayhi wasalam, anasema kwamba: «Kwa yakini kabisa, Allah amebeba ahadi kwa mtu anayetumia kilevi kwamba atamnywesha kinywaji cha uchafu wa watu wa motoni».(Muslim, 2002)
  • Kila mwenye kushiriki au kusaidia katika unywaji wa pombe kwa namna moja au nyingine ataingia katika ahadi hii ifuatayo: «Mtume wa Allah amewalaani watu kumi kuhusiana na pombe: Mtengenezaji na anaye tengenezewa na mnywaji wake na anayebeba na anayepelekewa, mhudumu wake, muuzaji wake, mlaji wa thamani yake, anayenunulia watu pombe na anayenunuliwa pombe».(Tirmidhiy, Hadithi Na. 1295)

Kuilinda akili

Dini hii tukufu imekuja ili kufanikisha mambo yenye manufaa kwa binadamu katika dunia yao na Akhera yao. Ya juu kabisa katika hayo ni kulinda mambo matano ya msingi: Dini, roho, akili, mali na kizazi.
Akili ndio mahali ambapo sheria inalenga, na ndio kiini ambacho Allah kumteua na kumpa heshima mwanadamu kwacho. Kwa sababu hiyo, ndio maana sheria imeilinda akili na kuihami dhidi ya kila jambo linaloweza kuidhoofisha au kuipoteza.

Dawa za kulevya

Kutumia dawa za kulevya hata kama asili yake ni mimea au za kutengeneza, na sawa zinatumiwa kwa kuvuta au kumeza kudunga sindano ni miongoni mwa madhambi na maasi makubwa sana. Pamoja na kuwa dawa za kulevya zinaivuruga akili, pia zinauteketeza mfumo mzima wa mishipa ya fahamu ya mwanadamu. Pia zinamsababishia mtumiaji kupata aina mbali mbali za magonjwa ya akili na ya kisaikolojia, na wakati mwingine zinaweza kumsababishia kifo chake. Allah ambaye ni mwenye huruma kwa waja wake anasema kuwa: «Na msijiue. Hakika, Allah ni mwenye huruma kwenu».(Annisaa, aya 29)
Kila kitu ambacho imethibiti kuwa kina madhara ya kiafya ni haramu katika sheria..

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU