NYIRADI KUBWA ZAIDI:

NYIRADI KUBWA ZAIDI:

Hizi ni sura tatu fupi katika sura kubwa sana za Qur’ani
  1. Sura Ikhlas.
Hii ni mojawapo ya sura kubwa sana za Qur’ani na ni sawa na theluthi ya Qur’ani kama alivyosema Mtume. (Bukhariy 6267, Muslim 811) 
«Qul Huwallahu Ahad. Allahusw-swamad. Lam Yalid Walam Yuulad. Walam Yakun Lahuu Kufuwan Ahad»
«Qul Huwallahu Ahad»
Hii ni amri ya Allah ya kumtaka Mtume Mtukufu kusema kwamba: Allah ni mmoja, asiyekuwa na mshirika katika kuabudiwa.
«Allahusw-swamad»
Allah ndiye ambaye viumbe vyote vinaelekea kwake na kumtegemea yeye katika kutafuta mahitaji yao.
«Lam Yalid Walam Yuulad»
Ametakasika kwa kutokuwa na mtoto na kwakuwa hakuzaliwa. Yeye ni wa mwanzo ambaye hakuna kitu kabla yake.
«Walam Yakun Lahuu Kufuwan Ahad»
Hana wa kufanana naye au kushabihiana naye katika dhati yake na sifa zake, kwa sababu yeye ni muumba na visivyokuwa yeye ni viumbe.
  1. Sura Alfalaq 
«Qul Auudhu Birabbil Falaq. Minsharri Maakhalaq. Waminsharri Ghaasiqin Idhaa Waqab. Waminshariin-naffaathaati Fil-uqad. Waminsharri Haasidin Idhaa Hasad».
«Qul Auudhu Birabbil Falaq»
 Sema, ewe Mtume, kwamba: Ninaomba kinga na ninaomba hifadhi kwa Mola wa asubuhi.
«Minsharri Maakhalaq»
Anilinde dhidi ya shari ya viumbe vyote na madhara yao.
«Waminsharri Ghaasiqin Idhaa Waqab»
Na dhidi ya shari ya usiku wenye giza nene unapoingia na kuvinjari. Pia dhidi ya shari na vinavyodhuru ndani ya usiku huo.
«Waminshariin-naffaathaati Fil-uqad»
 [wa min charri’nafassatti fil ‘ouqad]
Na dhidi ya shari ya wanawake wachawi ambao wanatabana katika mafundo wanayoyafunga kwa lengo la kuroga.
«Waminsharri Haasidin Idhaa Hasad»
Na dhidi ya shari ya hasidi mwenye kuchukia watu anapowafanyia husda kwa sababu ya neema ambazo Allah amewapa na kutaka ziwaondoke na kuwafanyia madhara.
  1. Sura Annaas:
«Qul Auudhu Birab-binnaas. Malikin-naas. Ilaahin-naas. Minsharril Was-waasil Khan-naas. Alladhii Yuwas-wisu Fii Suduurin-naas. Minal Jinnati Wan-naas»
«Qul Auudhu Birab-binnaas»
Sema, ewe Mtume, kwamba: Ninaomba kinga na ninaomba hifadhi kwa Mola wa  watu ambaye pekee ndiye mwenye uwezo wa kuzuia shari ya wasiwasi.
«Malikin-naas»
Mfalme wa watu, mwenye uwezo wa kufanya katika mambo yao yote, asiye wahitaji.
«Ilaahin-naas»
Mola wa watu ambaye hakuna mwenye haki ya kuabudiwa kwa haki ila yeye tu.
«Minsharril Was-waasil Khan-naas»
Anilinde dhidi ya madhara ya shetani ambaye anatia wasiwasi wakati wa kughafilika na anajificha wakati wa kumtaja Allah.
«Alladhii Yuwas-wisu Fii Suduurin-naas»
Ambaye anasambaza shari na shaka katika nyoyo za watu.
«Minal Jinnati Wan-naas»
Ni mashetani wa kijini na kibinadamu. 

Wakati wa kusoma sura za kinga:

Sheria inataka sura za kinga zisomwe kila asubuhi na jioni. Imenukuliwa katika Hadithi kwamba: «Soma (Qul Huwallahu Ahad) na (Qul Auudhu Birabbil Falaq na Qul Auudhu Birabbin-naas) wakati wa asubuhi na wakati wa jioni mara tatu, zitakutosha kwa kukukinga dhidi ya kila kitu». (Tirmidhiy 3575)
Na kila baada ya swala ya faradhi, kama Mtume alivyomfundisha Swahaba mmoja. (Abudaudi 1523)
Na kabla ya kulala. Mtume alipokuwa akipanda kitandani kwake kila usiku alikuwa akiviweka pamoja viganja vyake halafu anatabana humo na kusoma (Qul Huwallahu Ahad) na (Qul Auudhu Birabbil Falaq) na (Qul Auudhu Birabbin-naas), halafu anajipangusa kwa kutumia viganja hivyo sehemu awezazo katika mwili wake akianza kichwa chake na uso wake na sehemu ya mbele ya mwili wake. Anafanya hivyo mara tatu». (Bukhariy 4729)
Sura hizo ni kinga kubwa sana inayomkinga mwanadamu dhidi ya uchawi na uovu. «Mtume alikuwa akiomba kinga dhidi ya majini na macho ya watu mpaka ziliposhuka sura za kinga. Alizitumia sura hizo na kuacha nyinginezo». (Tirmidhiy 2058)

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU