NYAKATI AMBAZO IMEKATAZWA KUSWALI SWALA ZA SUNNA

Wakati wowote inafaa kwa Muislamu kuswali swala yeyote ya sunna isipokuwa nyakati ambazo Uislamu umekataza kuswali katika nyakati hizo, kwa sababu ni nyakati za ibada za  makafiri. Haitakiwi kuswali katika nyakati hizo isipokuwa tu kulipa faradhi zilizompita au swala za sunna ambazo zina sababu maalumu kama vile swala ya maamkizi ya msikiti. Katazo hili ni la swala. Ama kumtaja Allah na kumuomba hilo linaruhusiwa muda na wakati wowote.
Nyakati ambazo imekatazwa kuswali ni kama ifuatavyo:
  1. Baada ya swala ya Alfajiri mpaka jua kuchomoza na kunyanyuka kidogo angani kiasi ambacho katika sheria kimeainishwa kwamba ni kiasi cha mkuki. Katika nchi zilio tambarare unyanyukaji huu wa jua unapatikana kwa karibu dakika 20 baada ya kuchomoza.
  2. Jua linapokuwa limesimama sawasawa mpaka litakapo kengeuka. Huo ni muda mfupi kuelekea kuingia kwa wakati wa swala ya Adhuhuri.
  3. Baada ya swala ya Alasiri mpaka jua lizame.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

Kisa Cha Nabii Ibraahiym عليه السلام - Sehemu Ya 1