Nini maana ya utumwa (kunyenyekea) kwenye Uislamu? Ni nini maana ya kumuabudu Allah?

Dear Brother / Sister,
Utumwa ni kitendo cha kutengeneza uhusiano baina ya mwanadamu na Muumba, Allah. Hivyo basi, ukweli kwamba Allah ndie Muumbaji na mwanadamu ameumbwa unasisitizwa kwenye aya za mwanzo kabisa kama zilivyoshushwa:
“Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba. Amemuumba binaadamu kwa tone la damu” (al-Alaq, 96/1-2).
Qur’an inavuta hisia za umakini kuhusu uhusiano huu mwanzo mwa aya inayomtaka mwanadamu kuabudu:
“Enyi watu! Muabuduni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni nyinyi na wale wa kabla yenu, ili mpate kuokoka.” (al-Baqara, 2/21).  
Inafahamika kuwa kutoka kwenye aya ya hapo juu kwamba kuabudu ni jukumu la kiuumbaji la asili ya mwanadamu, ni kupeleka shukrani kwa Muumba, na ni tendo tukufu linalopelekea kutambua lengo la kiroho na kimwili.
Sasa tutawasilisha ukweli wa kunyenyekea, ambao tumejaribu kuonesha katika baadhi ya mambo:
Kunyenyekea hufanywa kwa njia mbili: Ya kwanza ni unyenyekevu unaofanywa bila kuzingatia kuonekana kwa Muumbaji na kutokuzungumza na Yeye.; na wa pili ni unyenyekevu wa kumuelekea Yeye.
1. Unyenyekevu unaofanywa bila kuzingatia kuonekana kwa Muumbaji unaweza kufupishwa kama ifuatavyo:
a. Utumwa (Servitude): Kuthibitisha ukubwa wa Allah kusifia ufundi wake kwa kuangalia utendaji usiokifani wa Muumba unaoonekana ulimwengu mzima kama vile kutengeneza, kudhibiti, kupanga na kusanifu. 
b. Utumwa (Servitude): Kuangalia uzuri wa usanifu unaoakisi majina mazuri ya Mungu, kuyazungumzia, na kila mmoja kumuonesha mwenzake ili kupata mazingatio kupitia majina hayo.
c. Utumwa (Servitude): Kutathmini lengo la uzuri wa majina ya Allah, ambayo yana faida za kiroho, pamoja  na kiakili na kuyasifu toka moyoni.
d. Utumwa (Servitude): Kupokea, kufikiri na kutafakari kurasa za ulimwengu kama kitabu kilichoandikwa na kalamu ya nguvu na hekima ya Allah.
e. Utumwa (Servitude): Kuangalia Sanaa ya hali ya juu, darizi nzuri na maumbo yaliyopambwa yanayoonekana pembe zote za dunia, kuangalia uzuri wa kiroho na ukamilifu wa Muumbaji na kumjua kwa ukaribu mno, ili kumpenda na kumuheshimu.
2. Unyenyekevu mbele ya Allah na kuzungumza nae unaweza kufupishwa kama ifuatavyo: The servitude in the presence of the Creator addressing Him can be summarized as follows:
a. Utumwa (Servitude): Kujua kwamba mwanadamu siku zote yupo mbele ya Allah na kutenda ipasavyo. Kumfikia mtendaji kupitia matendo na kumfikia msanii kupitia Sanaa.
b. Utumwa (Servitude): Kufahamu kwamba Muumbaji anataka ajulikane kwa kuonesha Usanii wa hali ya juu na wa kimaajabu; na kujibu jambo hili kupitia Imani.
c. Utumwa (Servitude): Kufahamu kwamba Allah, ni mwingi wa huruma, anataka  kupendwa kwani huonesha matunda ya huruma yake   kama akisi/picha ya huruma yake isiyo na ukomo kwa kukamilisha hitaji hili la Allah; mwanadamu kuuweka upendo wake kwa Allah na kujaribu kujipendekeza ili apandwe na Yeye kupitia kumuabudu Allah.
d. Utumwa (Servitude): Kufahamu kwamba Allah, ambae ni Mkarimu, huwapa watu neema zisizo na ukomo za kimwili na za kiroho pamoja na kuvielekeza viungo vya hisia vya kimwili na vya kiroho vya watu, anataka avipe raha viwiliwili na akili; na hivyo basi, kupeleka sifa na shukran zake kwa Allah kupitia vitendo, maneno na fikra kwa kadri awezavyo.
e. Utumwa (Servitude): Kusema Subhanallah, Alhamdulillah, Allahuakbar”  (Ametukuka Allah, Shukran zote zinamstahikia Allah, Allah ni mkubwa) kwa ajili ya kumtukuza Allah juu ya utukufu wake (majesty) na uzuri wake (beauty), ambapo mfano wake unaonekana kila mahala kuanzia chembe ndogo ndogo (atoms) hadi maumbo makubwa (galaxies); kusimama, kurukuu na kusujudu mbele ya uwepo wake.
Kwa kuongezea, utumwa umegawika katika makundi mawili makubwa ambayo ni kuabudu na kuhudumia: funga, kuswali, kutekeleza nguzo ya Hijja, zaka ambapo zote hizi ni mifumo ya ibada; kuzalisha utaalamu wa aina zote wa kiteknolojia ambao unarahisisha maisha nayo pia huzingatiwa kama ibada. Kwa mfano, kutengeneza gari, kuunda meli, kutengeneza barabara na madaraja, kuanzisha viwanda ambavyo vitatoa bidhaa kadhaa za kiteknolojia vile vile nayo huzingatiwa kama ibada. Ni umuhimu usio na shaka kuazimia kupata radhi za Allah na kuwa mkweli hasa ikiwa mtu anataka ibada zake zikubaliwe.
Maswali juuyau islamu

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

Kisa Cha Nabii Ibraahiym عليه السلام - Sehemu Ya 1