Ni yapi madhara ya Kamari na kwanini imekatazwa (haram)?
Dear Brother / Sister,
Elmalılı Hamdi Yazır anaeleza yafuatayo kuhusu kukatazwa na madhara ya Kamari wakati akiitafsiri aya ya 219 katika Suratul-Baqara:
Jibu ni kama ifuatavyo: Kuna madhara na madhambi makubwa kwenye hayo. Kwa ujumla, yote mawili yanaharibu mazuri na huwaharibu watu. Kila moja linamuathiri mwenzake. Ulevi unaharibu akili; akili ni nguzo ya msaada kwa dini na dunia. Mtu anaweza kufanya mauaji kwasababu ya ulevi na kufanya maovu mengi kutokana na Kamari, ambayo haiwezekani kuyaorodhesha; yanaweza kufahamika kwa jina moja “madhambi makubwa”. Ingawa, yana manufaa machache kwa watu. Watu hupata furaha na ladha; wanapata pesa kwa kuuza pombe. Humpa ujasiri mtu muoga na kutia nguvu tabia ya mtu. Baadhi ya watu hupata bidhaa kwa Kamari. Ingawa, madhambi yake na madhara yake ni makubwa kuliko faida zake.
Lakini, faida zake si halisi na wala si madhubuti. Furaha wanayoipata husababisha akili kufunikwa. Ushujaa wa muda husababisha maafa. Tabia ya muda hudhuru afya;mazuri anayoyapata hayamnufaishi; faida ndogo inayopatikana huleta madhara mengi. Watakaoathirika hawawezi kuacha kirahisi. Kwa kufupisha, furaha na ladha zinaopatikana huwa ni za mtu binafsi na za muda mfupi ila matatizo na matokeo yake ni ya mtu binafsi na jamii; zinakuwa za kivitu na kimaadili. Husambaa kama maradhi ya kuambukiza. Wale ambao hawatoathirika mwanzoni wataathirika mwishoni. Si jambo lenye hoja za msingi kupendelea madhara halisi na ya jumla kwa kukumbatia manufaa ya kufikirika. Kuondosha madhara ndio njia ya kupendelea zaidi kuliko kupata faida. hivyo, huhitaji kuwa haramu kwa sababu za msingi. Aya inaelezea kwamba vyote kidini ni haramu kupitia ishara ambayo si ya moja kwa moja. Kama kungalikuwa hakuna aya zozote ndani ya Qur’ani zizonataja ulevi, aya hii tu ingetosha kuufanya kuwa haramu. Ingawa, katazo hili lisingekuwa katazo lililofahamika kutoka kwa maneno yanayojieleza yenyewe; wangetokea watu ambao wangalifikiri wanaweza kupunguza madhara ya pombe na kutumia faida zake kwa kutegemea ufahamu wa akili zao. Hivyo basi, baadhi ya Maswahaba walifikiri haikukatazwa kidini bali kifikra tu; baadae, aya ifuatayo iliifanya kuwa haramu kwa misingi ya kidini kwa uwazi na kwa njia ya moja kwa moja: “Ni uchafu … Basi jiepusheni navyo.” (al-Maida, 5/90).
Maswali juuyau islamu
Comments
Post a Comment