Ni nini riba na kwanini imekatazwa?

Dear Brother / Sister,
Hakuna mtu yoyote asiyejua kwamba riba imekatazwa katika Uislamu. Sababu kwanini riba imekatazwa kama agizo la Mungu iko wazi: Hairuhusiwi kwasababu Allah ameikataza. Kama ilivyo funga (swaumu) na kutoa zaka ni faradhi kwasababu ni “agizo la Mungu”, ni hivyo hivyo kwa riba imekatazwa kwa sababu hizo hizo. Na ndio sababu pekee kwanini tunaabudu. Kinyume na hayo, zipo baadhi ya sababu zingine kufuatiza agizo hilo la Mungu. Ni jambo la kawaida kwasababu, Aliekataza anajua vizuri tu ukweli wa uhalisia na tabia ya kila kitu na jinsi gani kila kitu kinatakiwa kuwa.
Kwa mfano, tunajua kufunga na kutoa zaka, ambapo tunatekeleza kwasababu Allah ametuagiza tufanye, kuna faida nyingi kwa mtu binafsi na jamii. Ingawa, hatujawahi kufunga ili tupoteze uzito au kutoa zaka ili kuweka sawa mgawanyo wa kipato kwenye jamii. Ukweli ni kwamba, mtu anaelipa kodi kama jukumu la kiraia hazingatiwi kwamba ametoa zaka; na mtu anaetafuta faida za kimwili kupitia swala ambapo hufanya mazoezi ya viungo hivyo basi hazingatiwi kwamba anatekeleza ibada ya swala. Ni hivyo hivyo, ikiwa ataanza ibada kwa lengo la kupata “faida” badala ya “kutekeleza amri”, mtu ambae hawezi kuona faida ingawa ameona ni agizo pia hana sababu zozote za kuendelea kuabudu.
Hata ivyo, faida inaweza kuwa chanzo cha mtu kuamini ambae anaabudu kwasababu ya agizo la Allah. Na kwa mtazamo huu, inaweza kusemwa kwamba faida ni muhimu kwasababu kila agizo linazo faida, ingawa si muhimu, baadhi ya faida na sababu mahsusi. Hivyo basi, tunafunga kwasababu Allah ametuamrisha kufanya hivyo na funga [swaum] ina baadhi ya faida. Ni sawa, riba imekatazwa kwasababu Allah ameikataza. Tukifikiria kwamba kila agizo Allah analotupa ni “njia ya kutujenga kinidhamu” kwa mujibu wa maelezo tuliyokwisha kuyatoa, tunaweza kurudi kwenye swali letu:
Kwanini riba inakatazwa?
Jibu letu lipo tayari: Inakatazwa kwasababu Allah kaikataza. Ikiwa tutaendelea kwa jibu hili, uwajibikaji kwetu kwa Allah kutaathiriwa ikiwa hatutotii katazo la riba. Hii ni kusema kwamba; uwajibikaji wetu kwa Allah utapungua thamani.Ikiwa moja katika ya umoja baina ya Mja-na-Mola wake ukipungua, moja huongezeka. Ikiwa mtu ataacha kumtumikia Allah, fikra ya kujiona Mungu itachukua nafasi yake (bila kujitambua, hujipa fikra za kiungu mwenyewe). Wakati fikra za kujiona Mungu zikitoweka, utambuzi wa dhati wa kumtumikia Allah huchukua nafasi yake. Ni Dhahiri kwamba kuepuka kutoa au kupokea riba ni matakwa ya kumtumikia Allah. Hivyo hivyo, inaweza kusemwa kwamba kutokutii agizo hili inahusisha kudai kuwa Mungu. Tunaweza kulielewa hili kupitia neno “amri”, ambayo, hujikita kwenye dhana ya “kutii-kutokutii.” Kwasababu hii, riba imekatazwa kwenye Uislamu. Ingawa, inawezekana sisi tukaona kwanini, vile vile inakatazwa kwa misingi ya “imani” sambamba na misingi ya “Uislamu” hasa tunapobainisha hekima nyuma ya katazo hili. Kwa mantiki hii, tukumbuke basi kwamba riba ni kama mfumo pia:
Ni kumkopesha kiwango fulani cha fedha mtu binafsi au taasisi, kama fedha taslimu. Ingawa, si njia nzuri ya kukopeshana fedha. Yeyote anaekopesha fedha huweka orodha ya masharti. Kiwango fulani cha fedha kitaongezwa kwenye kile kiwango ulichokopeshwa baada ya muda flani. Mtu, anaekopesha fedha, huhitaji “kitu fulani” na anachokihitaji “kipo”.  Ana uhakika nacho. Kwa ufupi, mtu anaekopesha pesa, mkopeshwaji, huchukua bila kujali. Kwa upande mwengine, kuna mtu anaeishi kwa kupanda ngano kwenye shamba lake au kwa kuuza mazao yake sokoni; na huyu mtu hana sharti lolote kwenye kipato chake. Si kwa faida wala kiwango fulani atakachopata kwamba kina uhakika. Kwa sababu hii, mara nyingi huomba dua. Akianza kupata faida, humshukuru Mungu. Siku zote humkumbuka Ambae amempa rehema na mafanikio haya. Hufanya kwa kiwango kizuri kadri atakavyo, kwa kadri sababu zilivyo; ingawa, anajua kwamba sababu hizi si zao la yale anayoyatarajia. Kwa sababu hii, huzizingatia juhudi zake sababu zisizotosha za kumfikisha kupata maisha yake. Hajiamini vyakutosha mwenyewe. Kuna tofauti kubwa kwenye hizi hali mbili. Hali ya kwanza, ni sababu madhubuti na za uhakika; hupata kipato chake, sio mafaniko wala rehma zinazopatikana kwake (rizq). (Determinism)
Riba humfanya anaekopesha awe mbali na kumtumikia Allah. Ukweli ni kwamba, matokeo haya kwenye kupanua ukuta wa sababu na wale wanaoegemea ukuta huu huanza kujiona wenyewe wanasifa za Uungu kwasababu ya mwanya unaosababishwa na kujiona wana uwezo wa kufanya lolote walitakalo. Kwa maneno mengine, riba huwadhibiti watu wakafikia kutokujitambua, ambapo huwafanya kuamini kwamba kila kitu kimeumbwa kwa visababishi. Hali hii humzuia mtu kuingia kwenye kumtumikia Allah. Mtu ambae yupo sehemu fulani kati ya kuogopa na matarajio, maisha na kifo, na shibe na njaa ni muumini kwa kadri atakavyokuwa na uelewa wa hali hii. Riba humzuia mtu kutambua hali hii. Na tunadhani hii ni moja kati ya hekima nyuma ya sababu kwanini riba ikatazwe. Haina shaka kwamba, kukatazwa kwa riba kuna umuhimu mkubwa sana katika Uislamu. Umuhimu wa mzizi wa jambo hili unatoka kwenye ukweli kwamba riba, ambayo imekatazwa kwa nguvu zote katika Qur’an na Hadithi, ni moja kati ya nukta za msingi kwenye uchumi wetu leo (ambao si wa Kiislamu). Mbali na hilo, si jambo la kutia chumvi kusema kwamba uchumi wa zama za leo umemezwa na sera na huduma za kiriba.
Kiwango cha fedha na masoko ya mitaji leo kinajulikana na kila mmoja. Kwa upande mwengine, ni vigumu hasa kuona kampuni au mjasiriamali ambae anamiliki mtaji wake binafsi kuanzisha biashara mpya au kuendelea na biashara zao kwa mafanikio yao ya kiuchumi. Inajulikana kwamba riba imekatazwa katika dini yetu kwa sheria kali sana ingawa inafanya kazi muhimu katika biashara na uchumi mkubwa zama hizi. Hatimae, inasababisha Waislamu wote ndani ya Uturuki na duniani kote wabaki njia panda na kuwafanya kama wafu kwenye biashara na maisha ya kijamii, ambapo ushirikiano na taasisi za kifedha ni takriban jambo la lazima leo. Matokeo yake kutokana na ukweli kwamba jambo la riba halielezwi kwa upana na kwa ufasaha kwenye maandiko ya Uislamu na vyanzo vyengine na hivyo watu wenye dini ambao hawapati taarifa za kutosha kuhusiana na jambo lenyewe hupendelea kujitoa kwenye taasisi na huduma za kifedha kwa kuogopa kwamba watafanya makosa na kufanya madhambi. Lengo la Makala hii ni kuchangia kwa kiasi kwenye kuwaangazia watu wetu, ambao huhoji juu ya riba.
Maana ya riba
Kwa mujibu wa wataalamu wa uchumi, riba, ambayo imekuwa na kazi muhimu katika uchumi wa soko huria, huamua mgawanyo kati ya matumizi na manufaa ya vyanzo. Matumizi ya vyanzo huelekezwa moja kwa moja zaidi kwenye maeneo yanayozalisha kupitia mfumo wa riba. Pakiwa na upungufu wa vyanzo, basi hupendekezwa kuwekeza sehemu zinazozalisha kidogo.  Kwa mujibu wa maana pana, riba ni gharama inayobebwa ili kurudishwa kwenye pesa iliyoazimwa.  Kwenye dhana finyu, riba ni gharama ambayo mkopeshaji humlipisha mkopaji kwa matumizi ya fedha za mkopeshaji. Kwa mtazamo huu, hubadilishwa kulinganga na usambazaji (supply) na mahitaji (demand) kwenye soko la mtaji. Vile vile huitwa “gharama za riba”.
Riba ni kipato kinachojitegemea kisichotokana na mtu binafsi ambae ndie mmiliki wa fedha. Inaonesha kwamba kiwango cha riba kwa ujumla hupangwa kwa mujibu wa masharti ya soko na kwamba mkopeshaji hajishughulishi na chochote. Ukweli ni kwamba, uhusiano binafsi uliopo baina ya wateja na taasisi za kifedha hupotea taratibu na mamilioni ya watu hawawajui kabisa wamiliki au mameneja wa mabenki ambayo huweka fedha zao. Hii ni kusema; uhusiano binafsi baina ya taasisi na watu hufikia hatua takriban kufutika kabisa. Kwa mtazamo mwengine, riba ni gharama inayotozwa kama mrejesho kwa ajili ya kuahirisha au kuendeleza matumizi ya bidhaa au huduma. Huwezesha kuunganisha baina ya leo na siku za usoni.
Riba ni gharama ambayo huamuliwa kwa ndani ya muda fulani ambao mkopeshaji hujinyima pesa aliyoikopesha kwa kiwango (rate) fulani, kukiwa na deni la kurudisha kiwango fulani cha pesa. Ufafanuzi huu, ambao unatathmini jambo lenyewe kwa mtazamo wa kisheria, huweka mbele vitu viwili – muda na kiwango cha riba – ambavyo vinawezesha kuibuka kwa riba. Kwa maana mbalimbali,  tunaona kuwa riba ni gharama inayotozwa kama mrejesho wa matumiz ya fedha. Si kweli; kwasababu si lazima kwa mkopaji kutumia fedha hizo ili mkopeshaji awe na haki ya kupata riba. Jambo muhimu na linalotosheleza kuibuka kwa riba ni ukweli kwamba mkopeshaji amejinyima pesa na kuikopesha kwa muda. Ni lazima kupata riba kutoka kwenye fedha iliyokopeshwa iwapo tu fedha imepokelewa na aliyekopa kwa sharti kwamba atarejesha baada ya muda fulani. Na kwa mujibu wa maana maarufu na pana, riba inamaanisha kipato kwa ajili ya mkopeshaji na kupitia gharama za mkopaji. Kwa neno la Kiislamu, riba imeelezwa kwa dhana ya “riba”. Riba maana yake ni kupunguza, wingi na kuongeza. Kwa hiyo, kiwango cha ziada cha pesa or bidhaa kinachotozwa kama mrejesho kwa chochote kilichoazimwa kinaingia katika mawanda ya kilichokatazwa. Riba vile vile maana yake ni kipato cha haramu. Kwa mujibu wa maana nyengine kwenye Sharia za Uislamu, “riba ni sharti la kupunguza katika biashara.”
Aina za Riba
Zipo aina nyingi sana za riba kidhahania na kiuhalisia na zinaweza kugawanywa kwa kuzingatia vigawanyo fulani. Tumeona ni sahihi kuzungumzia jambo hili kwa upana kusaidia ufahamu mzuri wa jambo hili la riba. Kwa kawaida, riba inalipwa pamoja na mtaji wa fedha mwishoni mwa muda ulioruhusiwa. Inaitwa riba ya kawaida; ni rahisi kuipigia mahesabu na si ngumu hata kidogo. Hakuna tofauti kati ya kiwango cha riba kilichotangazwa au kilichokubaliwa na kile cha uhalisia. Kinachomaanishwa ni kwamba “riba kwenye maandishi” ni riba ya kawaida; ingawa bado haitozingatiwa kwamba ni riba halisi. Ni “riba ya kiwanja” (compound interest) ambayo huongezeka na mtaji wa wanyama na kumtoa kwenye njia mkopaji. Na kwa ufupi, inamaaisha kubadili riba juu ya riba. Kwa mfano, riba inakusanywa mara nne kwa mwaka kabla ya deni kurudishwa ndani ya muda ulioruhusiwa, kwenye mikopo ya kibiashara, ambayo huwa ya mwaka mmoja. Kwa sababu hii, kiwango cha riba ambacho hutangazwa kwa mteja kama 60% kwenye maandishi huwa 75% kiuhalisia. Riba ya kiwanja (compound interest) huongezeka zaidi  kwenye kadi ya madeni ya mikopo (credit card debts) ambapo mtaji na riba huganywa kwa kuweka fedha kila mwezi (monthly installments). Hakuna benki wala taasisi za kifedha zinazowaambia wateja wake kuhusu kiwango cha riba ya kiwanja. Ingawa, chakufurahisha zaidi, benki hizo hizo hasa zinazowataarifu wateja wake kuhusu riba hiyo na kuweka msisitizo juu ya riba ya kiwanja katika marejesho kwenye kipato ambacho wanawapatia wateja wao. Riba ya kiwanja husababisha matokeo mabaya sana kwa wakopaji. Baadhi ya wakati huwafanya wakopaji kushughulika na deni lililokwisha mezwa hata kabla hawajagundua; kama vile mpira mdogo wa theluji “snowball” na kugeuka kuwa maporomoko ya thelugi (avalanche).
Riba ya punguzo (Discount Interest): Ni hali ya kipekee ya mkopo ambayo riba inawekewa kiwango maalumu, na baadae asilimia hiyo huondolewa kutoka kwenye kiwango cha mkopo, na mkopaji hupewa mabaki ya mkopo. Aina hii ya riba kwa kawaida humdanganya mkopaji. Kwa mfano, riba ya punguzo la riba, ambapo muda wake ni miezi sita, ambayo husemwa na benki kuwa ni 40%, kampuni ya kiwanda au mkopeshaji yoyote kwa mwaka hufikia 56% kiuhalisia.
Riba ya Changamoto (Default Interest): Kiwango kikubwa cha riba ambacho lazima mkopaji alipe baada ya changamoto alizopata. Kama mkopaji atapata matatizo kwenye mkopo, ni lazima alipe riba ya changamoto ili amfidie mkopeshaji kwa kiwango cha hatari kilichoongezeka kwa ajili ya kumuongezea mkopo. Husimamia dhana kwamba wakopaji siku zote wanatabia mbaya na hawalipi mikopo yao ipasavyo. Hapafanywi utafiti kujua labda mkopaji amepata matatizo yoyote. Wakopeshaji hawataki kuthibitisha walichopoteza ili kuwa na haki ya kuwatoza wakopaji riba ya changamoto (default interest) na wakopaji hawawezi kujitoa kwenye riba ya changamoto hata kwa kuthibitisha matatizo yao.
Riba ya Fidia (Compensatory Interest): Riba inayotozwa hasa kwa kufidia hasara iliyofikiriwa ya mkopeshaji ambae hakulipwa ndani ya muda. Mkopeshaji halazimiki kuthibitisha hasara yake; kuchelewesha malipo ya deni inatosha kuwa sababu.
Riba ya kuvunja makubaliano (Penal Interest): Ni riba ya adhabu inayotozwa na mkopeshaji iwapo kiwango cha malipo (installments) hakikulipwa kwa mujibu wa mikataba ya mkopo. Inaweza kuwa aina yoyote ya deni kwenye kuongezea madeni ya fedha iliyokopeshwa.
Riba ya kisheria (Legal Interest): Kiwango cha riba ambacho kimeruhusiwa au kilichotakiwa kutozwa kwa mujibu wa sheria; kulingana na mafungamano yenye kujitegemea. Hata kama wahusika hawakuweka kumbukumbu ya sharti la riba kwenye mkataba, asiyelipa deni lake hutozwa riba kwa mujibu wa sheria.
Riba ya Makubaliano (Conventional Interest): Ni aina ya riba ambayo haimo kwenye maandishi ya taasisi ya kiserikali. Kiwango cha riba kinaweza kuamuliwa na kurikodiwa kwenye mkataba kwa makubaliano ya pande mbili.
Riba ndani ya mapito ya Kihistoria
Riba iliibuka kutokana na kukopeshana katika zama za zamani sana. Uchimbaji uliofanyika Uturuki umeonesha kwamba wafanyabiashara wa Ashuru (Assyrian) walikuwa wakiuza tini (tin) na ngano kwa Wa-Anatolia (ambapo kwa sasa inajulikana kama Uturuki) kwa riba ya 100% kwa dhahabu iliyokopwa na sarafu za fedha, miaka 2000 kabla ya ujio wa Nabii Issa (Yesu). Riba, ambayo ni kongwe kama ilivyo historia ya mwanadamu, ndio imekuwa sehemu ya kivutio kwa wanafalsafa na wachungaji. Imekuwa ni jambo la kuingiliwa na serikali kwenye dini zote na mifumo yote ya sheria. Imeonekana ni jambo lenye hasara kwenye pande zote mbili kitabia na kijamii kwasababu inathibitisha kwamba mkopeshaji anajivunia kupata kipato kisicho cha heshima na kumsababishia mkopaji hali ngumu za kifedha kama kikiwa kwenye kiwango cha fedha ambacho hupelekea kutoka kwenye makubaliano ya ukopeshanaji au aina zingine za mikataba ambayo huongeza deni. Tangu zama hizo za zamani, riba imetathminiwa kama mafundisho ya dini, jambo la haki na tabia.
Aristoto, mwanafalsafa maarufu wa Kigiriki, anaeleza yafuatayo kwenye kitabu chake maarufu kilichoitwa “Siasa”:
“Jambo linalochukiwa sana (lenye mnasaba na kupata utajiri) na lenye sababu yenye nguvu, ni riba, ambayo hutengeneza mazingira kujipatia fedha kutokana nayo na sio kutoka kwenye kitu halisi. Pesa ilikusudiwa kuwa chombo cha kubadilishana na sio kuongeza riba…Katika mifumo yote ya kupata utajiri, kwa kiasi kikubwa si asili”.
Thomas d’Aquin anasema:
“Haiwezekani kuuza pesa na matumizi ya pesa yakatenganishwa. Haiwekani kutenganisha matumizi ya kitu kutoka ndani ya kitu chenyewe na kukiuza kwa njia hii, si haki, ni kama wizi kumtoza mtu riba kwa matumizi ya kitu kwasababu ni kukiuza kitu hicho hicho mara mbili (matumizi ya kitu na kukitenganisha kitu chenyewe). Ikiwa riba ni gharama ya muda, hakuna mtu mwenye haki ya kuidai; kwasababu muda ni jambo la kawaida kwa kila mtu na unamilikiwa na Mwenyezi Mungu. Hivyo basi, kutoza riba ni wizi na vile vile ni uhalifu unaofanywa dhidi ya Mwenyezi Mungu ambae anawapa watu muda bila malipo.”
Sheria zote za Roma na Ugiriki ya zamani, riba ilikatazwa na ikapigwa marufuku kabisa, kwa kutumia mbinu mbali mbali.
Kwenye Uyahudi halisi, riba ilikatazwa. Baadae, katazo hili liliharibiwa kutokana na mahusiano yaliyopo baina ya Waisraeli na ikahitimishwa kwamba katazo hili lilikuwa sahihi tu baina ya Waisrael na ikaruhusiwa kuwatoza riba wasiokuwa Wayahudi.
Mtazamo dhidi ya riba kwenye Ukristo ulijitokeza kwa hatua mbalimbali. Nabii Issa (Yesu) kwa njia isiyo ya moja kwa moja alikataza matumizi ya kinachotokana na riba na akapendekeza kwa mitume wake kutenda mema kwa kuchangia na kuwasaidia wengine bila kutaraji malipo. Ingawa kanisa liliendelea kutekeleza katazo hili kwa muda mrefu, Ilitokea kuikubali riba taratibu kwasababu ya ukandamizaji uliofanywa kifedha na kijamii na hasa ulipoibuka mfumo wa Ubepari. Jean Calvin aliruhusu matumizi ya kipato kitokanacho na riba kwasababu aliizingatia kama sio njia pekee ya matumizi bali hata uzalishaji. Kulingana na wafanyabiashara, riba ni kodi ya mtaji. Kuizingatia riba sawa na kodi ya ardhi na kodi ya uwekezaji wa mashamba (real estates), Wafanyabiashara wakasema, “Riba ni kodi ya mtaji.” Kwa mujibu wa wanauchumi wa Kifaransa karne ya 18 (physiocrats), riba kwenye kiwango kilichokopeshwa haiwezi kuwa chini ya kipato ambacho ardhi iliyonunuliwa na kwa kiwango ambacho fedha hiyo kingetoa. Wataalamu wa jadi wa uchumi kama vile Adam Smith na David Ricardo wanaizingatia riba ni mrejesho ambao mkopaji hulipa kwa mkopeshaji kutokana na faida ambayo mkopaji ataipata ya fedha alizokopa. Kwenye uchumi wa kijadi, ambao msingi wake ni wa muwezeshaji fedha-mjasiriamali, riba na faida vinatathminiwa na kuchanganywa pamoja. Kwa mfumo wa viwanda wanauchumi wa jadi walifikia kuthibitisha kwamba fikra hiyo ni sahihi. Karl Marx, ambae anajulikana kama mtu ambae ameisoma Kur’an, anaitaja riba kama jambo ambalo si halisia na ovu. Keynes, si kama walivyo wanauchumi wa jadi wengine, ametetea kwamba riba si jambo muhimu kwenye uwekezaji. Kwa mujibu wa yeye, riba haichochei uwekezaji; na kinyume chake, riba hurudisha nyuma uwekezaji.
Katazo la riba katika Uislamu
Riba ilikatazwa taratibu kwenye Kur’an na ikaelezwa kwenye aya mbalimbali. Kwenye aya ya 279 ya suratul-Baqara kwa ufupi na kwa ufasaha sana inasema:
“…Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe.”
Aidha, Mtume (rehma na amani ziwe juu yake) amesema katika hotuba yake ya kuaga:
“Mwenyezi Mungu amewakataza msichukue riba, kwa hivyo aina zote za riba lazima zifutwe. Mtaji wenu, ndio haki yenu kuuhifadhi. Hamtoingiwa na tamaa wala hamtokabiliwa na dhulma.”
Ujumbe wa aya hizi na hadithi, kwa ufupi ni kama ifuatavyo:
Mtu hatakiwi kuchukua ziada ya anachokopesha. Mkopeshaji ana haki ya kuchukua mtaji wote aliokopesha. Kwa mujibu wa maana ya msingi na ya moja kwa moja hapa, utaratibu wa kukopeshana haufanywi kwa misingi ya kutengeneza faida. Tukizingatia pamoja na hadithi zingine, tunafahamu kwamba mrejesho wa ziada haupaswi kuwa wa aina sawa na kilichokopeshwa.
Na hii ni kusema kwamba; kwa mfano, ikiwa kitu kilichokopesha ni aina A, riba bado imekatazwa hata kama ni aina B. Maana nyengine kwenye aya na hadithi ni kwamba mkopeshaji ana haki ya kuchukua mtaji wake wote aliokopesha. Ingawa inaonekana ni maumbile, si siku zote kwamba inawezekana kukusanya mtaji wote kama ulivyo.  Kwa mfano, fedha iliyowekwa kwenye benki za Ulaya inapungua eti kwasababu inahifadhiwa na kulindwa na benki; ilipaswa kuongezeka. Kwenye nchi za mwanzo za umoja wa kisovieti ikiwemo Jamhuri ya Kituruki na Shirikisho la Urusi leo, pesa inayowekwa benki hurejeshwa kwa mwenyewe baada ya kupunguzwa 10-15%. Ingawa huduma hii kwa aliyeweka ingeweza kujikita kwenye makubaliano ya pande mbili, lakini si hivyo. Kwakweli, ni jambo lisilopingika kwamba mabenki – ambayo yanaheshimiwa na ziko bayana – zimepata nguvu za ushawishi ambazo zinawashawishi wateja wao kuyakubali masharti yao. Uwanja mwengine wa biashara wa uwekezaji mabenki, ambazo ni taasisi zenye nguvu za ustaarabu wa Kimagharibi, ni kudhibiti utajiri wa watu kwenye mitaji ya mtu na kukusanya riba. Ingawa, kwenye kipindi cha anguko la uchumi, yale mabenki yaliyorudisha kiwango kidogo cha pesa kuliko wanachopokea, huku wakitangaza hasara. Inajulikana kwamba mtaji wa kuwekeza, ambao umeenea Uturuki, baadhi ya wakati husababisha madhara kwa wawekezaji, ambao huwajibika. Ingawa katika Uislamu, wawekezaji, wanaoweka pesa na wakopeshaji hulindwa kwa haki zao za kuchukua mtaji wao kama ulivyo. Kwa mtazamo huu, mtu ambae halipi deni lake kwa wakati huzingatiwa kama kalazimishwa. Kwa mujibu wa wataalamu wa tafsiri ya Kur’an, mkopeshaji/mwenye kuweka/muwekezaji halazimishwi kuchukua fedha zake ikiwa hazijatimia. Mbali na hilo, kuna tafsiri zinazoelezea kwamba mkopeshaji/mwenye kuweka/muwekezaji wanaweza kuomba fidia kwa upotevu kwa ongezeko la mtaji ikiwa hakulipwa kwa wakati, kwa sharti kwamba ni makubaliano yalirikodiwa mwanzoni kabisa.
Sababu kwanini riba imekatazwa
Maana ya pili muhimu iliyomo kwenye aya na hadithi ambazo zimetajwa hapo juu ni kwamba riba hupelekea dhulma. Ni jambo lisilopingika kwamba ima mkoposhaji au mkopaji atahudumiwa bila kuzingatia haki ikiwa itatozwa riba wakati wa kukopa. Maisha ya kifedha kwenye sehemu zote mbili kwenye nchi na dunia kwa ujumla ina mifano mingi inayothibitisha vilivyo jambo hili. Ukweli ni kwamba, mabenki yanatafsiriwa kama “taasisi ambazo huweka miavuli kwa wateja wao kwenye kipindi cha jua na wanaichukua mara tu mvua ikianza kunyesha” kwenye ulimwengu wa Magharibi, ambapo taasisi hizo zilivumbuliwa. Historia ya hivi karibuni ina ushahidi wa kesi nyingi kubwa ambapo kwa pamoja mkopeshaji na mkopaji walikiuka haki za kila mmoja na hatimae haki za watu wengi wasio na hatia zilikiukwa. Wakurugenzi wa mabenki waliojitokeza kutoka kusikojulikana wakiwa na vyeti feki walinunua ofisi rahisi na ndogo na kukusanya kiwango kikubwa cha fedha kutoka kwa watu wakiwaahidi riba. Pensheni kwa wastaafu na mishahara iliwekwa kwa wakurugenzi hao wa mabenki wakiwa na matumaini ya kupata riba. Baadhi ya watu walifikia hadi hatua ya kuuza nyumba walizokuwa wakiishi na wakaanza kuishi kwenye nyumba za kukodi/kupanga ili waweke fedha kwa wakurugenzi wa mabenki wapate faida. Hatimae, ilienda mbali sana kutokana na udanganyifu usiokwisha wa wakurugenzi wa mabenki na kufikia kiwango hatari cha tamaa/kufilisika cha wawekaji pesa kwamba riba ilitozwa kwa pesa iliyowekwa hata kwa siku moja ili kuongeza kilichojulikana kwa jina la “mlolongo wa furaha”.
Na mwishowe, wakurugenzi wa mabenki walipotea na fedha zote walizokusanya. Baadhi yao walikamatwa hawana chochote cha kuchukua toka kwao. Bado wengine walifikia kuuliwa na wengi kati yao walifungwa jela. Watu waliporwa mbele ya macho ya serikali kipindi cha matukio haya ambayo yalirikodiwa kama janga la wakurugenzi wa mabenki kwenye historia ya uchumi. Tunajua kwamba wafanya biashara wengi wakubwa na wadogo walifilisika kwasababu ya madeni yao waliyodaiwa na watoza riba kwenye miji yote kwenye nchi yetu hasa ikiwemo Istanbul. Na baadhi ya wakati tunawasikia waliomuua mtoza riba anaewadai kama suluhisho la mwisho la kujikwamua kwenye madeni. Muuwaji wa Nesim Malki ambae alitokea mwaka 1996 ni kesi ya wazi inayoonesha kwamba wakopaji si siku zote kwamba hawana hatia. Wakati mtikisiko wa uchumi ulipoanza mwaka 1994, mabenki yalituma tahadhari fupi ya maandishi kwa wateja wao wakisema kwamba wanatoza riba ya 700% kwa wateja wenye kadi za madeni asbuhi yake. Viwanda vingi na biashara zilifungwa siku chache baadae. Uhakika wa kuweka fedha bila kikomo zilianza kuandikwa kurasa za mbele na serikali kugeuza kama ngao kuzilinda riba za mapato kutoka kwa wale ambao hawakuwa na pesa walizoweka mabenki. Wakati wa anguko la uchumi Novemba 2000 na Februari 2001, viwango vya riba viliongezeka ghafla na kufikia 3000%.
Makampuni yasiyo idadi yalifilisika na maisha yao ya fedha yakaishia hapo. Kwa upande mwengine, baadhi ya wafanyabiashara walihamisha faida walizokuwa wakipokea kutoka mabenki na kuziweka kwenye akaunti zao binafsi badala ya kuzitumia kwenye biashara. Hata wamiliki wa mabenki hawakuona chochote kibaya kwa kusua sua benki zao. Hatimae, benki 22 zilifilisika; wamiliki wake wakafungwa jela na wakaadhiriwa mbele ya kila mtu. Haya yote yanayotokana na mitikisiko hiyo ambayo ilitupiwa jamii.
Kwa ufupi, hekima nyuma ya katazo la riba ni kwamba ima mkopeshaji au mkopaji, wote kama ilivyoelezewa juu watakosewa na hatimae jamii nzima itadhuriwa ingawa haikuhusika na kesi. Tumegundua riba iliyofichwa nyuma ya mabarakoa kwenye kila jambo linalohusu uchumi kutokana na zana za kutosha na aina mbali mbali za fedha na taasisi katika zama za leo. Kwa mawazo yetu, tunapohitimisha, ikiwa kuna njia yoyote ya kifedha inaingizwa kwenye uwanja wa katazo la riba leo, kigezo chetu ni kwamba lazima njia hizo za fedha ima zitasababisha dhulma au madhara kwa mkopaji na mkopeshaji au jamii.
Maswali juuyau islamu

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU

Kisa Cha Nabii Ibraahiym عليه السلام - Sehemu Ya 1