Ni ipi amri juu ya ushungi katika Uislamu? Kuna hatari gani kwa wanawake ya kutoka bila ya kuvaa ushungi?
Kwenye nukta hii, kuna aya mbili katika the Quran Tukufu. Katika aya hizi, Allah Mtukufu anatangaza waziwazi:
“Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao (wanapotoka nje ya nyumba zao na wanapokuwa mbele ya wanaume wasiokatazwa kuwaoa kwa sababu ya nasaba).” (1)
“Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao …” (2)
Katika aya hizo, haioneshwi waziwazi jinsi gani wanawake waumini wajitande mitandio, na mahali gani wanaweza kuonekana. Hata hivyo, hadithi hii inatafsiri aya hizo kama ifuatavyo: Mtume Muhammad (S.A.W) alimwambia shemeji yake, Asma: “Ewe Asma! Mwanamke haruhusiwi kuonesha sehemu za mwili wake kwa wageni isipokuwa mikono yake na uso baada ya kufikia umri wa baleghe.” (3)
Kuwa Mwanamke Muislamu katika umri wa baleghe anapaswa asitiri nywele zake kwa amri ya Allah (SWT) na Mtume’s (SAW). Yaani, ni wajibu kusitiri kichwa kwa namna ambayo uso utakuwa wazi na kusitiri shingo na kifua. Ama kuhusu mtu kutokujisitiri kwa mtandio, kunamaanisha kuacha wajibu na hilo limekatazwa. Anapata madhambi na kwamba anabebeshwa jukumu kwa kuwa hazingatii amri ya Allah (SWT) na Mtume (S.A.W). Mtu mwenye madhambi lazima atubu na kuomba msamaha kutoka kwa Allah (SWT) ili afutiwe dhambi yake.
“Na ambao pindi wafanyapo uchafu au wakajidhulumu nafsi zao humkumbuka Mwenyezi Mungu na wakamwomba msamaha kwa dhambi zao - na nani anaye futa dhambi isipo kuwa Mwenyezi Mungu? - na wala hawaendelei na waliyo yafanya na hali wanajua. Hao malipo yao ni msamaha kwa Mola wao Mlezi, na Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu, na mwema mno ujira wa watendao!” (4)
Kwa hivyo, ili toba ipokelewe au dhambi isamehewe, mtu anatakiwa asiendelee na dhambi hiyo pasi na udhuru wowote.
Hapa kuna hadithi juu ya nukta hiyo:
“Muumini anapotenda dhambi, hutokea doa jeusi moyoni mwake. Ikiwa ataiacha dhambi hiyo na akamwomba msamaha Allah (STW), moyo wake utasafika doa hilo jeusi. Ikiwa ataendelea na dhambi hiyo, doa jeusi litakuwa kubwa. Ni kwa hali hii ndipo “dhambi huufunika moyo, ambayo ipo katika Qur’an.” (5)
Kauli “Katika kila dhambi kuna nia inayopeleka kwenye ukafiri.” inaeleza ukweli ulio muhimu. Mtu anayedumu katika kutenda dhambi anaizoea dhambi hiyo kadiri wakati unavyosonga mbele na hawezi kuiacha. Tabia hiyo inamvutia kwenye hatari kubwa za kiroho. Anaanza kuamini kuwa dhambi hiyo haina adhabu huko Ahera na Jahanamu haitakuwepo hata kidogo. (6)
Ili mtu huyo asikutane na hatari kama hizo na asidanganywe na Shetani, anahitajika ajiondoe na kuiacha dhambi hiyo, hilo litaleta toba yake.
(1) (al-Ahzab, 33:59)
(2) (an-Nur, 24:31)
(3) (Abu Dawud, Libas, 33)
(4) (Aal-i Imran, 3:135-136)
(5) (Ibn Majah, Zuhd, 29)
(2) (an-Nur, 24:31)
(3) (Abu Dawud, Libas, 33)
(4) (Aal-i Imran, 3:135-136)
(5) (Ibn Majah, Zuhd, 29)

Comments
Post a Comment