Namna ya Adhana na Iqama

Allah amewawekea Waislamu Adhana kwa ajili ya kuwaita watu katika swala, na kuwatangazia kuingia kwa wakati wake. Pia ameweka Iqama kwa ajili ya kuwatangazia juu ya kufika kwa wakati wa kuanza kwa swala. Waislamu  walikuwa wanakusanyika na kuswali katika nyakati zake bila ya kuwepo yeyote aliyekuwa akiitolea taarifa swala. Siku moja walilijadili jambo hilo. Baadhi yao walisema kuwa: «Wekeni kengele kama kengele za Wakristo». Wengine wakasema kuwa: «Hapana! Wekeni tarumbeta kama matarumbeta ya Wayahudi». Omar akasema kuwa: «Hivi mnaonaje mkimtuma mtu akawa anawatangazia watu swala?». Mtume ,swallalahu alayhi wasalam, akasema kuwa: «Ewe Bilali, simama na ita (watu) kwenye swala». (Bukhari, Hadithi Na. 579.   Muslim, Hadithi Na. 377)

Namna ya Adhana na Iqama

  • Adhana na Iqama ni lazima katika swala za Jamaa, si kwa mtu anayesali peke yake. Kama watu wata acha kuadhini na kuqimu kwa makusudio swala yao ni sahihi lakini watapata dhambi.
  • Sheria inataka Adhana itolewe kwa sauti nzuri na kubwa ili watu wasikie na waje kuswali.
  • Zimethibiti kunukuliwa namna  mbalimbali za Adhana na Iqama kutoka kwa Mtume,swallalahu alayhi wasalam. Maarufu zaidi ya namna hizo ni hizi zifuatayo:

Adhana:

«Laa Hawla Walaa Quwwata Illaa Billaah». Maana yake ni kwamba: Hatuna nguvu na uwezo wa kufanya ibada isipokuwa tu kwa kuwezeshwa na Allah.    
1Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar.  (Allah ni mkubwa sana, Allah ni mkubwa sana, Allah ni mkubwa sana, Allah ni mkubwa sana). 
2Ash-Hadu Al-Laa-Ilaaha Illallah, Ash-Hadu An-Laa-Ilaaha Illallah (Ninakiri kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah tu, Ninakiri kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah tu).
3Ash-Hadu Anna Muhammadan Rasuulullah, Ash-Hadu Anna Muhammadan Rasuulullah, (Ninakiri kuwa Muhammad ni Mtume wa Allah, Ninakiri kuwa Muhammad ni Mtume wa Allah).
4Haiyya Ala-Sswalaa, Haiyya Alaa-Sswalaa (Njooni kuswali, njooni kuswali).
5Haiyya Alal-Falaah, Haiyya AlalFalaah. (Njooni kwenye mafanikio, njooni kwenye mafanikio).
6Allahu Akbar, Allahu Akbar.(Allah ni mkubwa sana, Allah ni mkubwa sana).
7Laa-Ilaaha Illallah.(Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah tu).
  • Katika Adhana ya Alfajiri ataongeza “Asswalaatu Khairun Minan-naum, Asswalaatu Khairun Minan-naum” baada ya “Hayya Alalfalaah”.

Iqama: 

1Allahu Akbar, Allahu Akbar.(Allah ni mkubwa sana, Allah ni mkubwa sana).
2Ash-Hadu Al-Laa-Ilaaha Illallah, (Ninakiri kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah tu).
3Ash-Hadu Anna Muhammadan Rasuulullah, (Ninakiri kuwa Muhammad ni Mtume wa Allah).
4Haiyya Ala-Sswalaa, (Njooni kuswali, njooni kuswali).
5Haiyya Alal-Falaah. (Njooni kwenye mafanikio).
6Qad Qaamatis-swalaa, qad qaamatis-swalaa. (Hakika, swala imesimama, hakika swala imesimama).
7Allahu Akbar, Allahu Akbar.( Allah ni mkubwa sana, Allah ni mkubwa sana).
8Laa ilaaha illa-llaah.( Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah tu).

Kusema kama anavyosema Muadhini

Inapendekezwa kwa anayesikia Adhana aseme kama Muadhini anavyosema, isipokuwa Muadhini atakapo sema: (Haiyya Alaas-swalaa, (Njooni kuswali,) au (Haiyya Alal-Falaah. (Njooni kwenye mafanikio) yeye atasema: (Laa haula walaa quwwata illaa billaah) (Hakuna ujanja (wa kufanya mema) wala nguvu (ya kuepuka maovu) isipokuwa kwa uwezo wa Allah tu).
Halafu aliyeisikia Adhana na baada ya kuikariri atasema: «Allahumma Rabba hadhihid-dawati-ttaamma waswalaatil-qaaimma aati Muhamadan alwasiilata walfadhiila wab-ath-hu maqaaman mahamuudan alladhii wa-attahu) (Ewe Mola wangu, Bwana wa wito huu uliotimia, na swala yenye kusimama, mpe Muhammad wasila na fadhila na mfikishe katika sehemu yenye kusifika ambayo umemuahidi.)

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU