Mwakinyo: Mfilipino Hafiki Raundi Mbili
BONDIA Mtanzania, Hassan Mwakinyo amesema kuwa mpinzani wake, Arney Tinampay raia wa Ufilipino, hataweza kumaliza hata raundi mbili kwenye pambano lao litakalofanyika Novemba 29 kwenye Uwanja wa Uhuru.
Akizungumza na Kijiwe cha Ndondi, Mwakinyo alisema: “Kwa jinsi nilivyojiandaa na pambano hilo, sidhani kama Tinampay atafika raundi ya pili, kwa sababu mimi napenda sana kumpiga mtu kwa KO, hivyo natarajia kufanya hivyo hata kabla raundi ya pili haijaisha.”

Comments
Post a Comment