MIFANO KATIKA MAISHA YA MTUME, SWALLALAHU ALAYHI WASALAM, NA TABIA ZAKE

Sifa na mema ya Mtume yakiwa yamechorwa katika Kibla cha Msikiti wa Mtume.
Mtume, swallalahu alayhi wasalam, alikuwa mfano wa kuigwa wa tabia za kibinadamu za kiwango cha juu sana. Kwa sababu hii, Qur’ani imezisifia tabia zake kwamba zilikuwa tukufu.Ummu Abdillah Aisha, Allah amuwiye radhi, mke wa Mtume hakupata wasifu unaoweza kuzieleza kwa undani zaidi tabia za mumewe isipokuwa tu alisema kwamba: «Qur`ani ilikuwa ndio tabia zake». (Ahmad, Hadithi Na. 24601). Maana ni kwamba Mtume alikuwa mtekelezaji wa vitendo wa mafundisho ya Qur`ani na maadili yake..

Unyenyekevu

  • Mtume, swallalahu alayhi wasalam, alikuwa hayuko radhi kumuona mtu  yeyote akisimama kwa ajili ya heshma yake, bali alikuwa akiwakataza maswahaba kufanya hivyo. Maswahaba, pamoja na mapenzi yao makubwa kwa Mtume, walikuwa  hawasimami wanapomuona anakuja. Hali hiyo sio kwa sababu nyingine isipokuwa kwamba walikuwa wanajua kuwa Mtume alikuwa akilichukia suala hilo. (Ahmad, Hadithi Na. 12345. Albazzaar, Hadithi Na. 6637)
  • Adiy Bin Hatim, Allah amuwiye radhi, ambaye alikuwa miongoni mwa mamwinyi wa Kiarabu alikwenda kwa Mtume kabla hajawa Muislamu akitaka kujua ukweli wa mahubiri ya Mtume. Adiy amesema: «Nilikwenda kwa Mtume na kukuta yuko pamoja na mwanamke na watoto wawili au mtoto mmoja», na akataja jinsi watu hao walivyokuwa wamekaa karibu na Mtume «..nikatambua kuwa Mtume hakuwa mfalme wa Kisra wala Kaisari». (Ahmad, Hadithi Na. 19381). Unyenyekevu ni  tabia ya Mitume wote.
  • Mtume alikuwa akikaa na maswahaba zake kama mtu miongoni mwao. Hakuwa akikaa mahali panapomfanya awe tafauti na wengine kiasi kwamba hata mtu mgeni ambaye hamjui akifika katika baraza aliyokaa hawezi kumtafautisha yeye na maswahaba zake. Alikuwa akiuliza kuwa: «Katika nyinyi, Muhammad ni nani?» (Bukhariy, Hadithi Na. 63)
  • Imenukuliwa kwa Anas, Allah amuwiye radhi, akisema kuwa: «Alikuwa kijakazi miongoni mwa vijakazi wa mji wa Madina akiushika mkono wa Mtume na kwenda naye popote anapotaka». (Bukhariy, Hadithi Na. 5724).  Makusudio ya kushikwa mkono ni ishara ya upole na kumsikiliza mtu mdogo na dhaifu. Pia Hadithi hii inataja aina nyingi za unyenyekevu wa Mtume wa kiwango cha juu sana, kwa ushahidi kwamba ametajwa mwanamke badala ya mwanaume, ametajwa mwanamke kijakazi badala ya mwanamke asiyekuwa kijakazi, kijakazi huyo anakwenda na Mtume popote atakapo kwa lengo la kutaka kutatuliwa matatizo yake. 
  • Amesema Mtume, swallalahu alayhi wasalam, kuwa: «Haingii peponi mtu ambaye moyoni mwake kuna chembe ya kiburi». (Muslim, Hadithi Na. 91)
Muislamu anasujudu juu ya ardhi katika kila swala ili akumbuke kuwa ameumbwa kutokana na mchanga na, kwa hiyo, afute kila athari ya kiburi katika moyo wake.   

Huruma

Amesema Mtume, swallalahu alayhi wasalam, kuwa: «Wenye huruma watahurumiwa na Allah Mwingi wa rehema. Wahurumieni walioko ardhini, atakuhurumieni aliyeko mbinguni». (Attirmidhiy, Hadithi Na. 1924. Abudaud, Hadithi Na. 4941).
Na hururma inaonekana dhahiri katika maeneo mengi. Miongoni mwa maeneo hayo ni haya:

Kuwahurumia watoto

  • Bedui (Muarabu anayeishi milimani) mmoja alikuja kwa Mtume, swallalahu alayhi wasalam, na kusema: «Hivi nyinyi  mnawabusu watoto wenu? Sisi hatuwabusu. Mtume swallalahu alayhi wasalam, akamjibu kwa kusema: Hivi nifanye nini mimi kama Allah amenyofoa huruma katika moyo wako?». (Bukhariy, Hadithi Na. 5652.  Muslim, Hadithi Na. 2317).     Mtu mwengine alimuona Mtume akimbusu Hussein Bin Ali akasema: «Hakika, mimi nina watoto kumi, sijawahi kumbusu yeyote kati yao». Mtume akasema: «Ilivyo ni kwamba, mtu ambaye hana huruma, hatahurumiwa». (Muslim, Hadithi Na. 2318)
  • Siku moja Mtume aliswali akiwa amembeba mjukuu wake Umama Binti Zainab. Akawa anamuweka chini akisujudu, na akisimama anambeba. (Bukhariy, Hadithi Na. 494. Muslim, Hadithi Na. 543)
  • Mtume alikuwa akiswali kwa wepesi na haraka asikiapo mtoto analia wakati yeye yumo ndani ya swala. Imenukuliwa kwa Qatada akisema kuwa, amesema Mtume, swallalahu alayhi wasalam kwamba: «Mimi huwa nasimama kwa ajili ya kusali nikikusudia kurefusha swala. Lakini nasikia mtoto akilia, na hivyo, naifanya nyepesi swala yangu kwa kuona vibaya kwamba nitamsumbua mama yake». (Bukhariy, Hadithi Na. 675. Muslim, Hadithi Na. 479)
Mtume alikuwa anaharakisha kuswali akisikia kilio cha mtoto.

Hururma yake kwa wanawake

Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amehimiza kuwalea watoto wa kike na kuwafanyia mambo mazuri. Mtume alikuwa akisema kwamba: «Mwenye kusimamia jambo kwa hawa watoto wa kike, na kwa hiyo, akawafanyia mambo mazuri, watakuwa kinga yake ya moto». (Bukhariy, Hadithi Na. 5649. Muslim, Hadithi Na. 2629)
Bali Mtume amekazia katika usia wa kutekeleza haki za mke, kuyajali mambo yake na hali zake. Amewaamrisha Waisalmu wausiane katika hilo, na kusema kuwa: «Usianeni kuwafanyia kheri wanawake». (Bukhariy, Hadithi Na. 4890)
Mtume ni mfano mzuri sana katika kuihurumia familia yake, kiasi kwamba alikuwa akikaa mbele ya ngamia wake na kusimamisha goti lake ili Sofia, Allah amuwiye radhi, akanyage goti la Mtume na aweze kupanda juu ya ngamia. (Bukhariy, Hadithi Na. 2120). Mtume alipokuwa akifuatwa na Fatma binti yake, alikuwa anaushika mkono wake, anambusu na kumkalisha mahali ambapo yeye amekaa. (Abudaud, Hadithi Na. 5217)
Mwenye kumhangaikia mjane na masikini ni kama mwenye kupigana Jihadi katika njia ya Allah na ni kama ambaye anafunga mchana na kusali usiku.

Huruma yake kwa wanyonge

  • Ni kwa sababu ya hurumu kwa wanyonge ndio maana Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amehimiza watu kuwalea watoto yatima. Alikuwa akisema kuwa: «Mimi na mlezi wa yatima tutakuwa kama hivi peponi». Alitoa ishara kwa kidole cha shahada na kidole cha kati. (Bukhariy, Hadithi Na. 4998).
  • Mtume amemfanya mtu anayemhangaikia mjane na masikini sawa na mpiganaji Jihadi, na sawa na mwenye kufunga saumu mchana na anayesimama kuswali usiku. (Bukhari, Hadithi Na. 5661. Muslim, Hadithi Na. 2982)
  • Mtume amefanya huruma kwa  wanyonge na kuwapa haki zao ni sababu ya kupata riziki na kupata ushindi dhidi ya maadui. Amesema kuwa: «Nitafutieni wanyonge (niwasaidie). Ilivyo ni kwamba mnapewa ushindi na mnapewa riziki kwa sababu ya (kuwasaidia) wanyonge wenu». (Abudaud, Hadithi Na. 2594)

Huruma yake kwa wanyama

  • Mtume alikuwa akihimiza watu kuwa na huruma kwa wanyama, kutowabebesha mizigo wasiyoweza  kuibeba na kutowasumbua. Amesema Mtume, swallalahu alayhi wasalam, kuwa: «Kwa yakini, Allah ameandika kufanya uzuri katika kila kitu. Mkiua ueni vizuri, na mkichinja  chinjeni vizuri, na mmoja wenu anoe kisu chake na amtulize mnyama wake aliyemchinja (asimuache akapaparika)». (Muslim, Hadithi Na. 1955).
  • Swahaba mmoja amesema kuwa: «Na Mtume aliona kichuguu cha wadudu chungu tumekichoma moto, akauliza: Ni nani aliyechoma moto kichuguu hiki? Tulijibu: Ni sisi. Mtume akasema: Ilivyo ni kwamba, hatakiwi kuadhibu kwa moto isipokuwa tu Muumba wa moto». (Abudaud, Hadithi Na. 2675)

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU