Meli Mpya MV Victoria Yaanza Kujengwa


WAKATI Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli inaendelea kujenga miradi mikubwa ya kimkakati ya kuelekea katika uchumi wa kati bado Mkoa wa Kagera haujasaulika bali sasa wananchi wake wanakumbushwa kujiandaa kikamilifu kwa kuchapa kazi za kilimo na biashara wakati nchi inaelekea katika mapinduzi makubwa ya kiuchumi ili kutembea na kasi ya uchumi wa kati.



Ni baada ya meli ya MV Victoria meli kongwe na maarufu kwa wakazi wa Mkoa wa Kagera kukamilika ukarabati wake ifikapo Machi 2020 na kurejea katika Ziwa Victoria kwa kufanya kazi kati ya bandari za Mwanza, Bukoba na Kemondo kusafirisha abiria zaidi 1000 pamoja na mizigotani 200 ambapo kutakuwepo na nafuu kubwa ya bidhaa za viwandani pamoja na usafiri wa wananchi kati ya Bukoba na mwanza.




Uhakika wa meli ya MV Victoria kukamilika ukarabati wake mwakani Machi 2020 pia na ujenzi wa meli mpya ulishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti pamoja na Kamati ya amani ya Mkoa wa Kagera iliyowajumuisha viongozi wa dini watatu Askofu Methodius Kilaini Askofu msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba, Askofu Dk. Abednego Keshomshahara Askofu wa (KKKT) Jimbo la Kasikazini Magharibi na Sheikh Haruna Kichwabuta Sheikh wa Mkoa wa Kagera.


Mkuu wa Mkoa Gaguti akiwa katika ziara hiyo ya kutembelea na kujionea maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa Meli mpya pamoja na cherezo katika Bandari ya Mwanza Kusini alisema kuwa anampongeza Rais Magufuli kwa kuleta mradi huo kwa ajili ya ukombozi wa kiuchumi wa wananchi wa Kagera kwani utaweka usafiri wa uhakika pia alitoa wito kwa wananchi wa Kagera kujielekeza katika kazi zenye tija za kilimo na biashara na kujiandaa kutumia maboresho ya usafiri kuinua uchumi wa mkoa.


Askofu Msaidizi Methodius Kilaini baada ya kuiona miradi hiyo mitatu alisema kuwa anamshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kutekeleza maajabu katika miradi ya ujenzi na ukarabati wa meli, aidha alisema kuwa Mkuu wa Mkoa Gaguti amewafanyia jambo jema sana la kuwafanya wao kama viongozi wa dini wapate nguvu ya kuleta tumaini na uelekeo kwa watu na kuufanya Mkoa wa Kagera kusimama tena kiuchumi.



Askofu Dk. Keshomshahara mara baada ya kujionea ujenzi wa meli mpya na cherezo na ukarabati wa Meli ya MV Victoria alisema kuwa sasa wao kama viongozi wa dini wamepata neno la kuwaeleza waamini wao na kuwahamasisha kujiandaa kwaajili ya kuitumia fursa ya Meli hizo zikikamilika.



Sheikh Haruna Kichwabuta naye alisema kuwa Rais Magufuli alihaidi wakati wa kampeini sasa ametekeleza bila ahadi hewa hasa kwa wananachi wa Mkoa wa Kagera.



Bw. Eric B. Hamissi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za meli nchini alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Gaguti kutembelea miradi hiyo ya ujenzi na ukarabati wa meli na kutoa wito kwa wananchi na viongozi wengine nchini kwenda kutembelea miradi hiyokujionea maendeleo ya ujenzi wa meli mpya na cherezo pia na ukarabati wa meli za zamani.


Bw. Eric alisema kuwa mradi unatekelezwa na Kampuni ya JV of Gas Entec CO. Ltd Kang Nam Corporation na SUMA JKT ambapo kwa ujumla utagharimu jumla ya shilingi bilioni 152 na tayari Serikali imetoa shilingi bilioni 60 wakandarasi wanadaiwa kazi hawaidai Serikali aidha, mradi umegawanyika katika sehemu kuu nne.



Kwanza ni ujenzi wa meli mpya ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba tani 400 Abiria 1200 ikiwa na urefu wa meta 92.6, urefu kwenda juu meta 11.2 (sawa na ghorofa nne) na upana wa meta 17 na gharama yake ni shilingi bilioni 90.


Mradi wa pili ni ujenzi wa cherezo ambacho kitakuwa na uwezo wa kubeba meli zenye uzito wa tani 4000 ambapo meli mpya itakuwa na uzito wa tani 3500 tu aidha, cherezo kama hicho hakuna katika nchi za Afrika Mashariki na Kati na kikikamilika kitaiingizia Serikali Mapato kama kitatumika kwa kujenga meli zenye uzito mkubwa hasa kutoka nje ya Tanzania. Mradi wa cherezo utagharimu shilingi bilioni 36 na ujenzi wake umefikia asilimia 52.



Mradi wa tatu ni ukarabati wa Meli ya MV Victoria ambao utagharimu shilingi bilioni 22.8 na ukarabati wa meli hiyo umefikia asilimia 50 ambapo inakarabatiwa ikiwa ni pamoja na kubadilishwa mfumo wake wa zamani na kuwekewa mfumo wa kidigitali.



Mradi wa wa nne ni ukarabati wa meli ya Butihama ambapo mradi huo nao utagharimu shilingi bilioni 4.9 na ukarabati wake umefikia asilimia 40.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU