MAVAZI HARAMU

  1. Vazi linalo onesha uchi: Ni wajibu kwa Muislamu kusitiri uchi wake kwa kuvaa nguo, kama alivyosema Allah Mtukufu kuwa: «Kwa yakini kabisa tumekuteremshieni nguo zinazositiri tupu zenu». (Al-aaraaf, aya 26)
Uislamu umeweka mipaka ya kusitiri utupu kwa wanamume na wanawake. Uchi wa mwanaume ni kuanzia magotini mpaka kitovuni mwake. Uchi wa mwanamke mbele ya wanaume wasiokuwa maharimu wake ni mwili wake wote isipokuwa uso na viganja. 
Haifai kujisitiri kwa nguo ya kubana inayo ainisha viungo vya mwili. Pia haifai kujisitiri kwa nguo nyepesi inayo onesha mwili ulio ndani. Kwa sababu hii, Allah amemuahidi adhabu kali mtu ambaye anavaa nguo inayo onesha uchi wake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Aina mbili za watu ni miongoni mwa watu wa motoni» na akataja miongoni mwa watu hao ni: «…na wanawake waliovaa (lakini) wako uchi». (Muslim 2128)
  1. Vazi linalo onesha kujifananisha kati ya Jinsia mbili: Kwa maana kwamba wanaume wanajifananisha na wanawake kwa kuvaa mavazi yanayowahusu wanawake tu, na wanawake wanajifananisha na wanaume kwa kuvaa mavazi yanayowahusu wanaume tu. Jambo hili ni haramau na ni miongoni mwa madhambi makubwa sana. Pia inaingia katika uharamu huu kujifananisha katika namna ya kuzungumza, kutembea na mitikisitiko. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amemlaani mwanaume anayevaa vazi la kike na mwanamke anayevaa vazi la kiume. (Abuudaud, Hadithi Na. 4098). Pia Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amewalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake, na wanawake wanaojifananisha na wanaume. (Bukhariy, Hadithi Na.5546 ). Maana ya laana ni kutengwa na kuwekwa mbali na rehema za Allah. Uislamu unataka umbo la mwanaume na muonekano wake uwe tofauti na mwanamke, na pia unataka umbo na muonekano wa mwanamke uwe tofauti na mwanaume. Hayo ndio matakwa ya maumbile salama na mantiki sahihi.
  1. Vazi linalofanana na vazi la makafiri: Haya ni yale mavazi maalumu ya makafiri, kama mavazi ya watawa na mapadri, kuvaa msalaba na kila kitu ambacho ni alama maalumu ya dini fulani. Ni haramu kavaa vazi hilo. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kujifananisha na watu, basi yeye ni miongoni mwao». (Abuudaud, Hadithi Na. 4031). Sio katika kujifananisha na makafiri Muislamu kuvaa vazi lililoenea katika jamii yake, hata kama wengi wa wanaovaa vazi hilo ni makafiri. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, alikuwa akivaa kama walivyokuwa wakivaa makafiri wa Kikuraishi, isipokuwa tu lile vazi lilokatazwa kwa katazo maalumu.
  1. Vazi linalo onesha kiburi na majivuno: Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Haingii peponi mtu ambaye moyoni mwake kuna chembe ya kiburi».(Muslim, Hadithi Na. 91)
    Na kwa sababu hii, Uislamu umekataza kuburuza nguo na kuzirefusha zikavuka na kuwa chini ya fundo mbili za mguu kwa wanamume, ikiwa kufanya hivyo kunasababisha kiburi na majivuno. Amesema Mtume, swallalahu alayhi wasalam, kuwa: «Mwenye kuburuza nguo yake kwa majivuno na kiburi, Allah hatamuangalia  mtu huyo(kwa jicho la huruma) Siku ya Kiama».(Bukhariy, Hadithi Na. 3465. Muslim, Hadithi Na. 2085) Pia Uislamu umekataza kuvaa vazi la majigambo. Hili ni vazi ambalo mtu akilivaa watu wanamshanga, wanamzungumza yeye tu na kwa hiyo, mvaaji wake anakuwa maarufu kwa vazi ama kwa sababu: vazi hilo ni geni au watu kutolipenda kutokana mtindo wake au rangi yake inayochukiza au kwa sababu vazi hilo linaonesha kiburi na majivuno. Amesema  Mtume, swallalahu alayhi wasalam, kuwa: «Mwenye kuvaa vazi la umaarufu duniani, Allah atamvalisha vazi la udhalili Siku ya Kiama».(Ahmad, Hadithi Na. 5664. Ibnumaaja, Hadithi Na. 3707)
  1. Vazi linalo onesha kiburi na majivuno: Mtume, Allah amfikishie rehema na amani, amesema kuwa: «Haingii peponi mtu ambaye moyoni mwake kuna chembe ya kiburi». (Muslim, Hadithi Na. 91)
    Na kwa sababu hii, Uislamu umekataza kuburuza nguo na kuzirefusha zikavuka na kuwa chini ya fundo mbili za mguu kwa wanamume, ikiwa kufanya hivyo kunasababisha kiburi na majivuno. Amesema Mtume, Allah amfikishie rehema na amani, kuwa: «Mwenye kuburuza nguo yake kwa majivuno na kiburi, Allah hatamuangalia  mtu huyo (kwa jicho la huruma) Siku ya Kiama». (Bukhariy, Hadithi Na. 3465. Muslim, Hadithi Na. 2085)
    Pia Uislamu umekataza kuvaa vazi la majigambo. Hili ni vazi ambalo mtu akilivaa watu wanamshanga, wanamzungumza yeye tu na kwa hiyo, mvaaji wake anakuwa maarufu kwa vazi ama kwa sababu: vazi hilo ni geni au watu kutolipenda kutokana mtindo wake au rangi yake inayochukiza au kwa sababu vazi hilo linaonesha kiburi na majivuno. Amesema  Mtume, Allah amfikishie rehema na amani, kuwa: «Mwenye kuvaa vazi la umaarufu duniani, Allah atamvalisha vazi la udhalili Siku ya Kiama». (Ahmad, Hadithi Na. 5664. Ibnumaaja, Hadithi Na. 3707).
  1. Vazi linalo onesha ubadhirifu na uharibifu: Amesema Mtume, swallalahu alayhi wasalam, kuwa: «Kuleni na toeni sadaka na vaeni bila ya  ubadhirifu wala majivuno».(Annasai, Hadithi Na. 2559) Suala hili linabadilika kwa kutokana na hali na mazingira. Mtu ambaye ni tajiri anaweza kununua nguo ambayo masikini sio sahihi kwake kuinunua nguo hiyo kulingana na fedha zake, pato lake la kila mwezi, hali yake ya kiuchumi na haki nyingine ambazo anapaswa kuzitimiza. Nguo moja inaweza kuwa ni ubadhirifu kwa masikini na sio ubadhirifu kwa tajiri.

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU