MAANA YA TOHARA

Chimbuko la maana ya twahara ni usafi, unadhifu na umaridadi
Allah Mtukufu amemuamrisha Muislamu kuusafisha mwili wake na moyo wake. Ausafishe moyo wake uepukane na vitu dhahiri vya haramu, vitu vibaya na vichafu. Pia ausafishe moyo wake uepukane na Shirki na maradhi ya nyoyo, kama: husda, kiburi na mfundo. Akifanya hayo, atastahiki kupata mapenzi yaAllah, kama Allah alivyosema kuwa: «Kwa yakini, Allah anawapenda wenye kutubu sana na anawapenda wenye kujitwaharisha». (Sura Albaqara, aya 222).
Na Allah ameamrisha kujitwaharisha kwa ajili ya swala, kwa sababu swala ni kukutana na kuzungumza na Allah Mtukufu. Ni suala linalofahamika kwamba mtu anajisafisha na kuvaa nguo zake nzuri sana ikiwa atakutana na mfalme au rais. Hali ikoje basi kwa mtu ambaye anakutana na mfalme wa wafalme aliyetakasika?

Ni ipi twahara inayotakiwa kwa ajili ya swala?

Allah amemuamrisha Muislamu kujitwaharisha kisheria kwa maana maalum kwamba ni amri ya wajibu ikiwa anataka kusali au kushika msahafu au kutufu Alkaaba Tukufu. Pia amefanya Twahara kuwa ni jambo linalopendekezwa katika mazingira kadhaa. Miongoni mwa mazingira hayo ni kusoma Kur’ani bila ya kushika Msahafu, kuomba dua, kulala na mengineyo.

Kujisafisha najisi

  • Najisi ni vitu yakinifu ambavyo sheria imehukumu kwamba ni uchafu na kutuamrisha tujisafishe kwa ajili ya kufanya ibada.
  • Msingi katika vitu vyote ni kufaa kutumika na ni twahara. Najisi ni jambo la kuzuka. Kwa hiyo, tukiwa na shaka ya twahara ya nguo, kwa mfano, na tusiwe na hakika ya kuwepo kwa najisi, msingi ni kwamba nguo hiyo ni twahara.
  • Na tukitaka kusali ni wajibu kwetu kujitwaharisha Najisi katika mwili, nguo na eneo ambalo tunasali.

Vitu najisi ni:

1Mkojo wa mwanadamu na kinyesi chake.
2Damu. Na damu chache inasameheka.
3Mkojo na kinyesi cha kila mnyama ambaye ni haramu kuliwa (Tazama uk. 224).
4Mbwa na nguruwe.
5Wanyama waliokufa. (Makusudio ni wanyama wote waliokufa, isipokuwa tu mnyama ambaye anafaa kuliwa, ikiwa amechinjwa kwa namna ya kisheria. Tazama uk. ……). Ama maiti ya mwanadamu, samaki na wadudu ni twahara.

Kujitwaharisha na najisi:

Katika kuisafisha najisi iliopo katika mwili au nguo au mahali au sehemu nyingine, inatosha Najisi yenyewe kuondoka katika sehemu paliponajisika kwa kutumia nyenzo yoyote ambayo usafishaji umefanyika; kwa kutumia maji au kitu kingine, kwa sababu sheria imeamrisha kuondoa Najisi, na katika kusafisha Najisi hiyo haikuweka idadi maalum isipokuwa tu katika Najisi ya mbwa . (Najisi ya mbwa ni ute wake, mkojo wake na kinyesi chake). Katika najisi hiyo, sheria imeweka sharti la kuosha mara saba, mojawapo ya mara hizo iwe kwa kutumia mchanga. Ama Najisi zilizobaki, inatosha kusafisha najisi yenyewe, na kubaki kwa rangi na harufu hakudhuru, kama Mtume, Allahswallalahu alayhi wasalam, alivyomuambia Swahaba mmoja mwanamke katika kusafisha damu ya Hedhi kwamba: «Inakutosha kuosha damu na wala athari yake haikudhuru». (Abudaud, Hadithi Na. 365).

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU