MAANA YA HIJA ,SHARTI,FADHILA ,NA MASHARTI YAKE

Hija ni kuikusudia Nyumba Tukufu ya Allah kwa ajili ya kutekeleza matukio ya ibada ya hija. Hija ni vitendo na maneno yaliyo nukuliwa kwa Mtume,swallalahu alayhi wasalam, kama vile kunuia (kuhirimia), kutufu katika Alkaaba mara saba, kufanya Saayi(kuzunguka) kati ya vilima vya Swafa na Mar`wa mara saba, kuwepo(kusimama katika viwanja vya  Arafa, kurushia vijiwe minara iliopo Mina na matukio mengineyo.
Katika hija kuna faida na manufaa makubwa kwa waja ikiwemo kutangaza upekee wa Allah (Tawhiid), msamaha mkubwa wa kufutiwa dhambi wanaoupata mahujaji, Waislamu kufahamiana, kijifunza sheria za dini na mengineyo. 

Wakati wa hija

Matukio ya ibada ya hija hujikita kati ya siku ya nane mpaka siku ya kumi na tatu katika mwezi wa Dhul Hijja, ambao ni mwezi wa kumi na mbili katika miezi miandamo katika kalenda ya Kiislamu.

Hija ni wajibu kwa nani?

Ili hija iwe wajibu, ni sharti Muislamu anayebeba majukumu kisheria (Mukallaf) awe na uwezo. Maana ya Muislamu anayebeba majukumu kisheria (Mukallaf), kama ilivyo tangulia kuelezwa, ni mtu mwenye akili timamu, mwenye kubaleghe. 
Maana ya uwezo:
Ni uwezekano wa kufika katika Nyumba Tukufu kwa njia sahihi na za kisheria na kutekeleza matukio ya ibada ya hija bila ya usumbufu mkubwa zaidi ya usumbufu wa kawaida wa safari. Pia kuwepo na usalama wa nafsi na mali, na gharama za mahitaji yake yote ya hija yake yawe  nje ya mahitaji yake ya msingi na nje ya matumizi ya wale wote wanaomtegemea.

Hali za uwezo wa Muislamu wa kufanya hija

  1. Ni yeye mwenyewe kuweza kwenda hija; kwa maana kwamba anao uwezo wa kufika Alkaaba yeye mwenyewe bila ya usumbufu ulio nje ya usumbufu wa kawaida, na kwamba anazo fedha za kutosha kwa ajili ya hiyo. Hapo, itakuwa wajibu kwake kufanya ibada ya hija yaye mwenyewe.
  2. Ni kuwa na uwezo wa kuhiji kwa kumtumia mtu mwengine na sio yeye mwenyewe. Huyu ni mtu ambaye hawezi kuhiji yeye mwenyewe kwa sababu ya maradhi au uzee, lakini anaweza kumpata mtu wa kumfanyia hija, na anao uwezo wa kumpa fedha akamhijie. Atalazimika kutoa fedha kumpa mtu atakayemhijia. 
  3. Ni Mtu ambaye hana uwezo wa kufanya hija yeye mwenyewe na wala kumtumia mtu mwengine. Huyu hija sio wajibu kwake, madamu hana uwezo.Mfano ni mtu ambaye hana fedha zinazozidi mahitaji yake na mahitaji ya familia yake, fedha ambazo zitamtosha kwa ajili ya kufanya hija.
    Halazimiki kuchangisha ili aweze kuhiji, lakini wakati wowote akipata uwezo itamlazimu kwenda hija.

Sharti la Maharimu kwa hija ya mwanamke

Ili hija iwe wajibu kwa mwanamke ni sharti awe na Maharimu. Hija sio wajibu kwa mwanamke isipokuwa tu ikiwa yule anayefuatana naye katika Hija ni mmojawapo wa Maharimu zake.  Maharimu hao ni hawa: Mume au yule mtu ambaye ni haramu kuolewa naye daima kama baba, babu, mtoto, mjukuu, ndugu wa kiume (kaka) na watoto wao, ami na mjomba. (Tazama uk. 246)
Iwapo mwanamke atahiji bila ya kuwa Maharimu kwa namna ambayo atakuwa na amani ya usalama wake, hija yake itakuwa sahihi na itakuwa imetosha.

Fadhila za hijja

Katika hija imeelezwa kuwa kuna Fadhila na kheri nyingi, na miongoni mwake ni hizi zifuatazo:
  1. Hija ni miongoni matendo bora sana. «Mtume,swallalahu alayhi wasalam, alipoulizwa  kwamba: Ni amali gani bora zaidi? Alijibu: ((Ni kumuamini Allah na Mtume wake)). Akaulizwa tena: Kisha ni amali ipi? Akajibu: ((Ni kupigana Jihadi kwa ajili ya dini ya Allah)). Akaulizwa tena: Kisha ni ipi? Akajibu: ((Ni hija yenye kukamilika)). (Bukhari, Hadithi Na. 1447. Muslim, Hadithi Na. 83)
  2. Ni msimu mkubwa wa kusamehewa dhambi. Mtume,swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kuhiji kisha asiseme maneno machafu na asifanye vitendo vichafu, atarudi kama siku alipozaliwa na mama yake». Maana ni kwamba atarudi akiwa hana dhambi kama vile amezaliwa sasa hivi. (Bukhari, Hadithi Na. 1449. Muslim, Hadithi na.1350). 
  3. Ni fursa pekee ya kuepushwa na moto. Mtume,swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakuna siku ambayo Allah humuepusha sana mja na moto katika siku hiyo kuliko siku ya Arafa». Muslim, Hadithi na.1348). 
  4. Malipo ya hija ni Pepo. Mtume,swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hija iliyo kamilika haina malipo isipokuwa pepo tu». (Bukhari, Hadithi Na. 1683. Muslim, Hadithi na.1349). 
    Fadhila hizi na nyinginezo atazipata yule mtu ambaye nia yake ni safi na ya kweli. Pia nafsi yake iwe safi na afuate kwa usahihi mafundisho ya Mtume wa Allah, rehema na amani zimfikie. 

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUSWALI HATUA KWA HATUA

Maana ya kufunga Maana ya kufunga katika Uislamu: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Allah kwa kujizuia na kuacha kula, kunywa, kujamiiana, pamoja na vitu vyote vyenye kufunguza, kuanzia kuchomoza kwa alfajiri –ambao ni muda wa adhana ya Alfajiri- mpaka kuzama kwa jua – ambao ni muda wa adhana ya Magharibi-. «...Basi atakayekuwa katika mji (hayuko safarini) miongoni mwenu katika mwezi (wa Ramadhani) aufunge». Sura Albaqara, aya 185. Ubora wa mwezi wa Ramadhani Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa tisa katika miezi ya mwezi muandamo katika kalenda ya Kiislamu. Ni mwezi bora zaidi katika mwaka. Allah ameuhusisha peke yake kuliko miezi mingine kwa sifa nyingi bora na za kipekee, na miongoni sifa hizo bora ni hizi: Kwamba Ramadhan ni mwezi ambao Allah ameuhusisha na kushuka kwa Qur’ani kitabu kitukufu na bora kuliko vitabu vyote. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani ikiwa ni muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za muongozo na upambanuzi. Basi atakayekuwa mjini miongoni mwenu katika mwezi huu, basi afunge». (Sura Albaqara, aya 185) Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Utakapoingia mwezi wa Ramadhani milango ya pepo hufunguliwa, na milango ya Jahanamu hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo». (Bukhari, Hadithi Na. 3103, Muslim, Hadithi Na. 1079). Hakika Allah ameuandaa mwezi huu kwa waja wake ili waelekee kwake kwa kufanya ibada na kuacha maovu. Kwamba mwenye kufunga mchana wa Ramadhani na akasimama usiku wake (kwa kuswali), Allah humsamehe madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia Mtume amesema kuwa: «Mwenye kusimama (kwa kuswali) katika Ramadhani kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, hadithi na. 1905, Muslim, Hadithi Na. 759). Kwamba ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna usiku wenye hadhi kubwa (Lailatul Qadri), usiku ambao ni bora sana kuliko nyakati nyingine za usiku za mwaka mzima. Allah ameeleza katika kitabu chake kwamba kufanya jambo jema ndani ya usiku huo ni bora zaidi kiliko kulifanya jema hilo siku nyingi nyingine. Allah amesema kuwa: «Lailatulqadri ni bora zaidi kuliko miezi elfu moja». (Sura Alqadri, aya 3). Mwenye kusimama katika usiku huo kwa kuamini na kutaraji kupata malipo ya Allah husamehewa madhambi yake. Huo ni usiku uliopo katika siku kumi za mwisho katika mwezi wa Ramadhani, na hakuna yeyote anayejua tarehe yake kwa uhakika. Ubora wa kufunga «Ambaye hakuacha kusema uzushi na kuutumia hakuna haja kwa Allah katika kuacha chakula chake na kinywaji chake». Kufunga kuna fadhila nyingi ambazo zimeelezwa katika sheria. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo: Kwamba mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Allah, kutii amri zake, kuamini fadhila zake zilizotajwa na sheria na kuwa na matarajio ya kupata thawabu kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyopita. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga Ramadhan kwa kuamini kutaraji kupata malipo ya Allah, husamehewa madhambi yake yaliyopita». (Bukhari, Hadithi Na. 1910, Muslim, Hadithi Na. 760). Pia mwenye kufunga atafurahia malipo atakayoyapata wakati wa kukutana na Mola wake kwa sababu ya funga yake. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mwenye kufunga ana furaha mbili: furaha wakati wa kufungua kwake na furaha wakati wa kukutana na Mola wake». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Peponi kuna mlango unaoitwa Arrayaan. Haingii yeyote kupitia mlango huo isipokuwa tu wenye kufunga. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakika, peponi kuna mlango unaoitwa Arrayyaan. Wenye kufunga wataingia kupitia mlango huo Siku ya Kiama. Haingii yeyote kupitia mlango huo ila wao tu. Patatolewa tangazo kwamba: Wako wapi wenye kufunga? Watasimama. Hataingia yeyote kupitia mlango huo isipokuwa wao tu. Wakishaingia, utafungwa na hataingia yeyote kupitia hapo». (Bukhari, hadithi Na. 1797, Muslim, Hadithi na. 1152) Pia Allah ameyahusisha kwake yeye tu malipo na thawabu za mfungaji. Ikiwa malipo ya mtu yanatoka kwa Mkarimu, Mtukufu, Mtoaji sana na Rahimu sana, anatakiwa ayafurahie yale ambayo Allah amemuandalia. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, katika Hadithi Qudsiy amesema kuwa: «Matendo yote ya mwanadamu ni yake yeye isipokuwa funga. Funga ni yangu, na mimi ndiye nitakaye itolea malipo». (Bukhari, Hadithi Na. 1805, Muslim, Hadithi Na.1151) Hekima ya funga Allah amefaradhisha kufunga Ramadhani kwa hekima nyingi na faida mbali mbali katika dini na dunia, na miongonimwazo ni hizi: Kuthibitisha kumtii Allah na kumuogopa. Hiyo kutokana na kuwa funga ni ibada ambayo mja anajiweka karibu ya Allah kupitia ibada hiyo kwa kuacha anavyo vipenda, na kuyazuia mataminio yake. Anaidhibti nafsi yake kwa kumcha Allah na kumuogopa kila sehemu na kila wakati, katika siri na katika dhahiri. Kwa sababu hii, Allah Mtukufu anasema kuwa: «Enyi mlio amini, mmefaradhishiwa kufunga kama walivyofaradhishiwa waliokuwepo kabla yenu ili mpate kuwa wenye kumuogopa Allah». (Sura Albaqara, aya 183) Mazoezi ya kuacha maasi na madhambi Mwenye kufunga ajizuiapo kufanya mambo yaliyo halali kwa kufuata amri ya Allah atakuwa na uwezo zaidi wa kuyadhibiti mataminio yake ya kutaka kufanya maasi na madhambi, atachunga mipaka ya Allah na hatajiachia katika kufanya maovu. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Mtu ambaye haachi kusema uzushi na kuufanyia kazi, basi Allah hana haja ya kuacha chakula chake na kinywaji chake». (Bukhari, Hadithi Na. 1804). Maana ni kwamba: Mtu ambaye haachi uongo na kufanya uchafu katika kauli na vitendo, huyo hajayafikia makusudio ya funga. Kuwakumbuka wenye shida na kuwasaidia Hiyo inatokana na kwamba katika funga kuna mazoezi ya kupambana na ukata, njaa, na kuwakumbuka maskini ambao wanapambana na hali ya kutokuwa na pato la kutosha siku zote. Kwa kufunga, mja huwakumbuka ndugu zake masikini na namna wanavyoteseka na mambo mawili machungu; njaa na kiu, na kwa sababu hiyo, atafanya juhudi ya kuwasaidia na kuwafariji.

UTUKUFU WA MJI WA MAKKA NA MSIKITI MTUKUFU